Tunataka akina Dr Slaa wengi bungeni!!

Kama ningeweza kupata wasaa wa kumtaja Mh Mbunge bora wa awamu ya nne ya uongozi wa TZS kwa kipimo cha UKWELI NA UTETEAJI WA MASLAHI YA TAIFA, basi ninge mtaja Dr Slaa. Siyo kwa sababu ni wa CHADEMA, bali kwa namna alivyojitoa kusimama kidete, hata mahala ambapo akili ya mtu asiyejali wengi, angeweka mpira kwapani.

Ninaomba safari hii tusifanye majaribio ya kuchagua viongozi. Udanganyifu wa MAFIGA MATATU waliokuwa wameutumia CCM 2005, usiwapumbaze watu.

Twendeni tusimike wabunge na madiwani kwa ubora wao na si vyama wanavyotoka. Kwa hapo tutajenga akina Dr Slaa wengi.

Excellent thoughts, well done "Sisimizi."
But I doubt if this idea will be digested in a positive way by many of us.
My comrade, I can give you a simple example which happened in 2005 in one the constituency in Lake zone, in day time most of the people were cheering for the upinzani and one of the smart guy came to me for the sake of voting for one of the strong contester, funny enough during the night, the same guy persuade me to vote the strong contester, came to me with some cap and T-shirt of CCM contestant, once I remind him, he ended up saying that he is looking for maslahi.
So if these are the type of people we're living with, do you think that you're splendid thought will be taken into consideration? Absolutely not!!!!!!!!!!!!
 
Watu kama Dr. Slaa ni vigumu kiasi kuwapata/wafahamu. Katika hali ya kawaida ya kuchagua kiongozi, ni rahisi kwa wanaochagua kufuata taratibu au vigezo walivyojiwekea kumpata wanayemtaka. Tatizo linakuja kwa yule aliyechaguliwa kwenda kinyume kabisa na matarajio ya waliomchagua. Mifano iko mingi ya viongozi waliochaguliwa wakiwa na sifa zote kama za Slaa lakini wakashindwa kabisa kufanya anayofanya Dr.
Pamoja na kwamba ni wajibu wetu kujitahidi kadri tuwezavyo kuchagua viongozi kama Slaa, naona kama kuna changamoto kubwa kuweza kuwapata kutokana na mmomonyoko mkubwa wa maadili ya uongozi katika nchi yetu. Watu kama hawa tutawapata tu kwa Neema ya Mungu.
 
Ni kweli huyu Dr. ni mtu anyefanya kazi yake kwa dhati. Mzee pia anauwezo wa kujenga hoja na kuchambua mambo kiuledi hasa. Huwa najiuliza huyu Dr. aliacha upadre illi aende kufanya siasa au alikuwa na sababu nyingine? Kama aliacha upadre ilifanye siasa ni kweli huyu mtu anahitaji support sana, anayodhamira ya kweli ya kuwatumikia watu. Binafsi nitaanza kutafuta historia yake toka aikiwa shule, najua alisoma seminary ya Dungúnyi ambayo nilitokea kufundisha kidogo pale...nitachimbua nione hii spirit yake imeanza lini. Wakati wa bunge, akipewa nafasi Slaa, mimi huacha kila kitu ninachofanya ni msikilize, na sijawhi kukosa kitu toka asemacho!

He is great man. let's give him support.
 
Kama kuna kipindi ambacho Dk Slaa amenifurahisha na kunigusa ni katika Bunge hili na hasa jana na leo katika hoja nyeti..Kwanza kabisa amenifurahisha kwa jana kwenye ripoti ya Richmomd kwa kwake kuendelea kusimamia kile alichokua akikiamini pamoja na kwamba makamanda wenzake waliojiita makamada wa kupinga ufisadi kurudi nyuma.nampongeza sana kwa dhamira yake ya dhati ya kulikomboa taifa hili.Pili amenifurahisha katiba kikao cha leo cha mjadala wa muswada wa gharama za uchaguzi,amejitahidi sana kwa kadiri ya uwezo wake pale ambapo aliona pana walakini..Kwa kweli anastahili pongezi baba wa watu..Huyu ndiye aiana ya viongozi tunaowataka katika taifa hili..Lakini kama mnavyofhamu hodhi ya chama kimoja inasababisha muswada huu kupita.....Hongera sana Dk Slaa,niko kwenye boti yako baba.Jamni hebu tujitahidi tuwaongeze kina Slaa wengine angalau 50 tu...
 
Aombe radhi au ajiuzulu? Ukishindwa kazi usingoje kuomba radhi unabwaga manyanga. JK nchi ilishamshinda siku nyingi basi tu kwa sababu ni Tanzania.
 
Dar kuna waelevu wengi,lakini bado wanamchagua mtu mweny fake 'Phd' ,Makongoro Mahanga.
Sasa kama SISIEM inaweza kutawala majimbo ya Dar,mnategemea vipi huko vijijini,wakati watu wetu wengi huko hawajui nini kinaendelea nchini!Hata neno ufidadi hawajui ni nini.
 
nikiandaliwa naweza kuwa candidate wa kuibeba bendera ya uwakilishi wa uaminifu bungeni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom