Tunaondoa watumishi hewa au serikali haina pesa?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Zoezi la kuhakiki watumishi lilianza baada tu ya serikali hii kuingia madarakani, hatua hii ilikwenda sambamba na kusimamisha ajira nchini, kupandishwa madaraja na mambo kadha wa kadha yanayohusu sekta ya ajira nchini.

Lakini hebu tuangazie kwa undani juu ya sekta ya utumishi wa umma nchini na namna ilivyokuwa ikifanya kazi kabla na baada ya zoezi hili linalochukua nusu mwaka sasa na bado linaonekana ni zoezi endelevu lisilo na kikomo huku hakuna dalili ya ajira kufunguliwa.

Utawala wa awamu ya nne kama sehemu ya kudhibiti na kuongoza sekta ya utumishi wa umma, uliamua kwenda Uingereza na kununua mfumo maalumu wa kudhiti watumishi wa umma nchini unaofahamika kama LAWSON kwa mabilioni ya shilingi za kitanzania.

LAWSON, maana yake ni HUMAN RESOURCE CAPITAL MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM
(HRCMIS)

Huu ni mfumo mzima unaoratibu na kudhibiti rasilimali watu ndani ya utumishi wa umma, kwa maana ya mtu abaki na cheque number moja tu, kudhibiti upandaji wa madaraja kiholela au kupeana vyeo hovyo hovyo, mfano huwezi kuteua mtu toka mtaani moja kwa moja na kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri au DAS wakati hajawahi hata kuwa mtumishi wa umma na kupitia ngazi mbalimbali za seniority au ukuu wa idara kama sheria inavyotaka.

LAWSON katika kudhibiti watumishi hewa inafanya kazi zaidi ya moja, mtumishi wa umma siku ya kwanza kabisa anapoajiriwa katika wiza au tasisi yoyote ya umma jina lake linapelekwa wizara ya utumishi kwenye Database (mfumo) iitwayo LAWSON, hapo unafunguliwa akaunti yako itakayokutambulisha kwamba wewe ni mtumishi wa umma mfano mwalimu wa shele ya msingi.

Akaunti yako hii ndio itakuwa utambulisho wako hata upokeapo mshahara, na LAWSON imeweka ukomo wa Akaunti, kwamba kila mtumishi nchini atakuwa na akaunti mmoja tu hata ungehama wizara na idara, bado akaunti yako utakayotumia kupokea mshahara itatambulika ile uliyosajiriwa nayo siku unaanza kazi serikalini.

Sheria ya utumishi wa umma inataka kwamba, mtumishi wa umma anapohama wizara, mfano ulikuwa Mwalimu (wizara ya Elimu) halafu ukahamishishwa kwenda wizara Kilimo, basi aliyekuwa na mamlaka kuidhinisha taarifa zako kuhamishwa kwenye LAWSON ni Katibu mkuu Kiongozi na sio vinginevyo.

Sasa watumishi wa hewa walipatikanaje? Kuna namna nyingi zinazizalisha watumishi hewa, Watumishi waliofariki majina yao kutoondolewa na akaunti zao kuendelea kulipwa mshahara, Watumishi walioacha kazi akaunti zao kuendelea kulipwa nk, na vitendea kazi vya kuzaa mtumishi hewa ni vingi kuanzia, RITA, NECTA na Afisa uajiri mhusika na lililorahisi ni la kugonganisha majina lakini ukitofautisha herufi moja tu, na kwa bahati mbaya nyaraka ngumu (hard copy) za ajira huishia kwa afisa uajiri tu hivyo ni rahisi kupeleka kwenye LAWSON nyaraka laini (soft copy) zauongo.

Mfano wa hili la kugonganisha majina, Database hii majina yakiingiliana au ukiingiza jina ambalo tayari lipo kwenye database itakataa kulipokea, Kilichokuwa kinafanyika nikwamba maafisa uajiri ndio walikuwa na uwezo wakutengeneza mtumishi hewa,

Mfano mimi Yericko Yohanesy Nyerere nimeajiriwa serikalini leo (wizara ya starehe na mambo ya huzuni), sasa Afisa wangu uajiri anataka kutengeneza mtumishi hewa, anachofanya ni kupeleka majina mawili, Yericko Yohanesy Nyerere na Yeriko Yohanesi Nyerere.

