Tunarudisha Passport yetu ya Serekali ya watu wa Zanzibar

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1]Azimio la Wazanzibari[/h]Written by Ghalib // 13/10/2012 // Habari // 3 Comments

Azimio la Wazanzibari Waliohudhuria Kikao Cha Kuzungumzia Mustakbal wa Zanzibar, Ukumbi wa Rumaisa Hotel.
13 Oktoba, 2012.
Sisi Wazanzibari tuliohudhuria kikao cha kuzungumzia Mustakbal wa Zanzibar, ukumbi wa Rumaisa Hotel, Malindi baada ya kutathmini hali halisi ya Zanzibar – hususan kuhusiana na uhusiano kati ya Zanzibar na Tanganyika chini ya mfumo wa Muungano wa Katiba wenye muundo wa “Taifa Moja Serikali Mbili”, kama ilivyo hivi sasa na kama ilivyokuwa kipindi cha takriban miaka hamsini; na baada ya kuzingatia umuhimu wa mchakato wa kutafuta katika mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mustakbal wa Zanzibar, na umuhimu wa kuwatafutia haki Wazanzibari kwa kupitia utaratibu wa amani na demokrasia, ambao msingi wake ni mawazo ya walio wengi yanatawala, tunaazimia ifuatavyo:
…
• Kudumisha umoja wetu, na kulinda maridhiano ya Wazanzibari; halikadhalika kugombania maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari bila ya kujali itikadi zetu za kisiasa, kabila, dini, jinsia au umri.
• Kwa kuamini kwamba mfumo muafaka wa uhusiano kati ya Zanzibar na Tanganyika ni Muungano wa Mkataba baina ya mataifa mawili: kujitahidi kwa juhudi zetu zote kuhakikisha kwamba Tume ya Katiba inafahamishwa kwamba wazanzibari wanahitaji Zanzibar yenye mamlaka na madaraka kamili kitaifa na kimataifa, kwa maslahi ya Wazanzibari wote; halikadhalika kuhakikisha kwamba Wazanzibari wote wanafahamu kwamba ni haki yao pekee kuamua hatima ya nchi yao, kwani Zanzibar ni mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa – umoja unaolinda wanachama wote, na mahusiano baina ya wanachamana kulingana na kanuni zake za kidemokrasia, kujitawala, na usawa baina ya mataifa yote bila ya kujali ukubwa au idadi ya watu.
• Kwa kuamini kwamba ni muhimu kuunganisha juhudi zetu: kuimarisha Umoja wa pamoja uliopo Zanzibar unaojumuisha taasisi zote za Wazanzibari zenye lengo na nia moja – kuhakikisha kwamba Zanzibar inatendewa haki na inaendelea kwa manufaa ya Wazanzibari wote; kwani Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulivyoasisiwa Aprili 1964 uliunganisha mataifa mawili huru, na lengo letu ni kuhakikisha ya kwamba Zanzibar inarejesha haki yake ndani ya Muungano wa Mkataba baina ya Zanzibar na Tanganyika ambao utakua ndio mwanzo wa ushirikiano wa kudumu na wenye kuleta faida kwa nchi zetu mbili.
Kwa hali hii huu ni mwito kwa Wazanzibari kuimarisha Umoja wetu, kudumisha amani na utulivu katika nchi yetu, na kuhakikisha ya kwamba harakati zetu za kuitafutia uhuru na maendeleo Zanzibar zinaendelea, kwa niaba ya Wazanzibari wote, na kwa ajili ya maendeleo yetu na usawa na udugu miongoni mwetu.
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar – KWANZA !

www.mzalendo.net

Vidio
Fwd: Kongamano la Katiba Juu ya Mustakbal wa Zanzibar, tarehe 06 Oktoba 2012: Part 1 | Mzalendo.net

