Tunaomba serikali itoe ufafanuzi kuhusu makato kwenye mishahara ya mwezi wa nane!

Hapo utetezi uko wapi? HESLB wameanza kuchukua makato yao and that is the most probable reason. Unless unaijua sababu nyingine uitaje maana kusema 'serikali imechukua' ndio sababu za kipuuzi kwangu! #mtazamo
Ndugu...nafurahi kukuona hapa, considering vifo vya "mapolisi" hizi siku za karibuni!
 
Hata mimi hapa nilipo nina hasira sana KWANI bodi ya mikopo ya elimu ya juu imenikata mara mbili.Sasa mimi nashangaa hiki kitengo cha urejeshwaji wa mikopo kazi yake nini kama inafikia kiasi cha kushindwa kufahamu kuwa munufaika wa mkopo ameisha anza kukatwa au bado.Mbaya zaidi wamekata watu wengine ambao hata hawajawahi kukopa mkopo elimu ya juu tangu ulimwengu huu uumbwe.Au ndio hili tatizo la IT wa Tz alilokuwa anasemea mheshimiwa rais Magufuri?.Inakuaje mtu akatwe mara mbili na huku check number ni moja.Naomba mkurugenzi wa bodi ya mkopo ya elimu ya juu awape onyo kali wale wote waliohusika na uzembe wa kukata watu mara mbili,na turejeshewe pesa zetu haraka iwezekanavyo.Nb IT wa bongo ni eli wa Rwanda.
 
Mimi sijakatwa chochote. Ushauri wangu kwako, subiri salary slip ndo utajua kama umekatwa na kama umekatwa ni kwasababu gani.
 
Mimi sijakatwa chochote. Ushauri wangu kwako, subiri salary slip ndo utajua kama umekatwa na kama umekatwa ni kwasababu gani.
Sasa mkuu nisubirie salary silip mpaka lini? kumbuka hawa watu wataendelea kukata. kwa mfano ktka halmashauri kwetu hizo salary silip hazijaonekana tangu mwez wa tano mpaka sasa.
 
Hapana

Hapana kaka. Ingekuwa hivyo singelia hapa. Kamshahsra kenyewe hakatoshi hata kulipa ada ya watoto, st ksyumba
St. kayumba hakuna ada. Watoto watakuwa St. Mahela.
Ila pole sana maana kwa style ya kukata mishahara ya watu bila taarifa ni sawa na uuaji. Well, hata kwa kutoa taarifa, unaanzaje kumkata mtu malipo yake halali ya ujira wa kazi aliyokwishafanya?
 
Hiyo sababu munayopewa haikubaliki. Salary slip zinakuwa tayari kabla ya mshahara kutumwa benki. Ni uvivu wa HR personnel wenu tu kuzifuatilia. Waache viji excuse vibovu na wafanye kazi wanayolipwa kufanya. Kama wakivyokuwa zamani wanasema mikutano haiwezi kufanyika kwenye ukumbi wa jengo la ofisi, mbona sasa wanaweza!
kwa kweli mkuu hii kitu ya kuchelewesha salary slips unnecessarily ni jipu...,sijui hata tumpate nani aitolee tamko ili tamko lifike masikioni mwao na kuingia akilini mwao,ni kweli salary slips zinakuwa tayari kabla hata ya mishahara,kuna kauzembe tu somewhere somehow.
 
Mwenyewe alishasema "Nikichaguliwa mimi watu watalimia meno" Huu ndo wakati wetu kulimia meno. Jamaa hana nia ya kuwanufaisha watanzania, yeye anataka watu wataabike. Pasco aliwahi kusema hapa kwamba mtu aliyepata/aliyeishi maisha ya tabu/kinyama utotoni mwake, anapokuwa mtu mzima aghalabu huwa na hulka ya kulipa visasi.
 
Kuna watu walipandishwa madaraja kiholela, baada kugundulika inabidi madaraja mapya yasitishwe kwanza , waweza kuwa mmoja wao. Fuatilia
 
Si nilisoma humu serikali inapanga kuongeza mishahara baada ya zoezi la wafanyakzi hewa kufanikiwa? Sasa wanakata mishahara tena!!
 
Hela hamna tunagawana kidogo kilichopatikana tuvumiliane yale makusanyo ni mbwembwe tu
 
Au ni Loan Board mkuu...!!!
Loan board hawakati kienyeji labda kama Mwajiri mbabe lakini kikawaida atachukua jina lako litapelekwa loan board kisha wataleta deni lako alafu mwajiri atakuuliza kama umekubali hilo deni na kutoa mapendekezo ya kiwango utakachokata (mara nyingi haizidi 30,000) hivyo ukikubali anaanza kukata (hiyo ni kwa HR anaejua kazi yake)
 
Wewe loan board wanakata zaidi ya 30000/= mbona cc wengine tunakatwa 58000/=
 
Unafikiri viwanda vitajengwaje? Mkuu inabidi ujikaze tu hakuna namna.
Ndiyo serikali yetu
 
Wewe loan board wanakata zaidi ya 30000/= mbona cc wengine tunakatwa 58000/=
Ndo hiyo sasa nimesema juu inategemea na ofisi na HR husika pia unalipwa ngapi, hii ni kwa wale waliojitokeza kulipa mara kwanza 2009/2010 ambao wanakatwa kwa style hiyo mkuu
 
Back
Top Bottom