Hao ni watu wawili tofauti, yupo mtu halisi na yupo mtumishi hewa (ghost) na wote anawasilisha akaunti zao za benki, akaunti moja ataimiliki yeye ile ya mtumishi hewa lakini hapo mwenye nyaraka halisi atakuwa mmoja tu, Hapa LAWSON haitawakataa itawapokea na kuwasajiri kama watumishi wa umma.

Lakini ni ukweli zoezi hili la kuzalisha watumishi hewa linahitaji umakini sana, na utatuzi wake (kuwaondoa) linahitaji umakini mara mia, kosa dogo tu linaweza kuliangamiza taifa letu.

Database hii mpaka leo hakukuwa na mtanzania wa kawaida anayeweza kuiendesha bali mtu binafsi (Mhindi) ndie peke yake mwenye uwezo wakuiendesha tangu ilipofungwa hapa Tanzania.

Serikali hii ya awamu ya Tano ilipoingia tu, katika opareheni yake ya kuondoa watumishi hewa, inaonekana kama imeachana na matumizi ya database hii, na kurejea kwenye mfumo wa zamani, kuna kila dalili kwamba sasa afisa uajiri wa Wilaya ya Nanyumbu anayo mamlaka ya kukuajiri na kukufukuza bila kikwazo cha makao makuu. Hili linaleta shaka na kuaminisha kuwa mfumo huo haupo tena kwasababu ya uajiri wa haraka wa Wakurugenzi na makatibu tawala wa Wilaya waliongia kwenye utumishi wa umma toka uraiani kinyume na utaratibu unavyotakiwa. Kwa lugha rahisi nikuwa Lawson ingekataa majina yao kwakuwa hawajawahi kuwa kwenye utumishi wa umma na kuongoza vitengo/idara kama sheria inavyotaka.

Kinachoweza kuzuia kwasasa mtumishi hewa asizalishwe ni nidhamu ya uoga iliyotengenezwa tangu Rais Magufuli aingie madarakani, lakini kwa mfumo huu wa sasa ikatokea leo hii Magufuli akaondoka, basi taifa linaweza kuelemewa na watumishi hewa, mlango wakuingilia upo wazi.

Hakukuwa na sababu za msingi za kusimamisha ajira na mambo mengine kwasababu tu ya hili zoezi, labda serikali iueleze umma kwamba inashughuli nyingune nje ya hili.

Katika hili Serikali inaweza kuingia hasara kubwa kwa pande mbili, kwenye oparesheni ya uhakiki, au baada ya uhakiki wakajikuta wamezalisha watumishi hewa mamilioni bila kutarajia. Kwakutumia mfumo uleule uliozaa watumishi hawa hewa, serikali ilikuwa na uwezo wakuondoa hao watumishi hewa bila kuathiri shughuli zingine za uajiri na mengineyo.

Ilikuwa ni mtu mmoja tu yule muhindi kumwambia a search majina yote yanayofanana kwenye LAWSON kisha serikali kwakutumia vyombo vyake ijipe muda wakumuita mtumishi mmoja mmoja mmoja na kumuhoji juu ya ajira yake, kama ni hewa bila shaka hatatokea, atapotelea hewani tu.

Zoezi hili hivi sasa limeleta athari kubwa katika sekta mbalimbali ambapo serikali itaingia hasara mara mbili au zaidi. Mfano mdogo ni sekta ya afya..

Madaktari waliokwisha kumaliza mazoezi ya vitendo (internship) miaka miwili iliyopita na wale waliomaliza mwaka huu. Pia kuna madaktari waliomaliza vyuoni mwaka huu wanaotakiwa kuanza hayo mazoezi ya vitendo (internship) mapema tangu mwezi wa nane lakini bado hawajaanza.

Kuna utaratibu wa kuomba nafasi kupitia mtandao wa baraza la madaktari la Tanganyika, (Tanganyika medical council, utaratibu huo ulifunguliwa kwa siku tatu tu ili watakaowahi wapate nafasi. Ambao hawajaomba ndani ya siku hizi tatu, labda hawakuwa na taarifa au hawakuwa na nyaraka zote zinazohitajika mara moja, hao inawezekana imekula kwao. Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wa baadhi ya madaktari waliomaliza vyuo mwaka huu wasifanye 'internship' kwa sababu serikali ama haina pesa ya kuwalipa ama bado zoezi hili linaathiriwa na oparesheni ya watumishi hewa, ama serikali inabana matumizi.