Fwd: Kongamano la Katiba, Kamati ya Maridhiano Six: Part 2 | Mzalendo.net

Fwd: Kongamano la Katiba, Kamati ya Maridhiano Six: Part 3 | Mzalendo.net

Kongamano la Katiba, Kamati ya Maridhiano Six: Part 4 | Mzalendo.net

Kongamano la Katiba, Kamati ya Maridhiano Six: Part 5 | Mzalendo.net

Tuasheni tupumue na Zanzibar yetu
Street Food - Zanzibar - 5 Jan 08 - Part 2 - YouTube
 
kWENDA ZENU HUKO SISI HATUITAKI HIYO TANGANYIKA MNAYOSEMA NA HUO MKTABA WENU KAMA HAMTAKI MUUNGANO SI MUONDOKE ZENU.
SISI HUKU NI NCHI MOJA NA TAIFA MOJA TANZANIA UZABAZABINA UISHIE HUKO
 
Nawatakia heri na ningefarijika kama mngeanza kutumia passport zenu kesho.
Tunawakaribisha wageni na watalii bila chuki wala kinyongo ili mradi tu wazingatie taratibu za uhamiaji.

Kila la heri na mungu awasaidie katika mipango ya kurudisha taifa lenu haraka sana.
Lakini si mngeeanza na kuvunja muungano kwanza ili muwe na jeshi lenu, passport, Polisi n.k.
Hamuoni kufanya vitu nusu nusu kunawagharimu muda na pengine pesa?
 
wanajaribu kutumia njia ndefu sana wakati fupi ipo. Sielewi kwanini.
 
Ondokeni hata kesho. Ila baada ya kuwa na passport yenu kuja bara kwa mzanzibar yoyote itakuwa ni tshs 2,000,000/= kwa kukaa kwa muda wa siku 5. Itakuwa ni marufuku kuondoka na chakula chochote.yeyote aliye somea zanzibar asiruhusiwe kufanyakazi huku bara.
 
wanajaribu kutumia njia ndefu sana wakati fupi ipo. Sielewi kwanini.

wanatikisa kiberiti hao.wavunje muungano waone watakapo haha kutafuta chakula,ajira kwao hakuna,hizo biashara ya mi used items watauza wapi wakati kwao ni masikini watupu.watakuwa wanaangaliana tu na kubwia madawa ya kulevya tu. kuna mtu ana hamu ya kukaa na wafuga ndevu.
 
Ondokeni hata kesho. Ila baada ya kuwa na passport yenu kuja bara kwa mzanzibar yoyote itakuwa ni tshs 2,000,000/= kwa kukaa kwa muda wa siku 5. Itakuwa ni marufuku kuondoka na chakula chochote.yeyote aliye somea zanzibar asiruhusiwe kufanyakazi huku bara.

Mkuu maneno yako hayana busara.. msome MMJ alivyojibu.
 
Mkuu maneno yako hayana busara.. msome MMJ alivyojibu.
ujue kwanini nimewajibu hivyo? ni kwasababu wazanzibar wanadhani watu wa bara wanafaidika zaidi na uwepo wa muungano kuliko wao,kumbe wao ndio wanaofaidika zaidi in terms of say AJIRA,FURSA ZA BIASHARA,WANASIASA WAO WENGI AJIRA ZAO ZIKO BARA n.k. watu wenye akili zetu hatuwezi kupoteza muda kujadili kitu ambacho kiko wazi hivyo.uliona wapi wazanzibar wako mil 1.7 kwenye bunge la muungano wapo wabunge zaidi ya 60!! wakati wasukuma wote wako zaidi ya mil 17 wana wabunge wasiozidi 20.je hapo kuna haki??
 
mimi nadhani mwenye jukumu la kuvunja muungano ni wao wenyewe,naona wanazunguka mara mkataba mara maazimio ,inabidi waondoke kelele haziishi watu tuna mambo mengi ya kujadili kama ajira,kilimo nk.
 
mkjj mchonganishi upo ? kuna uzi umeanzishwa na mchambuzi nenda kapate elimu dunia. alau ujifunze somo la justice and balance

Vipi, Shain yupo pamoja nanyi?
Hebu watumeni hao wabunge wenu wachumia tumbo kuja kuleta motion kwenye bunge la JMT tuone itakuaje.

