Tunataka kuuana kwa ajili ya kitovu cha mtoto

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Nimepata mtoto wiki iliyopita. Mama mkwe wangu, mama yangu na bibi wa mke wangu wote tunagombania kitovu cha mtoto. Hatuongei, nyumba imegeuka uwanja wa matukano.
Waganga wanaletwa eti kumkinga mtoto, niwafukuza, nimeambiwa nitarogwa kama nitaendelea kung'ang'ania kitovu cha mwanangu.
Wana JF naomba mniweke maombini
 
mh!haya mambo haya yana shida haya!hebu mkabidhi mwanao mikononi mwa Mungu
huyo ni mtoto wako na wewe ndo una mamlaka ya mwisho kwa huyo mtoto na wewe ndiye unatoa maamuzi mwanao alelewe vipi!
 
na mwenyewe kesha ukiomba....

Solution hapo ndogo waite wote waambie huwapi kitovu cha mtoto.... Wewe ndo baba utakaa nacho......

Mwisho wa siku kitapotea tu.....

Sie wengine vitovu tuliambiwa tukavifukie tu.......

Hata hivyo kuwa makini vinatumika kwenye mambo ya nguvu za giza vilevile ndo maana nakwamnia usimpe hata mmoja kati yao..na vita vitakwaisha ukiwa firm.....

Halafu waafrica bwana badala ya kuhombea dhahabu tunagombea vitovu
 
https://www.jamiiforums.com/complaints-congrats-advice/333690-kiranja-mkuu-wa-jf.html

uzi huo nadhani uliletwa hapa last week, mara hii mtoto ameleta mtafaruku??
Hebu kuwa mwanaume japo kidogo, tumia meno yako haya kuwang"ata na kuwasambaratisha hao nduguzo wenye silka na hulka za kichawi
avatar21720_3.gif
 
nimepata mtoto wiki iliyopita. Mama mkwe wangu, mama yangu na bibi wa mke wangu wote tunagombania kitovu cha mtoto. Hatuongei, nyumba imegeuka uwanja wa matukano.
Waganga wanaletwa eti kumkinga mtoto, niwafukuza, nimeambiwa nitarogwa kama nitaendelea kung'ang'ania kitovu cha mwanangu.
Wana jf naomba mniweke maombini
mkuu kitovu ni uhai wa mtoto watakuulia mtoto tena kichome moto haraka sana na majivu tupa chooni do it hurry usimpe mtu yoyote yule wanamfanyia uchawi na wanamweka kwenye himaya zao pliz do it frthe sake of the kid pliz atateswa nanguvu za giza bila hatia hata zile nywele kuwa makini choma moto kabisa /ziflash chooni hata hicho kitovu utaanza kuhangaika wewe hospitali na magonjwa yasiyoisha wewe na ukicheza utampoteza mwanao
 
Nimepata mtoto wiki iliyopita. Mama mkwe wangu, mama yangu na bibi wa mke wangu wote tunagombania kitovu cha mtoto. Hatuongei, nyumba imegeuka uwanja wa matukano. Waganga wanaletwa eti kumkinga mtoto, niwafukuza, nimeambiwa nitarogwa kama nitaendelea kung'ang'ania kitovu cha mwanangu. Wana JF naomba mniweke maombini


Wewe binafasi unagombea hicho kitovu cha mtoto ili ukifanyie nini? Inaonekana wazi wote ni magwiji wa uchawi sasa mambo yamewashinda mnaanza kuyaweka hadharani. Mgeukie Yesu ukatubu, achana na mambo ya kishirikina.
 
Nimepata mtoto wiki iliyopita. Mama mkwe wangu, mama yangu na bibi wa mke wangu wote tunagombania kitovu cha mtoto. Hatuongei, nyumba imegeuka uwanja wa matukano.
Waganga wanaletwa eti kumkinga mtoto, niwafukuza, nimeambiwa nitarogwa kama nitaendelea kung'ang'ania kitovu cha mwanangu.
Wana JF naomba mniweke maombini
Pole ndugu na hao majaribu. Kwanza kwanini unaishi na hao ndugu zako wote?? Huwezi kujitegemea?? Huyo mtoto ni wa kwako,kwanini wao ndo wawe na uchungu kuliko wewe?? Usipokuwa imara utasumbuliwa sana na hii dunia. Mkabidhi mtoto kwa mungu na wewe usali sana, pia mpeleke mtoto akaombewe na mama yake pia.
 