Na ieleweke kuwa Daktari bila kufanya internship haruhusiwi kutibu na hata ajira zingine kwake ni deiwaka tu kwa sababu cheti cha 'nternship' kutumika kwenye maombi ya ajira.

Hii ni moja ya athari za namna ya kushughulikia tatizo la watumishi hewa, kimsingi lilikuwa tatizo dogo na wala lisingetangazwa kwa nguvu au kutumika kama alama ya nguvu za kiutawala.
 
Not every system is perfect, so most likely kulikuwa na loopholes watu wakaziexploit.
Therefore ni kweli in the beginning there might have been watumishi hewa, ila its obvious wameendelea kutumia kigezo hicho hicho kwa mambo mengine pia kwa vile hawana hela.
 
Upo sahihi.../ hapa nguvu tele akili kiduchu.
•katika kusimamisha ajira wapo sahihi kwa 100%.maana,bila kusimamasha actual base wataipataje?/
 
Zoezi la kuhakiki watumishi lilianza baada tu ya serikali hii kuingia madarakani, hatua hii ilikwenda sambamba na kusimamisha ajira nchini, kupandishwa madaraja na mambo kadha wa kadha yanayohusu sekta ya ajira nchini.

Lakini hebu tuangazie kwa undani juu ya sekta ya utumishi wa umma nchini na namna ilivyokuwa ikifanya kazi kabla na baada ya zoezi hili linalochukua nusu mwaka sasa na bado linaonekana ni zoezi endelevu lisilo na kikomo huku hakuna dalili ya ajira kufunguliwa.

Utawala wa awamu ya nne kama sehemu ya kudhibiti na kuongoza sekta ya utumishi wa umma, uliamua kwenda Uingereza na kununua mfumo maalumu wa kudhiti watumishi wa umma nchini unaofahamika kama LOWSON.

LAWSON, maana yake ni HUMAN RESOURCE CAPITAL MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM
(HRCMIS)

Huu ni mfumo mzima unaoratibu na kudhibiti rasilimali watu ndani ya utumishi wa umma, kwa maana ya mtu abaki na cheque number moja tu, kudhibiti upandaji wa madaraja kiholela au kupeana vyeo hovyo hovyo, mfano huwezi kuteua mtu toka mtaani moja kwa moja na kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri au DAS wakati hajawahi hata kuwa mtumishi wa umma na kupitia ngazi mbalimbali za seniority au ukuu wa idara kama sheria inavyotaka.

LOWSON katika kudhibiti watumishi hewa inafanya kazi moja tu, mtumishi wa umma siku ya kwanza kabisa anapoajiriwa katika wiza au tasisi yoyote ya umma jina lake linapelekwa wizara ya utumishi kwenye Database (mfumo) iitwayo LOWSON, hapo unafunguliwa akaunti yako itakayokutambulisha kwamba wewe ni mtumishi wa umma mfano mwalimu wa shele ya msingi.

Akaunti yako hii ndio itakuwa utambulisho wako hata upokeapo mshahara, na LOWSON imeweka ukomo wa Akaunti, kwamba kila mtumishi nchini atakuwa na akaunti mmoja tu hata ungehama wizara na idara, bado akaunti yako utakayotumia kupokea mshahara itatambulika ile uliyosajiriwa nayo siku unaanza kazi serikalini.

Sheria ilitaka kwamba, mtumishi wa umma anapohama wizara, mfano ulikuwa Mwalimu (wizara ya Elimu) halafu ukahamishishwa kwenda wizara Kilimo, basi aliyekuwa na mamlaka kuidhinisha taarifa zako kuhamishwa kwenye LOWSON ni Katibu mkuu Kiongozi na sio vinginevyo.

Sasa watumishi wa hewa walipatikanaje? Database hii majina yakiingiliana au ukiingiza jina ambalo tayari lipo kwenye database itakataa kulipokea. Kilichokuwa kinafanyika nikwamba maafisa uajiri ndio walikuwa na uwezo wakutengeneza mtumishi hewa,

Mfano mimi Yericko Yohanesy Nyerere nimeajiriwa serikalini leo (wizara ya starehe na mambo ya huzuni), sasa Afisa wangu uajiri anataka kutengeneza mtumishi hewa, anachofanya ni kupeleka majina mawili, Yericko Yohanesy Nyerere na Yeriko Yohanesi Nyerere.

Hao ni watu wawili tofauti, yupo mtu halisi na yupo mtumishi hewa (ghost) na wote anawasilisha akaunti zao za benki, akaunti moja ataimiliki yeye ile ya mtumishi hewa. Hapa LOWSON haitawakataa itawapokea na kuwasajiri kama watumishi wa umma.

Lakini ni ukweli zoezi hili la kuzalisha watumishi hewa linahitaji umakini sana, na utatuzi wake (kuwaondoa) linahitaji umakini mara mia, kosa dogo tu linaweza kuliangamiza taifa letu.

Database hii mpaka leo hakukuwa na mtanzania wa kawaida anayeweza kuiendesha bali Mhindi mmoja hivi (kilema) ndie peke yake mwenye uwezo wakuiendesha tangu ilipofungwa hapa Tanzania.

Serikali hii ya awamu ya Tano ilipoingia tu, katika opareheni yake ya kuondoa watumishi hewa, ikaachana na matumizi ya database hii, na kurejea kwenye mfumo wa zamani, Sasa afisa uajiri wa Wilaya ya Nanyumbu anayo mamlaka ya kukuajiri na kukufukuza bila kikwazo cha makao makuu. Kinachoweza kuzuia kwasasa mtumishi hewa asizalishwe ni nidhamu ya uoga iliyotengenezwa tangu Rais Magufuli aingie madarakani, lakini kwa mfumo huu wa sasa ikatokea leo hii Magufuli akaondoka, basi taifa linaweza kuelemewa na watumishi hewa, mlango wakuingilia upo wazi.

Hakukuwa na sababu za msingi za kusimamisha ajira na mambo mengine kwasababu tu ya hili zoezi, labda serikali iueleze umma kwamba inashughuli nyingune nje ya hili.

Katika hili Serikali inaweza kuingia hasara kubwa kwa pande mbili, kwenye oparesheni ya uhakiki, au baada ya uhakiki wakajikuta wamezalisha watumishi hewa mamilioni bila kutarajia. Kwakutumia mfumo uleule uliozaa watumishi hawa hewa, serikali ilikuwa na uwezo wakuondoa hao watumishi hewa bila kuathiri shughuli zingine za uajiri na mengineyo.

Ilikuwa ni mtu mmoja tu yule muhindi kumwambia a search majina yote yanayofanana kwenye LOWSON kisha serikali kwakutumia vyombo vyake ijipe muda wakumuita mtumishi mmoja mmoja mmoja na kumuhoji juu ya ajira yake, kama ni hewa bila shaka hatatokea, atapotelea hewani tu.

Zoezi hili hivi sasa limeleta athari kubwa katika sekta mbalimbali ambapo serikali itaingia hasara mara mbili au zaidi. Mfano mdogo ni sekta ya afya..

Madaktari waliokwisha kumaliza mazoezi ya vitendo (internship) miaka miwili iliyopita na wale waliomaliza mwaka huu. Pia kuna madaktari waliomaliza vyuoni mwaka huu wanaotakiwa kuanza hayo mazoezi ya vitendo (internship) mapema tangu mwezi wa nane lakini bado hawajaanza.

Kuna utaratibu wa kuomba nafasi kupitia mtandao wa baraza la madaktari la Tanganyika, (Tanganyika medical council, utaratibu huo ulifunguliwa kwa siku tatu tu ili watakaowahi wapate nafasi. Ambao hawajaomba ndani ya siku hizi tatu, labda hawakuwa na taarifa au hawakuwa na nyaraka zote zinazohitajika mara moja, hao inawezekana imekula kwao. Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wa baadhi ya madaktari waliomaliza vyuo mwaka huu wasifanye 'internship' kwa sababu serikali ama haina pesa ya kuwalipa ama bado zoezi hili linaathiriwa na oparesheni ya watumishi hewa, ama serikali inabana matumizi.

Na ieleweke kuwa Daktari bila kufanya internship haruhusiwi kutibu na hata ajira zingine kwake ni deiwaka tu kwa sababu cheti cha 'nternship' kutumika kwenye maombi ya ajira.

Hii ni moja ya athari za namna ya kushughulikia tatizo la watumishi hewa, kimsingi lilikuwa tatizo dogo na wala lisingetangazwa kwa nguvu au kutumika kama alama ya nguvu za kiutawala.
Hatari sana hii kitu kama ni kweli ulichoandika
 
Kuna vitu vingi sana tunafichwa!! alafu akiwa jukwaani sasa anavyotoa povu daaahh!! vijana kazi hawana alafu wanaenda chukua walimu wa sayansi marekani.

Na kuna uwezekano hata yeye anataka kupiga panga. LAKINI TUKISEMA HAWANA HELATUNAKUA TUNAKOSEA, KAMA HAWANA HELA MBONA WAMENUNUA PANGABOI? MBONA WANAJENGA UWANJA WA NDEGE?
 
mm naona ni presha tu ya wateule pamoja uoga walio nao, mm ni miongo mwa watu ambao tulishawahi kufanya project hii ya LOWSON, iko very simple and workable, ila baadae serikali iliamua kuagiza huo mfumo nje...
na inawalipa wahind mamilion ya pesa, kuusimamia, kuufanya maintance, repair, kuimpliment, na kuongeza functionalities kwa kadili ya maitaji, jambo ambalo wapo watanzania wenye uwezo mkubwa wa kufanya hivyo

bado serikali inaendelea kutumia garama kubwa, kutoa seminer kwa kila afisa utumish wa umma, na baadhi ya watuimish wa umma, hata wale waliokuwa hawezi kubonyeza button moja ya kompyuta, ili kuweza kuutumia huu mfumo ile hali wana mafisa tehama kwenye idara zao....

namshauri rais, hili zoez wanaoendelea nalo, linawapa watu fursa ya kutengeneza mianya mingne ya kupiga pesa za uma, garama zinazotumika ni bora, akaturudisha kazin vijana wenye uwezo tuliosimamiswa kupisha zoez hili tukawajibike kuliko kuendelea kutaabika mitahani na kuona rais juhudi zake ni kama kuendelea kutukandamiza sisi wtot yatima..

mifumo ya kompyuta haiitaji nguvu nying na rasilimali pesa nying kuufanyia monitoring, zaid hinaitaji securty na backup with highly integrity and consistency...

hayo ya ziada ni watu kutafuta umaarufu usio na tija na kugharimu taifa, hao wanaomwambia rais zoez liendelee wamepata mianya ya kutengeneza pesa zao, kwa mgongo wa zoezi la watumish hewa
 
Watumishi hewa wapo kwa namna nyingi sana.Hilo la kufananisha majina ni moja tu.

Kushuhulikia tatizo hili kwa assumption kuwa wote ni wa namna moja tu ya kufananisha majina litawaacha watumishi hewa wengi sana.

Kwamba kama wewe ni mtumishi hewa na jina lako sio la mfanano kwenye system uliyoitaja wala hautaguswa
 
Upo sahihi, lakini mimi nimeweka hiyo kama njia tu moja rahisi ya kuanzia
 
Tumuachi mwenyewe ataamua japo kuna maumivu sana asa kwa vijana ambao serikali iliwaajiri na kuwasimamisha
 
Zoezi la kuhakiki watumishi lilianza baada tu ya serikali hii kuingia madarakani, hatua hii ilikwenda sambamba na kusimamisha ajira nchini, kupandishwa madaraja na mambo kadha wa kadha yanayohusu sekta ya ajira nchini.

Lakini hebu tuangazie kwa undani juu ya sekta ya utumishi wa umma nchini na namna ilivyokuwa ikifanya kazi kabla na baada ya zoezi hili linalochukua nusu mwaka sasa na bado linaonekana ni zoezi endelevu lisilo na kikomo huku hakuna dalili ya ajira kufunguliwa.

