Tunamkumbuka Mzee Rashid M. Kawawa - Simba wa Vita

Lol...

Maneno yako mwenyewe ndio data nilizotumia kukuita mzushi. nitafuta kauli yangu endapo utamtaja huyo "mzee" aliyekuambia aliyokwambia. Other than that wewe ni Kazushi Sakuraba.

Wewe ulizipitia au uliambiwa na "mzee"?

Superstitions kivipi? Na kama huzitaki basi nazichukua. Sikukulazimisha uzipokee.

I have no reason not to believe that you are not an agent of the government, and I will reiterate that I will not name my sources, citing age old conventions of protecting sources.

Kuwa trigger happy katika kuita watu wazushi bila kujua undani wa mambo ndio uzushi mkubwa zaidi, maana unamuita mtu mzushi kwa kitu usichokijua.

No wonder huelewi hata superstition ni nini.
 
well spoken ...mwaminifu..sana ,mwadilifu..na mwenye nidhamu...as you said waliokuja kuharibu kidogo au kadiri mtu atakavyoona historia yake ni kweli ni MTANDAO ...walimteka nyara mwaka 2005..hasa wakijuwa baada ya mwalimu ..ambaye angalau ccm 2005 iliwasikiliza ni kawawa, mwinyi na kingunge ambaye nao waliwashika!!..jambo hili liliwasononesha sana wenzake aliokuwa nao toka zama kina ...salim.,malecela,msuya,warioba ,gamaetc.....viongozi wengi wa zamani waliacha kabisa hata kumtembelea pale madale wakiamini aliwasaliti kwa kujiunga mtandao walitaka abakie neutral kama mzee..wao

kawawa aliendelea kumuunga mkono kikwete hata pale viongozi wote wa zamani ambao saa wamekuwa wapinzani wakubwa wa kikwete yeye amebaki kumtetea..nadhani kiikwete ana sababu ya ziada ya kusononeka!!!

- Hiki kifo mkuu kinabadilisha kabisa marathon ya 2010, inaogopesha sana maana everything lately seems to be working for Lowassa, yes I said it hii ni big plus kwake!

Respect.

FMEs!
 
I have no reason not to believe that you are not an agent of the government, and I will reiterate that I will not name my sorces, citing age old conventions of protecting sources.

What's wrong with you? Are you suffering from paranoid schezophrenia or something?

Kuwa trigger happy katika kuita watu wazushi bila kujua undani wa mambo ndio uzushi mkubwa zaidi, maana unamuita mtu mzushi kwa kitu usichokijua.

Wewe unayekijua si utujuze sisi tusiokijua. Unaombwa habari kamili unaanza visingizio...oooh age old conventions fo blah blah blah...WTF? mTAJE HUYO "mzee" otherwise failure to do so renders you Kazushi Sakuraba.

No wonder huelewi hata superstition ni nini.

I'm better off not understanding let alone knowing what it is.
 
What's wrong with you? Are you suffering from paranoid schezophrenia or something?

Wewe unayekijua si utujuze sisi tusiokijua. Unaombwa habari kamili unaanza visingizio...oooh age old conventions fo blah blah blah...WTF? mTAJE HUYO "mzee" otherwise failure to do so renders you Kazushi Sakuraba.

I'm better off not understanding let alone knowing what it is.

Hahaha,

Your tactics are not working on me.Habari ndiyo hiyo, utake usitake.The record is straight, aliyetaka tuimbe chorus ya sifa tu ajue kwamba hapa ni JF, where we dare speak openly.
 
- Hiki kifo mkuu kinabadilisha kabisa marathon ya 2010, inaogopesha sana maana everything seems to working for Lowassa, yes I said it hii ni big plus kwake!

Respect.

FMEs!

