sweetlady
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 16,947
- 8,409
Asiyetaka kuhesabiwa aweke alama ya v kwenye geti au mlango wake.
Wengi tu wameweka hiyo alama na hawajahesabiwa.
Asiyetaka kuhesabiwa aweke alama ya v kwenye geti au mlango wake.
Nasema hivi, sisi hakuna kitu tunachokiweza.
jamani nimesikia wimbo wa taifa ghafla nikamsikia kikwete anazungumza lakin sikupata nafasi ya kumsikliza kwa hyo mwenye taarifa sahii atujuze alikuwa anasemaje
Sensa kwa maendeleo yako jitahidi uhesabiwe!
Mimi sijahesabiwa na niliacha idadi ya wanakaya nyumbani na hawakupita na huo muda wa kwenda kwa mtendaji sina kutokana na shughuli zangu .je,nimetenda kosa kisheria
Sitaki kuamini kama tumefika hapo.Ikiwa kweli nahama nchi.Huku kwetu huandikishwi hadi ulipe Mchango wa ujenzi wa soko wa Tsh15,000.
Hili zoezi linasimamiwa na Viongozi wetu wa Mtaa.
Tena uhesabiwe Mara Moja tu!
Leo ndio siku ya mwisho, baada ya hapa unatakiwa kupeleka taarifa zako mwenyewe kwa mwenyekiti wako wa mtaa.Kesho nitakuwa nyumbani waje kunihesabu,ila saa tisa naenda kuangalia mechi
This is so "stone aged" nashangazwa hata ku type unajuwa!Mimi nimepiga chaki mlangoni kwangu, na wengi wengine wamefanya hivyo, wana ushahidi gani kama sijahesabiwa? wakiona chaki wanapita.
Kwi kwi kwi teh teh teh!
Utakuwa umevunja Sheria namba 1 ya takwimu ya mwaka 2002. Hukumu yake ni kwenda jela miezi sita au faini au vyote kwa pamoja.
Naishauri Serikali itumie list za sensa kugawa vitambulisho vya taifa. Asiyeonekana kwenye hizo list atapaswa kujieleza ilikuwaje asiwepo; kama atakuwa na sababu za msingi will be OK vinginevyo kama ni hadithi za akina Ponda hatua stahiki zichukuliwe. Halafu maajabu ya firauni utamkuta Ponda yumo kwenye sensa - kishawauza wenzie.
Rais amewataka watu wote watakaoshindwa kuhesabiwa mpaka siku ya mwisho ya sensa, wapeleke taarifa zao kwa viongozi wa maeneo yao ndani ya siku saba ili taarifa zao zipelekwe panapohusika. Baada ya muda huo kupita wale watakaoshindwa kufanya hivyo watashughulikiwa.
Source: Hotuba Ya Rais