Tunawasilisha TZelect: Chombo cha Ushahidi

SN_VijanaFM

Member
Mar 25, 2010
58
0
Source: http://vijana.fm/2010/09/28/tunawasilisha-tzelect-chombo-cha-ushahidi/

Vijana FM inatumia Crowdmap, chombo kilichojengwa na Ushahidi, kukusanya taarifa, mawazo na uzoefu wakati wa Uchaguzi Mkuu Tanzania. Ni matarajio yetu kwamba chombo hiki kitawapa jukwaa watu kutoa taarifa, maoni, kuanzisha mijadala na kueneza ujuzi wa mchakato wa uchaguzi na matukio mbalimbali.





Taarifa zinaweza kuwasilishwa kwa njia tatu:


  1. Kwa kutuma barua pepe: TZelect (at) gmail (dot) com
  2. Kwa Tweeter hashtags #TZelect au #uchaguzitz (Shukrani Jamii Forums)
  3. Kwa kujaza fomu kwenye tovuti
Msisite kuwasiliana nasi mtakapohitaji msaada.


Imetengenezwa na:






___________________________________________


Nyongeza:

Neno "Ushahidi" lina maana yake. Kwahiyo, taarifa ziwe kamili. Na watu wengine wakishuhudia tukio fulani, itakuwa vema na wao wakituma taarifa zaidi (sehemu, mtaa, jimbo n.k.).

Kwa mfano, kama mtu ameacha taarifa ya watu kushindwa kupiga kura kwenye jimbo fulani itakuwa vizuri kama watu wakimsaidia kwa kuongezea mambo (iwe picha, video clip (youtube), au hata taarifa zaidi) -- kuna kitufe cha "kuongezea."

Nawatakia usiku mwema!


 
Moderators, naomba msaada wa kuweka "STICKY" kwenye hii post.

Natanguliza shukrani za dhati.
 
Fanunue zaidi kuhusu chombo hiki kwani wengi hatukielewa vizuri.
 
Sir R,

Mara nyingi watu tumekuwa tukiwategemea waandishi wa habari kutupasha mambo yanayotokea kwenye sehemu mbalimbali. Lakini chombo kama hiki kinawapa watu wote uhuru wa kuripoti yoyote yale yanayotokea mitaani; kubadilishana taarifa n.k. Pia, yanayobandikwa kwenye tovuti yanaweza kuonwa na kila mtu duniani.

Lakini, najua wengi watauliza, mbona hapa JF, blogs na tovuti za Tanzania zinafanya kazi hiyo?

Umuhimu wa chombo kama hiki ni kuwa na ripoti ambazo ni rahisi kuzielewa na kuzitafsiri -- na ramani inasaidia kwa kiasi kikubwa sana kwenye hilo, kwasababu inakupa picha ya sehemu gani hasa zenye matukio na ya aina gani. (Mfano, angalia kwenye tovuti hii:Uchaguzi, ili uone matukio mbalimbali yaliyoripotiwa wakati wa kura za maoni Kenya.)

Kwa kifupi, chombo kama hiki kikitumiwa ipasavyo kinaweza kikawapa wananchi NGUVU ya hoja; na sio kutegemea wahariri au mashirika mengine kutupa ripoti.

Kwa mfano, labda umeona wahusika wanachelewa sana kuhesabu na kutanganza matokeo kwenye kituo chako, unaweza ukaripoti. Na watu wengine wanaweza wakaja kuhakiki uliyosema (inawezekana kufanya hivyo kwenye hiyo tovuti i.e. TZelect). Isitoshe, watu wanaweza kuweka picha na video clips! Kwahiyo ni kama chombo ambacho kinakusanya Ushahidi ambao utatupa picha halisi ya mwelekeo mzima wa uchaguzi au tukio husika.

Muhimu ni hiki: kila mtu ana UHURU wa kuripoti anayoyaona kwenye jimbo au kituo cha kupiga kura.

Nitakupa mfano wa pili ambao utakuelewesha ile "nguvu" ya hiki chombo. Wananchi wanaweza wakakitumia kufuatilia mahesabu ya kura. Hii inaweza ikaanzia kwenye kila kituo cha kupiga kura (yaani watu wakawa wanaripoti matokeo kwenye kila kituo). Hii ikishawekwa kwenye tovuti na watu wengi wakahakiki, itampa mtihani mkubwa sana mtu ye yote mwenye lengo la "kuchakachua" kura, kwasababu wananchi watakuwa wanajua tayari mwelekeo mzima wa Uchaguzi (kwenye kituo au jimbo husika) hata kabla ya NEC (makao makuu) kutumiwa taarifa kamili.

Ukiacha hayo, chombo kama hiki kikitumiwa ipasavyo huwa inapunguza "mizengwe" kwenye vituo vya kupiga kura; kwa kuwa wahusika wanajua kwamba wataanikwa na ulimwengu mzima utaona (unaweza ukaweka hata picha zao!).

Nitaendelea kutoa taarifa zaidi kadri muda unavyoenda... na kuna habari njema kwani wananchi wataweza kuripoti kwa njia ya SMS pia. Kwahiyo hata wa kule vijijini watakuwa na uwezo wa kutupasha yanayotokea.

Naelewa kuwa mtihani mkubwa ni kuelimishana, na hiyo sio kazi rahisi hasa kwa kuwa wahusika hawana access to media powerhouses! Kwahiyo ni jukumu letu kutaarifiana, kuelimishana na kuhakikisha karibia kila mtu awe anajua kutumia hiki chombo: TZelect

Kwa kumalizia (for now), nitakupa mfano wa uchaguzi wa Kenya (2008)... Serikali haikutaka watu nje ya Kenya wajue kilichokuwa kinatokea mitaani. Lakini bahati mbaya au nzuri, taarifa zilikuwa zimeshawafikia watu duniani kote kupitia Chombo cha Ushahidi. Soma zaidi hapa: About Ushahidi

@ Moderators
Sielewi kwanini hii post imeamishiwa kwenye 'Habari na Hoja Mchanganyiko' ilihali ishu ni maalumu kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu? Nafikiri labda mhusika hukuelewa nini hasa matumizi ya hiki chombo...
 
Back
Top Bottom