Tunaondoa watumishi hewa au serikali haina pesa?

Ninyi mnaompinga Yeriko mmeajiwa? Huku kwetu ni lazima kusaini sheet fukani hivi kabka ya tarehe 20 yenye majina yako yote unayotumia kazini, na check number na vikorombwezo vingi tu ili ipelekwe hazina. Kama mfumo wa lawson haujauliwa ni kwanini tusainishwe hiyo fomu? Yeriko ana hoja na sio mnatuambia habari za fiekd zenu ambazo hamruhusiwi kuyajua ya ndani kwa kina. Endelea kutuhabarisha bwana Yeriko.
 
Labda hatuelewani tu. Mifumo kama LAWSON na mingineyo hutumia 'key'-namba/neno unique kutunza taarifa. Hiyo key hutumika kutambulisha na kutafuta kumbukumbu. Hivyo mchezo upo kwenye key, sio majina. Lazima ucheze kwanza na key ndipo ufananishe jina. Sasa loophole ya key ni rahisi kugundulika, hasa kama key ni namba ya form four.

Kwa taasisi kama RITA ni ngumu zaidi maana lazima utunze kumbukumbu hata za wale ambao hawajaenda shule. Maana yake key inabidi iwe random au sequential number ambazo ni rahisi kucheza nazo. Nadhan ni wakati muafaka kila raia awe na namba inayomtambulisha kama ilivo social security number kwa USA-hapo angalau tunaweza kudhibiti kwa kiasi fulan.
Unaposema Key number unamaana namba ya Cheti, hapo tayari NECT umeihusisha mkuu
 
Ninyi mnaompinga Yeriko mmeajiwa? Huku kwetu ni lazima kusaini sheet fukani hivi kabka ya tarehe 20 yenye majina yako yote unayotumia kazini, na check number na vikorombwezo vingi tu ili ipelekwe hazina. Kama mfumo wa lawson haujauliwa ni kwanini tusainishwe hiyo fomu? Yeriko ana hoja na sio mnatuambia habari za fiekd zenu ambazo hamruhusiwi kuyajua ya ndani kwa kina. Endelea kutuhabarisha bwana Yeriko.
Wengi wanaopinga si watumishi wa umma bali wanapinga kwa hisia zao tu
 
Kuna ndugu yangu alikua Mwalimu ila akawa anatumia cheti kimoja na mtu mwingine yupo wizara nyingine ila mwaka Jana wakashtukiwa wakafungiwa mishahara yao wote wawili,kwahiyo itakua huo mfumo wa LAWSON ndo uliwatambua au?
 
Iko hivi jamani,
Baada ya kuonekana hili suala ni tata kidogo serikali imeamua haya.
Kwanza kugawa vitambulisho vya taifa kwa raia wote na vitambulisho hivyo vitakuwa nataarifa zote za muhusika ikiwemo
Vyeti vyote vya kitaaluma, kitambulisho cha kupigia kura, cheti cha kuzaliwa na finger prints.
Kwa hiyo hili zoezi litaanzia kwa watumishi wote wa umma tarehe 3 October. Litadum kwa wik 2 .
Hivyo hizo data za NIDA, NACTE na RITA zitakuwa linked.
Hapo mtoto hatumwi sokoni baba.
Hapo hata wakibaki ni wa kuhesabu.
Tuache uchochezi tuisapoti serikali inapojitahidi kuweka mambo sawa
 
Kuna uwezekano mkubwa kuwa ni kweli
 
Honestly mimi na familia yangu namchukia Jpm kutokana na hili la ajira, hata kama atafanya jema kiasi gani as long as mimi wadogo zangu tunamaumivu ya ajira hatuwezi kuona.

Kila siku danadana tu utadhani sisi sio binadamu kama yeye.
Bora aturudishe kazini tu kuliko kufuata ushauri wa hao wanaomwambia aendelee na uhakiki
 
Umeniwahi mkuu, hii kitu alioiandika yeriko ni sababu moja kati ya zaidi ya kumi zinazotumika kwenye uhakiki wa watumishi hewa thats why wanasema inabidi kabla ya kihukumu tu make sure tume fanya analysis ya pande zote ndio tuanze shutuma
maana kuna watumishi hewa wanatumia majina tofauti
kuna wale waliofariki lakini bado wapo kwa payrol
kuna wale walioenda kufanya kazi private sector lakini bado wapo kwa payrol ya gvt
kuna wale waliojifanya wameendakusoma but wanafanya kazi sehemu nyingine but still wapi kwa payrol ya gvt
yaani ni maeneo mengi sana ya kugusa kwahio ningeshauri tuiache serikali ifanye kazi yake
na ww uko kwenye kiyoyozi ndio maana huangalii wengine. ungekua unalia njaa kama wenzako au husomi shuleni kwa kukosa mwalimu wakati walimu wako mtaani, usingeandika huo ushabiki.

