Tunaopenda CCM yaweza kuwa Dogma

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,006
2,166
Wale mulio na elimu ya saikolojia, kuna hilo neno dogma.
Vijana wengi tuliozaliwa enzi za CCM hatukuwahi kusikia ubaya wa CCM sawa na jinsi ambavyo wengi hatujui ubaya wa wazazi wetu kabla ya kuzaliwa.

Mtu akisema mama yako bwege, Hiyo ni vita. Hutaki kusikia hilo ingawa mabwege pia huzaa!

Sasa hawa tulioamini kwamba CCM ni nambari wani kweli si rahisi kuamini kwamba ni hakuna kitu. ni dogma. Huko chamani kwetu kwa kweli hatuna jipya tena na ndo maana tunaishia kusema kama baba wa Taifa alivyosema ....

Baba wa Taifa is dead but still thinking on behalf of the living!
 
Una uhakika gani na hili ? CCM ilizaliwa mwaka 1977. Una uhakika kuwa vijana wengi waliozaliwa baada ya 77, hawaujui ubaya wa CCM ??
 
Wale mulio na elimu ya saikolojia, kuna hilo neno dogma. Vijana wengi tuliozaliwa enzi za CCM hatukuwahi kusikia ubaya wa CCM sawa na jinsi ambavyo wengi hatujui ubaya wa wazazi wetu kabla ya kuzaliwa.

mmh.. sasa nani kakuambia "dogma" inahusiana na Saikolojia? ungegoogle kwanza.... vinginevyo ungesema tu kwa wale walio na "elimu ya sisiemulojia" wangeweza kukuelewa tu.
 
Wale mulio na elimu ya saikolojia, kuna hilo neno dogma.
Vijana wengi tuliozaliwa enzi za CCM hatukuwahi kusikia ubaya wa CCM sawa na jinsi ambavyo wengi hatujui ubaya wa wazazi wetu kabla ya kuzaliwa.

Mtu akisema mama yako bwege, Hiyo ni vita. Hutaki kusikia hilo ingawa mabwege pia huzaa!

Sasa hawa tulioamini kwamba CCM ni nambari wani kweli si rahisi kuamini kwamba ni hakuna kitu. ni dogma. Huko chamani kwetu kwa kweli hatuna jipya tena na ndo maana tunaishia kusema kama baba wa Taifa alivyosema ....

Baba wa Taifa is dead but still thinking on behalf of the living!

Kata issue Mchunguzi...Najua wana CCM waelewa mko njia panda sasa hivi...Siwashauri muame chama bado...Bado kitambo kidogo tutajua wapi pa kwenda na Nani ni nani na ana/wanataka nini.
 
Ndoto za mchana kweupe hizi.

Hakuna hasiyeyajuwa mabaya ya CCM, wala mabaya haya hayakuanza leo, wala wabwabwaji wa mabaya ya CCM hawakuanza leo.

CCM itaendelea kushinda chaguzi na kadhalika itaendelea kuvurunda uchumi wa nchi na maisha ya wananchi, hadi hapo tutakapokuwa na chama cha upinzani. Kuyasema mabaya ya CCM kila kukicha kamwe hakumwondoi mtanzania katika lindi la umaskini bila ya kuwa na chama madhubuti kitakachompa mwananchi alternative.

Tatizo sio CCM, tatizo ni watanzania. Hawana substitute ya CCM. CUF, chama ambacho kina nguvu kule visiwani kimegeuka mtaji wa wachache. Kiongozi wake mwenye dira ya ufalme ameapa maisha kugombea urais kwa gharama zozote. Kwake demokrasia lazima iwe baina ya vyama na si ndani ya chama chake. Kwake usafi wa kikombe sio ndani bali nje. CUF bara ni dhaifu mno kiasi cha kudhoofisha nguvu za kisiasa za mwenyekiti wake wa taifa, chanzo cha udhoofu huu hakitakiwi kujadiriwa na wala udhoofu huu hauchochei maswali juu ya mwelekeo wa CUF kwa ujumla.

Chadema, chama ambacho kingeleta matumaini nacho kimegeuka kichekesho kwa mwananchi wa kawaida. Ukabila umejikita vilivyo, viwango vya elimu cha viongozi wake wakitaifa ni mushkiri, viongozi wake badala ya kwenda vijijini kuanzisha matawi wanakesha JF 24/7 kana kwamba kura za JF zinatosha kukipa Chadema madaraka. Hotuba za bunge badala ya kuwafikia wapiga kura wa vijijini zinaletwa JF. Vijijini kwenye wapiga kura wengi, helkopta ya kiongozi inaonekana tu wakati wa kampeni.

