Tunataka nini katika Mswaada wa Sheria ya Kutengeneza katiba mpya Tanzania?

Tunsume

Member
Aug 25, 2008
72
24
Wa-Tanzania wenzangu, serikali imetoa tamko kwamba itakamilisha mswaada wa sheria ya kutunga katiba mpya ya Tanzania hapo April 2011. Sheria hii ni muhimu sana kwani pamoja na mengine, itaainisha mchakato mzima wa kutupatia Katiba endelevu. Tukumbuke kuwa upatikanaji wa katiba ni matokeo ya mchakato. Kwa maana hiyo ni vizuri tuendeleze mazungumzo ya nini tunakitaka kiwemo kwenye mswaada huo wa sheria. Mchakato endelevu pekee ndiyo utakaotupa Katiba endelevu. Ili tupate sheria ya kutunga katiba endelevu tunapaswa kutafuta majibu ya maswali mengi ila mimi nitachangia yafuatayo:
1. Je tunataka tume huru ya namna gani? ya kuundwa na sheria na si kivuli cha wizara ya sheria ama bunge?Tunataka tume huru kutokana na uteuzi wa kamishna wake, majukumu, mamlaka na uendeshaji wake. Kidogo kama tume ya Haki za binaadamu ila iwe ya muda na kuishia pale tuu kura ya maoni itakapohitimishwa
2. Mamlaka ya tume hiyo yawe vipi?
3.Tume ijibu kwa chombo gani- Bunge kwa kupitia kamati ya kudumu ya kutunga sheria ama tuwe na kamati teule ya kusimamia uundaji wa katiba ambapo tume itwajibika kwayo?Ni vizuri tukawa na Kamati teule ya kusimamia utengenezaji katiba ili wajumbe wachaguliwe kutokana na maadili na vigezo vingine vya uwazi, ukweli na uwajibikaji. Ni matumaini yetu itikadi za vyama zitawekwa kando ili tuwe na kamati teule yenye kukidhi mahitaji ya zoezi hili.
4.Je nini majukumu ya Rais katika kusimamia shughuli za Tume ikijumlisha kuteua wajumbe wa tume? Kupitisha/assent hiyo sheria kwa muda muafaka; kupitisha majina ya kamisheni mara baada ya kupendekezwa na bunge
5. Wajumbe wa Tume wateuliweje- na Rais ama kwanza na Tume ya Bunge halafu wapitishwe na Rais?[Uhuru wa tume utapungua kama itateuliwa na Rais kwasababu kwa katiba yetu, Rais anamamlaka makubwa yanayomfanya aogopwe na kila mtu na vyombo vingine vya dola. Huyu mteule wa Rais atajihis anawajibu wa kulinda msalahi ya aliyemteua. Hiyvo basi ni vizuri tumuondolee Rais mamlaka hayo badala yake atayafanya baada ya Bunge na wanachi kufanya uchaguzi na uchunguzi
6. Uwakilishi:
(a) Tume iundwe na watu binafsi ama taasisi/asasi? wote wawe waTanzania ama wengine wawe watu wa nje na kwanini?[Ingawa Kenya walialika watu wa nje kwenye kamati yao ya wataalamu ya kutengeneza katiba, sidhani kama hili ni lazima kwa Tanzania. Hatujagawanyika kiasi hicho kwamba hatuaminiani kiasi cha kuhitaji watu toka nje. Wako wa-Tanzania wasiofungamana na upande wowte wa siasa za vyama ama udini ama ukabila] Ila wawakilishi wawe watu wasiofungamana na upande wowote wa siasa za vyama] Ni vizuri uwakilishi uwe wa watu walioteuliwa ama binafsi, ama na asasi zao lakini uwajibikaji utakuwa wa yule muwakilishi na siyo taasisi yake- Hii itamfanya muwakilishi kusukuma ajenda ya Tanzania na siyo ya taasisi ama kundi lililomteua huyo muwakilishi. Pia itapunguza ushindani wa taasisi kugombea nafasi kwenye kamisheni] Uzoefu wa Tanzania unaonyesha kuwa asasi nyingi za kiraia zinamahusiano ya karibu amam na serikali, ama vyama vya siasa hivyo kuzinyima uwezo wa kuwa huru katika maamuzi yao