hivi swala la kuajiri na kuondoa watumishi vinahusiana vipi? kwanini yy anateua wakumsaidia kazi? kama hataki kuajiri, basi angeacha hata kuteua wakumsaidia na kazi zote akafanya yeye. angechoka mpaka mkia. nadhani machungu ya kuchoka kwa kufanya kazi zote kwasababu ya kutoweka wasaidizi wakati wasaidizi wako mtaani bila kazi, yangekua sawa na machungu ya watoto wetu walioko shuleni na kuacha kusoma wakati walimu wako mtaani na hawana kazi au machungu yetu sisi wanyonge tunaopata huduma hafifu hospitalini kutokana na uhaba wa wataaalamu wakati wataalam wapo mtaani na hawana kazi.

mimi naona huyu Magu angeajiri tu. watumishi wote wapya wangefanyiwa uhakiki pindi wanaingia ktk ajira. muajiri gani ataongeza majina ya watumishi ktk hawa wapya wakati idadi inayojulikana imetoka wizarani na wizara zote zina ajina na idadi halisi? swala la kusema 'anasitisha ajira ili kupisha uhakiki' linafanana na kama angesema 'anawasimamisha watumishi wote wa uma kupisha uhakiki wa watumishi hewa', kwani hatuwezi kuendesha uhakiki huku tukiwa tunawalipa mishahara watumishi kwani na hewa watalipya pia. kipi kibaya kitatokea iwapo ataajiri wataofika na kufanyiwa uhakiki kwanza?
mimi sijaona sababu madhubuti ya kusitisha ajira.
 
Acha wanyooshwe kwa kukaa mitaani waliwachagua wenyewe.acha waisome namba
 
Iko hivi jamani,
Baada ya kuonekana hili suala ni tata kidogo serikali imeamua haya.
Kwanza kugawa vitambulisho vya taifa kwa raia wote na vitambulisho hivyo vitakuwa nataarifa zote za muhusika ikiwemo
Vyeti vyote vya kitaaluma, kitambulisho cha kupigia kura, cheti cha kuzaliwa na finger prints.
Kwa hiyo hili zoezi litaanzia kwa watumishi wote wa umma tarehe 3 October. Litadum kwa wik 2 .
Hivyo hizo data za NIDA, NACTE na RITA zitakuwa linked.
Hapo mtoto hatumwi sokoni baba.
Hapo hata wakibaki ni wa kuhesabu.
Tuache uchochezi tuisapoti serikali inapojitahidi kuweka mambo sawa
Umebebwa umewekwa hapo unapigwa kiyoyozi unaongea kirahisi tu.wenzako wanaopigwa jua mitaani huwajali.binadamu acha ubinafsi kwa nini ufaidike peke yako?acha na wenzako wapate ajira dada.
 
Yeriko unapotosha sana watu kwa mfano uliotoa. Hakuna mfumo duniani unaoweza kutumia majina kama 'primary key' kwenye database. Huo ni upotoshaji mkubwa sana kwa wanaoelewa database design. Kwa maoni yangu, naamini primary key ya database ya wafanyakazi wa serikali inapaswa kuwa namba ya mtihani ya form four. Namba ya mtihani ya form four ni unique na karibu kila mwajiriwa wa serikali amehitimu form four. Hivi ndivyo database ya HESLB inavyofanya kazi na naamin hata hiyo LAWSON inafanya kazi namna hiyo. Huwezi kuzuia majina ya watu kufanana kwa kuwa watu wengi hutumia majina mawili badala ya matatu na tumekuwa na kasumba ya kutumia majina ya kizungu-hivyo sio ajabu kuwa na akina Janeth Joseph watano ktk database moja na wote wakawa wafanyakazi halisi. Kinachowatofautisha na kuwatambulisha ni namba yao ya mtihani ya kidato cha nne tu.

Kumbuka namba ya mtihani ya kidato cha nne ina 1)serial namba ya mwanafunzi, 2) namba ya shule na 3)mwaka aliofanya mtihani. Wakati 1 na 2 zitafanana kwa watu wawili wa miaka tofauti, 3 itawatofautisha maana hiwezekan wanafunzi wawili wakapewa serial namba moja kwa mwaka mmoja wa mtihani. Watu wote waliokuwa wanatemwa na LAWSON sababu ilikuwa namba ya mtihani kidato cha nne. Hata ukitaka kucircumvent, trick iko hapo. Tumia namba ya mtihani ya mtu ambaye hayupo serikalin-japo yaweza kugundulika kama namba ya kwenye cheti ni tofauti na iliyoingizwa kwenye system. Wapigaji wote wa HESLB walikuwa wanacheza na namba ya kidato cha nne.

