Watanzania tunapenda na tumekubali kudanganywa(?)

Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
182
Je watanzania wanapenda kudanganywa?
Je watanzania ni wavivu kweli wa kufikiri?
Je watanzania hawana uwezo wa tenganisha ukweli na uwongo?

Nimesukumwa na hasira kuleta maswali haya, baada ya kusoma kwenye gazeti moja kuhusu ndoto mpya ya Raisi Kikwete. Ndoto yenyewe inahusu mpango wa serikali (ambao tayari umekamilika) wa kumwezesha kila mwalimu katika nchi hii kuwa na laptop yake, katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Hivyo ndivyo serikali inapanga vipaumbele.
Laptop kwa mwalimu wa Iponyaholo, Bulungwa, Ushetu kwa mfano itamsaidia nini?
Laptop kwa mwalimu asiye na nyumba imara itaitunza wapi?
Laptop kwa mwalimu ambaye bado hajafunza matumizi yake?
Ni Laptop isiyotumia umeme?
Laptop itachangia asilia ngapi katika kuboresha elimu?
Hivi kumbe tatizo kubwa la walimu wetu ni ukosefu wa computer?

Binafsi naelewa kuwa hiyo ni siasa tu ya kutafuta kura za walimu. Lakini swali ni je walimu wetu wanapenda kudanganywa? Kwanini mtu atumia a very cheap lie kuwanasa walimu? Maana yake viongozi wetu wanajua kuna tatizo la ujinga na uvivu wa kufikiri na kutenganisha uwongo na ukweli.

Mimi naona "Tanzania beyond tomorrow" kama inavyoitwa ndoto hiyo ya Raisi ni tusi kwa walimu wetu na kwa watanzania.

Nafikiri tunahitaji wakina "Kamau" wengi na "matusi" yao.
 
Si Watanzania tu, watu karibu dunia nzima wanapenda kusikia uongo mzuri zaidi kuliko ukweli mbaya.Sema inawezekana huko kwetu tumezidi.

Watu wangetaka ukweli tu mbona dini zingekosa waumini, na watu kibao wangekosa wake.
 
Ha ha ha!Veri funi but ukweli mtupu!Maisha bora kwa kila mtanzania....Inasikitisha sana tu.....Ila sisi nadhani tatizo letu ni kusahahu mapema,hatuwawajibishi warongo.
 
Mtu superstaa kama kanumba,kuwa kwenye tangazo la product ambayo ni mbaya.si o kwamba anaharibu reputation yake jamani? Mimi namshauri hawashtaki hawa jamaa kwa kudanganya public
vingamuzi gani hata kuwaka haviwaki? Sekunde 2 kimezima.craaaaaaaaaaaaaap
refer startimes advertisment.
 
Hivi Kanumba na yeye ni Superstar?
nakushauri utumie DSTV maana hayo mambo ya Star times yatakuja kua kama ya GTV
 
hivi kanumba na yeye ni superstar?
Nakushauri utumie dstv maana hayo mambo ya star times yatakuja kua kama ya gtv
nshakitupa kwenye dustbin siku nyingiiii ni vile naona watanzania wenzangu wanaendelea kudanganywa roho inauma
 
nshakitupa kwenye dustbin siku nyingiiii ni vile naona watanzania wenzangu wanaendelea kudanganywa roho inauma

roho isikuume bana, unajua watanzania always tunapenda vya bure, hivi unapata Channel za kulipia kwa shilingi 9000 kwa mwezi halafu ukienda DSTV bei ya chini ni sh 29,000. hiyo inaingia akilini?
mimi hua nawacheki tu watu ambavyo hua wanaingia mkenge, Bi mkubwa alikinunua katumia siku 9 kikawa kinazingua akipiga simu customer care full usumbufu, akaamua kupotezea, akaenda DSTV mambo poa bila chenga ingawa kulipa 87,000. kwa ajili ya entertainment tu hapa Bongo ni ishu.
 
roho isikuume bana, unajua watanzania always tunapenda vya bure, hivi unapata channel za kulipia kwa shilingi 9000 kwa mwezi halafu ukienda dstv bei ya chini ni sh 29,000. Hiyo inaingia akilini?
Mimi hua nawacheki tu watu ambavyo hua wanaingia mkenge, bi mkubwa alikinunua katumia siku 9 kikawa kinazingua akipiga simu customer care full usumbufu, akaamua kupotezea, akaenda dstv mambo poa bila chenga ingawa kulipa 87,000. Kwa ajili ya entertainment tu hapa bongo ni ishu.
hata kama ni elfu 2 ni hela.kwanza wanaibia nchi hawa wachina viongozi wetu tu hawajui ni ufisadi huu
 
hata kama ni elfu 2 ni hela.kwanza wanaibia nchi hawa wachina viongozi wetu tu hawajui ni ufisadi huu

mbona wenyewe vifaa vyao hapa ni bomba sana,yaani huu ni mwaka wa 2 sasa natumia lakini sijapata usumbufu wowote ule,ila hiki changu nimenunua mwenyewe china,sijui nyie mnaoibiwa na watz,poleni sana
 
mbona wenyewe vifaa vyao hapa ni bomba sana,yaani huu ni mwaka wa 2 sasa natumia lakini sijapata usumbufu wowote ule,ila hiki changu nimenunua mwenyewe china,sijui nyie mnaoibiwa na watz,poleni sana
heri yako bwana.sijui niwapeleke mahakamani??
 
Kauli ya Mhe.Mahiga na kauli iliyotolewa EU zinatoa picha ya aina ya viongozi au jamii tuliyonayo..nadhani yapo mambo mengine hatupaswi kuhoji ukweli ni upi! Yapo mambo serikali inaweza kuamua kukaa kimya kuepusha misuguana kwenye jamii...yapo mambo imefika wakati Kama taifa tuyaone yanalichafua taifa letu.....mtu mwenye mawazo tofauti siyo adui yetu Bali anapaswa kutupa mshawasha wakufanya vizuri zaidi...
 
Umesema ukweli. Hata huko bungeni unasikia mtu analalamika halafu akipatiwa majibu unasikia anaanza “ninashukuru kwa majibu mazuri ya waziri.....” kwa kuwa tu kaahidiwa waziri atazuru jimboni. Na tatizo hilo hilo litasemwa tena mwaka ujao na ujao! Mara nyingi tumekuwa wepesi kuamini maelezo yanayotolewa na viongozi wa serikali. Hata katika press conference - waandishi wa habari hawana nia wala maarifa ya kuuliza mambo ya msingi yaliyokinzana. Hili jambo litatuumbua!!
 
Hata katika press conference - waandishi wa habari hawana nia wala maarifa ya kuuliza mambo ya msingi yaliyokinzana. Hili jambo litatuumbua!!
Naunga mkono hoja.
Kiukweli sisi waandishi ni sehemu moja muhimu inayolikwamisha taifa, waandishi tunapoalikwa press conference, hatuulizi maswali magumu, tunauliza maswali mepesi na kupewa majibu mepesi, ukijumlisha na zile bahasha zetu za takrima, ndio basi tena.
P.
 
Tukiconclude TZ ni taifa la wajinga tutakosea???
 
HILI HAPANA.

Kilichotokea leo uwanja wa Taifa sio haki, sio heshima kwa wajasiriamali. Yapaswa Serikali kutoa kauli kuhusu hili lililotokea.

Wajasiriamali wameujaza uwanja wa Taifa leo baada ya kutangaziwa kuwa kutakuwa na mikopo kuanzia 500,000/-

Watu wamedamka asubuhi, wamepigilia suti za maana. Kufika kule hakuna cha mkopo wala nini badala yake ni tamasha la dini. Sio haki kabisa hii.

Waliowaongopea wadanganyika wawajibishwe haraka
 
Heee! Kweli vyuma vimekaza. Hivi unawezaje kuambiwa njoo uwanja wa Taifa upate mkopo kirahisi namna hiyo na kweli uamini? Labda hii serikali ilitaka kupima Watanzania wanadanganyika kirahisi kiasi gani ili waendelee kuwadanganya kirahisi!
 
Back
Top Bottom