Kwa maoni yangu wapinzani wametuangusha na wataendelea kutuangusha kwa kushindwa kwao kuwapa wananchi substitute ya CCM. Tz hatuhitaji wapinzani wa kuleta upinzani kwa CCM, bali upinzani wa kuing'oa CCM madarakani, that is what we need. Leo hii wapinzani wetu wameridhika kuwa kama mbwa anayebweka kila mwizi anapokuja hali akijuwa ni bosi wake tu ndiye anayeweza kumshika mwizi huyo. So at the end of the day mbwa ataendelea kubweka hata kama mwizi anayembwekea ni mtoto wa bosi wake. Upinzania lazima uwe wa kuing'oa CCM, upinzani wa kuorodhesha mafisadi wa CCM kila kukicha kamwe hautaleta maendeleo.

CCM inafungua matawi India, Chadema na CUF hazina tawi Tz kote. Leo hii wapinzani tunasema CCM kitanzini? Tunapata wapi nguvu hizi? Headlines za magazeti bongo yanayoongozwa na wapinzani zimejaa shutuma za CCM na serikali yake, kana kwamba wizi huu umeanza leo, hivi isingekuwa jambo la maana magazeti ya wapinzani yakawa yanaandika juu ya kuundwa kwa matawi ya vyama vya upinzani katika strongholds za CCM na mikakati ya ushindi 2010?

Tulichobakiwa wapinzani ni dua za bata (wala sio za kuku) na CCM wanajuwa hilo fika. Kama fisi wa mwituni tunakesha tukiomba mkono wa binadamu ung'oke tupate mlo, pasipo sisi kufanya jitihada zozote kuung'oa. Wapinzani tumewaangusha wananchi 100%, hatujawapa option.
 
Mwizi siku zake arobaini. CCM inatumia fedha ambazo viongozi wake wanawaibia wananchi kufungua matawi hata nje. Inatumia viongozi wa serikali ubalozini (ambao hawapashwi kuwa wana CCM) kufanya shughuli za kupanua chama. Mwaka 2005, CCM iliiba mabilioni ya shilingi za wananchi, toka BoT, ili kuhonga ishinde. All of these are llegal activities.

Si kweli kwamba hakuna Chama Mbadala. Mbona Zambia na Kenya vilitokea vyama kama vya kwetu vya upinzani na kushinda uchaguzi?

Kama hakungekuweko na wizi wa kura, mwaka 1995 CCM Bara ingewekwa benchi na Mrema, na CCM Visiwani ingewekwa benchi na Maalim Sharif Hamad. Sasa siku za mwizi zinahesabiwa. Siku za CCM zinahesabiwa sana.

You can fool some of the people some of the time, but you cannot fool all the people all the time!
 
ukinambia watu wazima wengi wa vijijini ndo hawajui mabaya ya ccm ndio ningekubali. na hapo bado ningetia shaka kidogo.
ccm haina wafuasi wengi kihivyo. wizi wa kura, kutumia pesa nyingi sana kwa kampeni za kuhonga wapigaji kura ndio hasa vinavyokifanya chama kisonge mbele.
ukitupilia hivyo chini, ccm leo isingekuwa na nguvu zaidi ya chadema cuf tlp na kadhalika.
 
Tulichobakiwa wapinzani ni dua za bata (wala sio za kuku) na CCM wanajuwa hilo fika. Kama fisi wa mwituni tunakesha tukiomba mkono wa binadamu ung'oke tupate mlo, pasipo sisi kufanya jitihada zozote kuung'oa. Wapinzani tumewaangusha wananchi 100%, hatujawapa option.

Very interesting!
 
Sasa wewe kama mpinzani mmojawapo una mpango gani wa kurekebisha hali hii? au ndio umekubaliana na hali hiyo?
 
Una uhakika gani na hili ? CCM ilizaliwa mwaka 1977. Una uhakika kuwa vijana wengi waliozaliwa baada ya 77, hawaujui ubaya wa CCM ??

korosho,
Ni hayo hayo niliyofundishwa huko CCM. Ukibanwa unaamua kuuliza 'una hakika?' Ki-elimu hakuna haja ya kuuliza swali kama hilo, Ila kama hujui, una uliza zaidi. Sema nipe maelezo ya ziada.

Zakia Megji ilijidai anajua uchumi kuliko mpinzani yeyote. Eti atapandisha bei ya mafuta bila kuathili mambo mengine. Alipobanwa alijibu hivyo hivyo, 'hawana hakika'

Where are we now!
 
Back
Top Bottom