Elections 2010 Tunataka uchaguzi utupe viongozi wenye maono, siyo wanaotuwekea vipingamizi

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Kumekuwepo na kejeli nyingi za kujeli baadhi ya ahadi zinazotolewa na wagombea wa vyama vya upinzani, hasa hasa Chadema kutoka kwa watu mbalimbali wa kambi ya chama tawala kuwa hizo ahadi ni sawa na ndoto za alinacha.

Wanasema haiwezekani kutoa huduma za elimu na afya bure, hata hivyo jana waziri mwenye dhamana ya elimu aliutangazia umma kuwa kuanzia mwaka 2012 serikali itatoa elimu bure kuanzia awali hadi kidato cha nne. Je hii ilikuwepo kwenye mipango ya awali ya serikali iliyopo? Kama ndiyo mbona hawajatuambia tangu awali? Kama sivyo mbona waliwabeza wapinzani hapo awali kuwa haiwezekani bila hata kufanya utafiti?

Kwa mtizamo wangu naamini kuwa viongozi waliopo, wakiongozwa na Kikwete hawana maono na kwa maana hiyo hawataweza kutuletea mabadiriko tunayoyataka. Kiongozi lazima awe na maono, siyo vipingamizi, bila ya maono meli zinazotoka Lima (Chile) kwenda Miami zingelazimika kupita Rio de Janeiro na kugharimu karibu mara 20 zaidi ya ilivyosasa. Marekani wangekuwa na viongozi wa aina ya Kikwete ingebaki ndoto tu kupitisha meli Panama, ingebaki ndoto pia kupeleka watu angani, lakini leo hii inawezekana na inatokea.

Tunataka viongozi wanaoamini kuwa inawezekana kusafiri kwa reli kwenda Mwanza kutokea Dar ndani ya masaa matatu, kuwa inawezekana watoto wetu kusoma bure, kwamba inawezekana wazazi wetu kutibiwa bure katika vituo vya afya na dhahanati zenye wahudumu, vitendea kazi na madawa.
Hatutaki wale wanaotuwekea vipingamizi, hatutaki wale wanaoamini kuwa ili tuendelee lazima tukaombe misaada Dubai, hatuwataki wale wanaotaka tuamini kuwa Botswana imefika pale ilipo kwa bahati na kwamba sisi hatuwezi kuwa kama wao.

Ikiwa zimebaki siku 4 ninawaomba wapiga kura wenzangu kutumia haki yetu vizuri kwa kuchagua mabadiliko. Ni mwenda wazimu tu anayeweza kutegemea matokeo tofauti kwa kuendelea kufanya yale yale aliyofanya jana na yakamletea matokeo asiyoyapenda,

Uongozi ni kuinua maono ya unaowaongoza juu zaidi, kuinua utendaji wao wa kazi kwenye ngazi za juu zaidi, kujenga maisha ya watu wako kupita matarajio yao, huu ndio uongozi tunaoutaka
 
Tunae sasa Dr.Slaa. Tumchague. Achana na Wababaishaji CCM. Chama cha familia!!
 
Back
Top Bottom