(b) Je vyama vya siasa vipewe uwakilishi kwenye tume ama la tutoe sababu?[Binafsi naona tusiruhusu hili, katiba ni ya Wa-Tanzania na siyo vyama vya siasa, Kamisheni inaenda kusimamia kutengeneza katiba vyama vya siasa vitashiriki kama makundi mengine. Ushiriki wa vyma vya siasa utageuza kamisheni uwanja wa mapambano ya itikadi za chama]. Vyama vya siasa vina nafasi ya kushiriki kupitia] wawakilishi wao bungeni.
(c) Je uwakilishi wa dini upewe nafasi kama ndivyo vipina kwanini
(d) Je uwakilishi wa jinsia upewe kipaumbele ama la? [Binafsi naona upewe kipaumbele kwani ni ukweli usiopingika ushiriki wa wanawake Tanzania bado ni changamoto]
(e) Je vijana wapewe nafasi maalumu katika tume?
(f) je Makundi yenye mahitaji maalumu na yaliyosahauliwa kama wenye ulemavu etc wapewe uwakilishi katika tume[uamuzi wa uwakilishi ufanywe bila jazba na juhudi za kukataa ukweli kuwa Tanzania imekumbwa na wimbi la manung'uniko kuhusu kubaguliwa kwa makundi mengine uachwe Tujiulize SUra ya Tanzania ikoje? Hatuko wamoja tuwatu wenye tofauti nyingi na hisia hizo zipo na ni vizuri kama taifa tuzikubali na tuzizungumze na kuzigeuza almasi za maendeleo yetu. Binafsi najivunia Tanzania yangu kwa kuwa inamjumuisho wa watu tofauti na vitu tofauti. Udini unakuzwa kwa kuukana. Kama upo tuuongee na kuangalia jinsi gani tutaubadilisha usiwe tatizo bali rasilimali.
7.Nini ziwe sifa za wawakilishi kwenye tume ya kubadili sheria
(a)elimu na uzoefu (a) elimu (c) uzoefu (d) maadili rushwa (kudhaniwa, kutajwa ama kuthibitishwa, uadilifu (e)
8. Je wananchi wapewe ushiriki wa moja kwa moja katika kuchagua wawakilishi kama watu kuomba na majina kutolewa kwenye gazeti na wananchi kutoa maoni yao na kisha kamati ya bunge teule ama ya kudumu kuyapitia na kuyapeleka kwa Rais kupitisha?[Kama wabunge wetu wangekuwa huru na kuweka maendeleo ya nchi juu ya maendeleo ya vyama vyao tungewakabidhi jukumu hili bunge,kwa vile vyama vyetu vya siasa vimeweka maslahi ya chama mbele, ni vizuri wananchi washiriki moja kwa moja katika kuwachambua wale wanaoomba kuwa kwenye Kamisheni)
9. Je tume iwe na watendaji ama itatumia watendaji wa ofisi ya Bunge? kama ndiyo watendaji hao wateuliweje? na Rais ama na Bunge?[Ili kulinda uhuru wao ni vizuri tume iwe na watumishi wake ambao uteuzi wao utakuwa wa huru na haki]
10. Nini nafasi ya wananchi kuwawajibisha makamishna wa kamisheni hiyo?
11. Nini yawe majukumu na mamlaka ya Kamisheni hiyo?[kuratibu utengenezaji wa katiba ikijumlisha kukusanya maoni ya wananchi kwa njia ya uwazi, ukweli na bial upendeleo; kupokea maoni ya wananchi;jenga hoja ya maeneo makuu ya kuwekwa kwenye katiba mpya na kusanya maoni ya wananchi kuhusu hayo; angalia kero za wananchi na kuangalia jinsi gani katiba itaweka mfumo mzuri wa kuyatatua;toa elimu ya katiba kwa umma ili waweze kushiriki kikamilifu;andika katiba mpya kwa ajili ya kukubaliwa na bunge na hatimaye kupigiwa kura za maoni na wananchi
12. Watatekelzaji majukumu yao haswa kuhakikisha ushiriki wa wananchi katika kutoa maoni ya katiba wanayoitaka?
13. Ukomo wa kamisheni na watamalizaje kazi yao
14. Je Katiba itapitishwa na bunge au kura ya wananchi? Kura ya Maoni Referendum ndiyo iwe hitimisho la kupitishwa kwa katiba mpya na mwisho wa kazi ya kamisheni.
Wengine mnakaribishwa kutoa maoni
 