Utawala wa awamu ya nne kama sehemu ya kudhibiti na kuongoza sekta ya utumishi wa umma, uliamua kwenda Uingereza na kununua mfumo maalumu wa kudhiti watumishi wa umma nchini unaofahamika kama LOWSON.

LAWSON, maana yake ni HUMAN RESOURCE CAPITAL MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM
(HRCMIS)

Huu ni mfumo mzima unaoratibu na kudhibiti rasilimali watu ndani ya utumishi wa umma, kwa maana ya mtu abaki na cheque number moja tu, kudhibiti upandaji wa madaraja kiholela au kupeana vyeo hovyo hovyo, mfano huwezi kuteua mtu toka mtaani moja kwa moja na kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri au DAS wakati hajawahi hata kuwa mtumishi wa umma na kupitia ngazi mbalimbali za seniority au ukuu wa idara kama sheria inavyotaka.

LOWSON katika kudhibiti watumishi hewa inafanya kazi moja tu, mtumishi wa umma siku ya kwanza kabisa anapoajiriwa katika wiza au tasisi yoyote ya umma jina lake linapelekwa wizara ya utumishi kwenye Database (mfumo) iitwayo LOWSON, hapo unafunguliwa akaunti yako itakayokutambulisha kwamba wewe ni mtumishi wa umma mfano mwalimu wa shele ya msingi.

Akaunti yako hii ndio itakuwa utambulisho wako hata upokeapo mshahara, na LOWSON imeweka ukomo wa Akaunti, kwamba kila mtumishi nchini atakuwa na akaunti mmoja tu hata ungehama wizara na idara, bado akaunti yako utakayotumia kupokea mshahara itatambulika ile uliyosajiriwa nayo siku unaanza kazi serikalini.

Sheria ilitaka kwamba, mtumishi wa umma anapohama wizara, mfano ulikuwa Mwalimu (wizara ya Elimu) halafu ukahamishishwa kwenda wizara Kilimo, basi aliyekuwa na mamlaka kuidhinisha taarifa zako kuhamishwa kwenye LOWSON ni Katibu mkuu Kiongozi na sio vinginevyo.

Sasa watumishi wa hewa walipatikanaje? Database hii majina yakiingiliana au ukiingiza jina ambalo tayari lipo kwenye database itakataa kulipokea. Kilichokuwa kinafanyika nikwamba maafisa uajiri ndio walikuwa na uwezo wakutengeneza mtumishi hewa,

Mfano mimi Yericko Yohanesy Nyerere nimeajiriwa serikalini leo (wizara ya starehe na mambo ya huzuni), sasa Afisa wangu uajiri anataka kutengeneza mtumishi hewa, anachofanya ni kupeleka majina mawili, Yericko Yohanesy Nyerere na Yeriko Yohanesi Nyerere.

Hao ni watu wawili tofauti, yupo mtu halisi na yupo mtumishi hewa (ghost) na wote anawasilisha akaunti zao za benki, akaunti moja ataimiliki yeye ile ya mtumishi hewa. Hapa LOWSON haitawakataa itawapokea na kuwasajiri kama watumishi wa umma.

Lakini ni ukweli zoezi hili la kuzalisha watumishi hewa linahitaji umakini sana, na utatuzi wake (kuwaondoa) linahitaji umakini mara mia, kosa dogo tu linaweza kuliangamiza taifa letu.

Database hii mpaka leo hakukuwa na mtanzania wa kawaida anayeweza kuiendesha bali Mhindi mmoja hivi (kilema) ndie peke yake mwenye uwezo wakuiendesha tangu ilipofungwa hapa Tanzania.

Serikali hii ya awamu ya Tano ilipoingia tu, katika opareheni yake ya kuondoa watumishi hewa, ikaachana na matumizi ya database hii, na kurejea kwenye mfumo wa zamani, Sasa afisa uajiri wa Wilaya ya Nanyumbu anayo mamlaka ya kukuajiri na kukufukuza bila kikwazo cha makao makuu. Kinachoweza kuzuia kwasasa mtumishi hewa asizalishwe ni nidhamu ya uoga iliyotengenezwa tangu Rais Magufuli aingie madarakani, lakini kwa mfumo huu wa sasa ikatokea leo hii Magufuli akaondoka, basi taifa linaweza kuelemewa na watumishi hewa, mlango wakuingilia upo wazi.