Msiwe kama mwanamke malaya anayetafuta kupewa talaka, analeta ukorofi wa mambo madogomadogo kila siku.
 
kWENDA ZENU HUKO SISI HATUITAKI HIYO TANGANYIKA MNAYOSEMA NA HUO MKTABA WENU KAMA HAMTAKI MUUNGANO SI MUONDOKE ZENU.
SISI HUKU NI NCHI MOJA NA TAIFA MOJA TANZANIA UZABAZABINA UISHIE HUKO
Kha! Nchi yako huitaki, maajabu! We pumbavu kweli :banghead:
Wewe kweli mchovu.

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
 
Last edited by a moderator:
Ondokeni hata kesho. Ila baada ya kuwa na passport yenu kuja bara kwa mzanzibar yoyote itakuwa ni tshs 2,000,000/= kwa kukaa kwa muda wa siku 5. Itakuwa ni marufuku kuondoka na chakula chochote.yeyote aliye somea zanzibar asiruhusiwe kufanyakazi huku bara.

Sijawahi kwenda KENYA nkalipia milioni 2, nishakwenda kenya na nikapita boda na msosi wangu, kama hujui katika vyuo vya zanzibar wapo wabongo, katika mashule zanzibar ndio mumejaa kama mlotumwa vile, hujatutisha bado :-D
 
wanatikisa kiberiti hao.wavunje muungano waone watakapo haha kutafuta chakula,ajira kwao hakuna,hizo biashara ya mi used items watauza wapi wakati kwao ni masikini watupu.watakuwa wanaangaliana tu na kubwia madawa ya kulevya tu. kuna mtu ana hamu ya kukaa na wafuga ndevu.

Umechangia katika jukwaa na wewe hongera! Zanzibar kabla ya muungano kwani ilikuwa inapata wapi chakula? Hivi kujiona mko karibu na visiwa ndo mnajiona kiwa tuna njaa ya vitu kutoka kwenu? Vitu vinavyotoka kwenu vinafaida gani? Hebu nambie, mi naona ivo vitu ghali kuliko ukiagizia nje! Huijui zanzibar wewe na porojo zako, apo zamani vyakula zanzibar vinatoka bara la ASIA vinakuja apa na hei inakuwa poa mara 1000 kuliko yenu! Eti biashara ya used, wazanzibar ndo wenye biashara weweeeee!!!afu kuna wazenji wanahela chafu wapo uko wanakutunzeni msiokuwa na shukrani nyieee,,,,, nikuulize wewe hivi dunia nzima kuna mtu anahamu ya kukaa na WALEVI,WAVUTA BANGI,WASIOJUA MAANA YA USTAARABU,WAPENDA STAREHE,WATEMBEA UCHI NA WALIOKOSA HAYA NA HESHIMA?

Bado hujasema kitu ndugu
 
Hakuna haja ya matangazo, just do it! Au wanatishia waone kama kuna mtu atawazuia?

Hii inanikumbusha darasa la nne, watoto wawili wanagombana, mmoja anajidai kakasirika sana lakini anaishia kusema "nishikeni, nitampiga huyu mtu".

Passport ni sehemu ndogo, muhimu ni kutangaza Zanzibar taifa huru, mengine yatafuatia.
 
Ondokeni hata kesho. Ila baada ya kuwa na passport yenu kuja bara kwa mzanzibar yoyote itakuwa ni tshs 2,000,000/= kwa kukaa kwa muda wa siku 5. Itakuwa ni marufuku kuondoka na chakula chochote.yeyote aliye somea zanzibar asiruhusiwe kufanyakazi huku bara.

hawa wapum..vu tuwatreat kama wakongo na wanigeria wanaokuja Tanganyika. hamna hiztoria ya undugu wala preferential treatment yeyote. hamna kazi huku bara wala kusoma huku bure, kufanya biashara kwa vibali maalumu vya wawekezaji na walipe work permit na kue na quota ya wangapi waruhisiwe kuingia nchini..hamna undugu na watu wasio na shukhrani, wabinafsi na wapenda mizozo. tuelekeze nguvu zaidi kwenye majirani wenye potential siyo hivi vichuguu kwenye bahari.
 
Back
Top Bottom