Kwanza niseme nimefurahishwa na vile vile nimesikitishwa post yako.Nimefurahiswa kwa sababu post yako imekuja wakati muafaka na ina mchango mizuri lakini nimesikitishwa kwamba pamoja ulichoandikia kitu muhimu wakati tunajiaanda kuandika katiba mpya hakuna hata mchango mmoja uliotolew wa kupongeza au kupinga hoja zako.Nidhairi kwamba watanzania ni washabiki wa hoja na mijadara myepesi.

Pamoja nakubaliana na baadhi ya mtazamo wako, ninao mawazo tofauti katika vipengele kadhaa:
1.Nani aandike katiba? - Kwangu mimi kuandika katiba na ambayo ina kidhi matakwa ya demokrasia ya sasa,yenye kugawa madaraka vizuri, yenye kuwaakikishia watanzania haki za binadamu tunahitaji wataalam waliobobea wa katiba, wa utawala, wa haki za binadamu, mifumo ya uchaguzi kutaja chache.Baadhi ya watu hawa tunaweza kuwapata katika baraza la katiba unalolipendekeza lakini shaka yangu ni ufanisi gani tutaupata katika kuandika katiba katika watu 250? Ukizingatia wengi wao watachaguliwa kwa mazingira ya utata?
2.Mimeona ume rejea sheria ya katiba mpya ya kenya ya mwaka 2008.mimi nimeisoma sheria hii, sheria hii inapendekeza katiba kuuandikwa na tume ya wataalam ambao ni tisa (9. Kwangu mimi idadi inaleta ufanisi na majadiliano na masikilizano kuliko kundi la watu 250.vile vile sheria inatamka wazi kwamba watatu kati ya hao wataalam watatoka nje ya Kenya na watakuwa watu wanaoheshimika.
3.Tofauti na Kenya ambako tume ya wataalam iliwasilisha mapendekezo kwa kamati ya kudumu ya sheria ya bunge,na kubaliana na wewe kwamba kwa Tanzanaia hii sio njia muafaka kwa sababu kwamba bunge lilipo halina uhalali. Kwahiyo basi tuunde baraza la katiba ambalo litakuwa inclusive. Kazi ya baraza hili iwe kupitia na kutaka marekebisho ya vipengele katika muswada wa katiba itakayoandikwa na tume ya wataalam na kuupitisha.
4.Baada ya marekebisho ya baraza, tume ya wataalam iandae elimu kwa raia na kuuanda referendum baada ya mswada wa katiba kutangazwa na mwanasheria wa serikali.

Kwa leo naomba niishie hapo
Mungu ibariki Tanzania
0712-266021
 
Abba
Nadhani watu bado wanasubiri hadi Draft Bill itoke ndiyo watachangia.
 
Hapa ndo watanzania tunapokesea. Tuna waamini sana viongozi wetu - mawaziri pamoja na wabunge.lakini kumbukumbu zinatuonyesha kwamba ndo wamekuwa chanzo kikubwa cha matatizo yetu kwa kupitisha maamuzi mabovu ikiwamo mikataba ya madini,sheria mbovu -rejea sheria ya PCCB ambayo inaipa meno na mkono wa kulia na kuinyanganya kwa mkono wa kushoto.naiona hatari ya mswada mbovu tusipo piga kelele sasa!
 