Hakukuwa na sababu za msingi za kusimamisha ajira na mambo mengine kwasababu tu ya hili zoezi, labda serikali iueleze umma kwamba inashughuli nyingune nje ya hili.

Katika hili Serikali inaweza kuingia hasara kubwa kwa pande mbili, kwenye oparesheni ya uhakiki, au baada ya uhakiki wakajikuta wamezalisha watumishi hewa mamilioni bila kutarajia. Kwakutumia mfumo uleule uliozaa watumishi hawa hewa, serikali ilikuwa na uwezo wakuondoa hao watumishi hewa bila kuathiri shughuli zingine za uajiri na mengineyo.

Ilikuwa ni mtu mmoja tu yule muhindi kumwambia a search majina yote yanayofanana kwenye LOWSON kisha serikali kwakutumia vyombo vyake ijipe muda wakumuita mtumishi mmoja mmoja mmoja na kumuhoji juu ya ajira yake, kama ni hewa bila shaka hatatokea, atapotelea hewani tu.

Zoezi hili hivi sasa limeleta athari kubwa katika sekta mbalimbali ambapo serikali itaingia hasara mara mbili au zaidi. Mfano mdogo ni sekta ya afya..

Madaktari waliokwisha kumaliza mazoezi ya vitendo (internship) miaka miwili iliyopita na wale waliomaliza mwaka huu. Pia kuna madaktari waliomaliza vyuoni mwaka huu wanaotakiwa kuanza hayo mazoezi ya vitendo (internship) mapema tangu mwezi wa nane lakini bado hawajaanza.

Kuna utaratibu wa kuomba nafasi kupitia mtandao wa baraza la madaktari la Tanganyika, (Tanganyika medical council, utaratibu huo ulifunguliwa kwa siku tatu tu ili watakaowahi wapate nafasi. Ambao hawajaomba ndani ya siku hizi tatu, labda hawakuwa na taarifa au hawakuwa na nyaraka zote zinazohitajika mara moja, hao inawezekana imekula kwao. Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wa baadhi ya madaktari waliomaliza vyuo mwaka huu wasifanye 'internship' kwa sababu serikali ama haina pesa ya kuwalipa ama bado zoezi hili linaathiriwa na oparesheni ya watumishi hewa, ama serikali inabana matumizi.

Na ieleweke kuwa Daktari bila kufanya internship haruhusiwi kutibu na hata ajira zingine kwake ni deiwaka tu kwa sababu cheti cha 'nternship' kutumika kwenye maombi ya ajira.

Hii ni moja ya athari za namna ya kushughulikia tatizo la watumishi hewa, kimsingi lilikuwa tatizo dogo na wala lisingetangazwa kwa nguvu au kutumika kama alama ya nguvu za kiutawala.
SERIKALI HAINA PESA INALETA KISINGIZIO TU
 
ila inashangaza kuona kichwa cha familia kinajitapa kuwa familia inapesa wakat tunakula ugali na matembele kila siku ukimuuliza kwanini usiwatafutie wanao na wadogo zako kazi anajib kwani hawa hawali wakt pesa ipo!!mbn juzi nimenunua tax kwa pesa zang za mfukoni hebu waambie hao watoto waende shambani tu!!!!lakin cha kushangaza hata shamba la familia hakuna
 
Serikali imeishiwa pesa...Hizi wanazojisifia nazo majukwaani ni propaganda uchwara tu kutuaminisha malofa kwamba wako vizuri...
Dawa hakuna kwenye vituo vya afya,...Waalim watasahihisha Mitihani ya Mock na NECTA bila posho n.k..
Hivi ni viashiria tosha kwamba tumebakiwa na za kununulia Bomberdier tu!
 
Hazina iko vizuri sema mirija ya dili ndio inaendelea kuzibwa ikiwemo hiyo mishahara hewa.Halafu siyo lazima serikali kuajiri kama nguvu kazi itakayobaki baada ya hili zoezi itakuwa inatosha.Kumbuka tunahitaji kuwa na serikali ndogo iliyo makini itakayohamia Dodoma
 
Back
Top Bottom