Upotoshaji kama huu ndio unafanya rais atamani malaika waifungie mitandao ya kijamii maana watu mnaaelezea vizuri kana kwamba mnajua technicalities kumbe kuna upotoshaji mkubwa.
sasa kama swala ni namba ya form four tu, huu muda wote unaokaribia mwaka ndio unaotumika kutambua namba halali za form four! tunajua walikagua vyeti, sasa zile namba zilizokuepo kwenye system wakati hazikutokea wakat wa uhakiki siwalizitoa haraka! kama swala lilikua ni hilo tu, basi zoezi lilishaisha na sasa wanaendesha zoezi la kuwapatia watumishi wa umma vitambulisho vya taifa. sasa kama zoezi la sasa ni kuwapatia watumishi vitambulisho vya taifa, kwann wasiajiri ili na hawa wapya wakavipata tu.
hakuna sababu ya kuzuia ajira huku wanafunzi hawasomi ktk shule zote za wanyonge (sio shule wanazosoma watoto wao), pia watumishi hospitalini ni hwachache (sio hospitali wanazotibiwa wao na watoto wao). kila siku wao wanasain makaratasi ya kupanda ndege kwenda kutibiwa nje ya nchi, mara india, mara ujerumani, sisi huku tunataabika ktk hospitali zetu zenye upungufu wa watumishi huku watumishi wapo na hawaajiriwi.

ama kweli pesa ya kununulia ndege ili wapande wao wenye hela ipo, ila haipo ya kuajiri walimu watufundishie watoto wetu na wataalamu wa afya wakutuhudumia.
 
Mimi nimefafanua jinsi mfumo unavyofanya kazi. Nampinga Yeriko kwa kupotosha jinsi mfumo unavyofanya kazi. Hayo mengine siwezi kuyazungumzia maana sina uhakika nayo.
 
Mimi nimefafanua jinsi mfumo unavyofanya kazi. Nampinga Yeriko kwa kupotosha jinsi mfumo unavyofanya kazi. Hayo mengine siwezi kuyazungumzia maana sina uhakika nayo.
tunakuomba utoe neno kuhusu uhalali au uharamu wa kuzuia ajira kupisha huu unaoitwa uhakiki. plz mkuu
 
Honestly mimi na familia yangu namchukia Jpm kutokana na hili la ajira, hata kama atafanya jema kiasi gani as long as mimi wadogo zangu tunamaumivu ya ajira hatuwezi kuona.

Kila siku danadana tu utadhani sisi sio binadamu kama yeye.

Bora aturudishe kazini tu kuliko kufuata ushauri wa hao wanaomwambia aendelee na uhakiki
huyu babu nimeanza kupishana nae kabisa. mwanzo nilikua namuamini, ila kwa hili la kutesa watu, namchukia kwasasa
 
yeye aliisoma namba kipindi cha kapeni,aliongea kila lugha lakini hakueleweka,alipiga push up lakini mkawa viziwi..sasa na nyie ni zamu yenu kuisoma namba,kunena kwa lugha zote hadi mkome...HAPA KAZI/AJIRA HAKUNA!!.
 
Na je kama ulimpa mtu cheti akaingilia serikalini alafu akawa amepata kitambulisho cha uraia kupitia hicho cheti cha form four na anatumia jina lako kwenye hicho cheti cha uraia,na amesha acha kazi serikalini,na kama Mimi niliye mpa hicho cheti nataka vitambulisho cha uraia kwa sasahivi nitapata kweli?
 
ulimpa mtu cheti chako!!!
ww ulikua mpiga dili, mm nasema utaisoma namba. ngoja wengine waje wakupe ushauri.
 
tunakuomba utoe neno kuhusu uhalali au uharamu wa kuzuia ajira kupisha huu unaoitwa uhakiki. plz mkuu
Hili jambo ni chungu sana kwa wanaotafuta ajira. Napenda kuamini serikali ina sababu zake za kusitisha ajira. Kwasababu sina taarifa za kina, nitakuwa msomaji na mtazamaji tu.
 
Ni kwamba serikali haina bajeti ya mwaka huu kuongezeka kwa increments za mishahara. Mishahara kupandishwa ni mwakani.
 
Back
Top Bottom