Nadhani kabla ya mtu kuandika lazima kuna mchakato unafanya ndipo inaffikia mahali pale unapoona umekusanya hoja za kutosha ndiyo unaandika, so kuandika ni kitu rahisi. Ugumu upo katika namna ya kupata hoja za kuandikwa katika katiba mpya tunayoipigania, ninaamini, umma wa watz bila kujali hali wakashiriki katika kuandaa nn cha kuandikwa katika katiba mpya, Kenya walifanya hivi na hata ugamnda walifanya sema huku kwa m7 kulifanyika wanachokijua kina m7.
hatuhitaji wanasheria waweke mawazo yao pekee katika uandikwaji wa katiba bali mawazo ya umma wa watz yachukue nafasi ya kwanza na hawa wanaoitwa wataalamu waandike ili kumfanya kila mmoja aweze kusoma na kuelewa
 
Madaraka ya Raisi nimakubwa mno; achague (ateue) mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, waku wa vyuo vikuu, wakurugenzi wa wilaya, miji, manispaa na jiji, wakuu wa Tume ya uchaguzi, wabunge, majaji na mambo mengine mengi yanayoonyesha mlundikano wa madaraka kwa rais hii ni hatari kuna haja ya katiba mpya.
 
Ndugu Obe nashukuru kuendelea kuchangia mada hii muhimu kwa mustakari wa taifa letu.kwanza nimesikitishwa na tamko la ofisi ya wazari wa katiba na sheria kwamba katiba mpya itakuwa tayari 2014!.Hii ni delaying tactics.


Mimi bado naamini katika njia ambayo Kenya walitumia kupata katiba yao.Mtu mwerevu haogopi kunakiri lilo la manufaa.Ili katiba ipate uhalali lazima itimize matakwa mawili: ya siasa na ya kisheria (rejea mada ya prof Shivji). Hili la kisiasa ambalo linahusu ushirikishwaji watu linapaswa liendeshwe kwa weredi mkubwa wa kisheria!sisemi wananchi wasishirikishwe bali washirikishwe baada ya kuwa na draftv0 ambayo imeandikwa na kamati ya wataalamu. Kuchukua njia tofauti ni kukaribisha malumbano ya sio na tija na ni kupoteza muda - ambao haupo. Ni vigumu kwa watu mia tano ambao wanauelewa mfinyu wa maudhui ya katiba kutengeza draftv0. Lakini vile vile katika hiyo kamati ya wataalam ninayopendekeza kuta kuwa na watu ambao watakuwa nuetral na kuweka mizania. Lakini vile vile kamati itaokoa muda!
 
tembelea www.mzalendo.net ili ujue upepo unaelekea wapi

Mimi naona Raisi kuteuwa wajumbe wa Tume sio tatizo. Tatizo ni mamlaka ya Raisi kuteuwa hao wajumbe kutokuwa na vikwazo vya kuhakikisha kwamba kuna checks and balance. Kwa maoni yangu, sheria ingeainisha moja kwa moja kwamba idadi gani ya wajumbe watawakilisha kila vikundi gani katika jamii. Kazi ya Raisi iwe ni kuteuwa wajumbe kwa mujibu wa maelekezo ya sheria. Halafu, baada ya kuteuwa hao wajumbe majina yao yapelekwa Bungeni kwaajili ya kuhidhinishwa.

Ndio nameupata mswaada bado nausoma ntaraji kuchangia zaidi baadae
 
C dhan kama katiba inaitaj muda mref kiac hicho lazima watanzania washilikishwe k kamilifu lazima katiba hi lenge wa2 wote na c tabaka tawala2 licha 2 ya katiba lazima kuwa na taasisi hulu ya kusimamia utekelezwaji wa katiba na isiwe wizala..
 
Back
Top Bottom