Pole Kiranja Mkuu, iyo kitu ipo sana hasa kwa wazazi wetu. Kwanza nakushauri mkabidhi mwanao kwa Mwenyezi Mungu tu, yeye amekupa mtoto na yeye ndiye atakayemlinda mwanao. Wewe kama baba wa mtoto una final say, sio mama yake wala mama mkwe! Waambie ukweli kuwa hutowapa hicho kitovu na kwamba hizo imani zao za kishirikina wewe huzitaki kwenye familia yako. Baada ya hapo kama walikuja kumuuguza mkeo wape nauli warudi kijijini kuangalia nyumba zao na mashamba mana shughuli imekwisha, period!!
 
JF watu kwa NDUMBAA!!! Siwaweziiii! Hadi vitovu dili? Mi nilijua vita ni vya KUGOMBEA MIPEDESHEE TUUU! Hiyo kali! Ila POLEEE!
 
Haya mambo huwa mnayakaribisha wenyewe kwenye familia zenu. Mimi nina shida kidogo linapokuja hili suala la kurundika ndugu nyumbani kwa sababu yeyote ile.

Hivi kujifungua ni ishu saaaana mpk mama mkwe wako, mama yako, bibi wa mkweo na ukoo mzima ujae nyumbani kwako? Mimi navyofahamu, siku za kwanza za maisha ya mtoto ni very delicate, sasa kuchukua wabibi kijijini kuwajaza nyumbani wengine wana magonjwa ya kuambukiza wengine wana harufu za ugoro n.k huko ni kumnyima mtoto haki ya kupata pumzi safi.

Kwa kifupi huo ndio mshahara wa maisha ya kiswahili. Sio mtoto kazaliwa tu hata mwezi hajatimiza basi kila mtu aje kumtia mikono yake, wengine wanga, wengine wana TB, ah jamani, badilikeni. Wafukuze wote bakia na mkeo
 
wanasemaga kila kabila wana mila jinsi ya kuvihifadhi vitovu vya watoto. mimi kwa kweli siamini katika hili na sijawahi fanya lolote kwa vitovu vya watoto wangu na wanaendelea kama kawaida. jambo kuu wewe kama mzazi sasa pamoja na mkeo ni kuhakikisha mnamuweka mtoto wenu kwenye ulinzi wa Mungu, hakuna kitovu wala jina litakalofanya mtoto apate madhala.
Nakumbuka nilipopata mtoto wa 2 baada kama ya wiki 3 hivi mtoto alianza kulia usiku ni balaa, hatulali, unajua niliambiwa kuwa analilia jina, likatumwa jina huko kwenye shina, nikawaambia mtoto tulishampa jina, there is no way akapewa jina sijui la babu zake..... nilichoamua, tulikuwa na rafiki Padre tukamwomba ambatize mtoto. bado kilio kinaendelea, watu wanang'ang'ania jina la babu mimi na mume wangu tunakataa.
siku akaja mama mmoja akaniambia huyu mtoto inawezekana kabisa ni njaa, maana watoto wa siku hizi njaa zinawashika haraka, jaribu kumpa maziwa ya kopo. nikaenda kununua maziwa nikampa ile usiku alipoanza tu kulia, alikunywa, alipomaliza akalala mpaka asubuhi
 
Hivi kumbe bado watu wanaendekeza imani za ajabu mpaka leo!
Muweke mbali mtoto wako na hao wachawi.
 
Wewe binafasi unagombea hicho kitovu cha mtoto ili ukifanyie nini? Inaonekana wazi wote ni magwiji wa uchawi sasa mambo yamewashinda mnaanza kuyaweka hadharani. Mgeukie Yesu ukatubu, achana na mambo ya kishirikina.
mi mwenyewe nimeona hao ni wapinzani wa jadi kwenye ulimwengu wa kiroho, sasa huko ngoma imekuwa nzito ndio anajidai kuja kusaka suluhu huku kwenye ulimwengu wa mwili
 
mi mwenyewe nimeona hao ni wapinzani wa jadi kwenye ulimwengu wa kiroho, sasa huko ngoma imekuwa nzito ndio anajidai kuja kusaka suluhu huku kwenye ulimwengu wa mwili

Ni kweli kabisa. Wakati wake wa kufunguliwa umefika! ashauriwe asiufanye moyo wake kuwa mgumu. ni bora akianza kutusimulia matumizi ya vitovu vya watoto huko kuzimu!
 
Wakristo walio safi na wakweli hata kukumbuka habari za kitovu hatukumbukagi,kama wewe ni mkristo jichunguze una matatizo ktk ukristo wako.
 
Back
Top Bottom