Tunaomba serikali itoe tamko kuhusu mishahara ya wafanyakazi

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Leo ni tarehe 5 na hakuna kinachoeleweka kuhusu mishahara ya wafanya kazi.Serikali kupitia raisi Kikwete ilitangaza kwamba ifikapo tarehe 26 ya kila mwezi wafanyakazi watakuwa wameshapata mishahara yao.Inashangaza kwamba mpaka leo wafanyakazi hawaja pata mishahara yao na serikali imekaa kimya kabisa kuhusu swala hili.Kwa ukimya huu sisi wafanyakazi tuna kila sababu ya kuaamini kwamba kuna jambo lisilo la kawaida, baya na la aibu ambalo limefanyika au linaendelea kufanyika, ndio maana serikali inasita kutoa tamko.Serikali ikumbuke kwamba wafanyakazi ni wanadamu ambao wanahitaji kula na kunywa na kupata haki zingine za msingi kama wanadamu wengine.Kuwa-nyima mishahara yao ni kuwanyima haki hizo kama wanadamu.Inashangaza kwamba serikali inaingia kwenye mikataba ya kimataifa ya kuwalinda wanyama lakini inashindwa kuwalinda wananchi wake hata katika yale mambo ya msingi kabisa.Katika hili naomba vikundi vya haki za binadamu viingilie kati kuishinikiza serikali iwalipe wafanyakazi mishahara yao,na kisha itoe tamko juu ya kile kilichotokea.Mwisho tunaitaka serikali ituombe radhi.
 
Hivi ni wafanyakazi wote hawajapata au sector yenu tu??? Vp wanajeshi na maaskari washapata?
 
Majeshi yote yameshapata na hii inafanyika hata katika miezi mingine.Tunajua hii inatumika kama hongo,for obvious reasons.
Hivi ni wafanyakazi wote hawajapata au sector yenu tu??? Vp wanajeshi na maaskari washapata?
 
Wanafanya mpango wa kukopa katika mabenki ili walipe maana hazina hakuna kitu kumedoda.
 
Kodi hazijakusanywa mwezi wa tisa? Au tumelipia madeni hela zote?
 
attachment.php

Huyu ndo atoe tamko!
 
Majeshi yote yameshapata na hii inafanyika hata katika miezi mingine.Tunajua hii inatumika kama hongo,for obvious reasons.

too conclusive cum blanket judgemnt- naimani idara nyingi za serikali zimeshapata mshahara, naimani idara yako ina matatizo , huenda inachelewesha kuandaa docs za mishahara.
 
Hamkujua kuwa NEC ya thithiemu ilikuwa na vikao? Kipaumbele kilikuwa ni kule, kwakuwa wamemaliza basi tutafanya mishahara yenu kuwa kipaumbele!!!!!!
 
Wewe ni agent mpuuzi tu wa serikali ambae naamini nia yako ni kuposha hoja.I believe nobody will take you seriously.

Pole sana mkuu,lakini pia acha jazba!Ni kweli kuwa wafanyakazi wengine waserikali kuu nikiwepo na mimi mwenyewe tumeshapata mshahara siku nyingi tu! Lakini ni kweli pia kuna wngine mpaka leo ni bila bila!
 
Wewe ni agent mpuuzi tu wa serikali ambae naamini nia yako ni kuposha hoja.I believe nobody will take you seriously.

kweli pesa sabuni ya roho, mtu akiikosa anapata jazba....anyway poleni watumishi wa umma, kumbukeni kutumikia umma ni wito.... Vumilieni pesa wametumia kupiga trip
 
Foolish answers for foolish questions.Unapofanya ujinga always remember there will be a negative reaction.Hata hivyo to substantiate your claim ni vema ukatutajia wizara ambayo wewe unafanya kazi na ambayo unadai wafanyakazi wake wameshalipwa mishahara excluding majeshi.
Pole sana mkuu,lakini pia acha jazba!Ni kweli kuwa wafanyakazi wengine waserikali kuu nikiwepo na mimi mwenyewe tumeshapata mshahara siku nyingi tu! Lakini ni kweli pia kuna wngine mpaka leo ni bila bila!
 
Very funny comments.Kweli ndio maana Tanzania badala yakupiga hatua inarudi nyuma.
too conclusive cum blanket judgemnt- naimani idara nyingi za serikali zimeshapata mshahara, naimani idara yako ina matatizo , huenda inachelewesha kuandaa docs za mishahara.
 
Back
Top Bottom