..that is possible buddy..EDWARD LOWASSA....anaweza kuwa Jacob ZUMA wa Tanzania....mnajuwa kuwa zuma alikuwa msaidizi mwaminifu wa mbeki ambapo power brokers walipomuona kuwa ni tishio walimchonganisha na mbeki ..na kwa kumtumia mkuu wa COBRA squad....AKISHIRIKIANA na mkuu wa usalama..wakamchomekea zuma rushwa ya silaha kupitia kwa msaidizi wake wa kiuchumi ....na baadaye kashfa mbaya ya mapenzi....kwa kweli ZUMA aliondoka ,madarakani akiwa mchafu na ananuka kuliko lowassa ambaye BUNGE na serikali yenyewe wanashindwa kumtia hatiani....wewe fikiria zuma alikuwa convicted kwenye baadhi ya makosa!!

kifo cha kawawa kwa kweli kinamuacha jk MKIWA .....lakini ni lazima mjuwe kuwa JK has CC[central commetee]..and lowassa may have NEC and GENERAL assembly!!....nadhani mnajuwa kuwa CC ni kila kitu and it can keep JK surving for a while though ni lazima ajihadhari fate ya Mbeki naye isimkute ....kwani hitoria ipo wazi kuwa lowassa was poweful kuliko jk ...tangu walipoanza mbio hizi 1995...na ni lowassa ambaye bid yake iliposhindwa aliamua kubank kwa kikwete na kumfanya awashangaze wachunguzi wa mambo pale Mkutano mkuu mwaka 1995....ambao walidhani baada ya kumtoa lowassa wanambakisha mgombea dhaifu KIKWETE..Akawashangaza hadi ikabidi wa strike deal ambalo baadaye lilimpa urais.......thuogh hata kawawa alikuwa anajuwa kuwa lengo lao na nyerere lillikuwa kumfix kikwete badaye aukose urais 2005 ikifika ...jambo ambalo KAWAWA alikuja kufanya kinyume chake!!!
 
Hahaha,

Your tactics are not working on me.Habari ndiyo hiyo, utake usitake.The record is straight, aliyetaka tuimbe chorus ya sifa tu ajue kwamba hapa ni JF, where we dare speak openly.

Habari ndiyo hiyo. Wazushi mko wengi humu.
 
- Hiki kifo mkuu kinabadilisha kabisa marathon ya 2010, inaogopesha sana maana everything seems to working for Lowassa, yes I said it hii ni big plus kwake!

Respect.

FMEs!

..that is possible buddy..EDWARD LOWASSA....anaweza kuwa Jacob ZUMA wa Tanzania....mnajuwa kuwa zuma alikuwa msaidizi mwaminifu wa mbeki ambapo power brokers walipomuona kuwa ni tishio walimchonganisha na mbeki ..na kwa kumtumia mkuu wa COBRA squad....AKISHIRIKIANA na mkuu wa usalama..wakamchomekea zuma rushwa ya silaha kupitia kwa msaidizi wake wa kiuchumi ....na baadaye kashfa mbaya ya mapenzi....kwa kweli ZUMA aliondoka ,madarakani akiwa mchafu na ananuka kuliko lowassa ambaye BUNGE na serikali yenyewe wanashindwa kumtia hatiani....wewe fikiria zuma alikuwa convicted kwenye baadhi ya makosa!!

kifo cha kawawa kwa kweli kinamuacha jk MKIWA .....lakini ni lazima mjuwe kuwa JK has CC[central commetee]..and lowassa may have NEC and GENERAL assembly!!....nadhani mnajuwa kuwa CC ni kila kitu and it can keep JK surving for a while though ni lazima ajihadhari fate ya Mbeki naye isimkute ....kwani hitoria ipo wazi kuwa lowassa was poweful kuliko jk ...tangu walipoanza mbio hizi 1995...na ni lowassa ambaye bid yake iliposhindwa aliamua kubank kwa kikwete na kumfanya awashangaze wachunguzi wa mambo pale Mkutano mkuu mwaka 1995....ambao walidhani baada ya kumtoa lowassa wanambakisha mgombea dhaifu KIKWETE..Akawashangaza hadi ikabidi wa strike deal ambalo baadaye lilimpa urais.......thuogh hata kawawa alikuwa anajuwa kuwa lengo lao na nyerere lillikuwa kumfix kikwete badaye aukose urais 2005 ikifika ...jambo ambalo KAWAWA alikuja kufanya kinyume chake!!!
 
buriani mzee kawawa.

kwa tunaokumbuka mema yake ni vyema tukafanya hivyo kwa kiasi kwani kama binaadamu na mwanasiasa pia yalikuwepo aliyoyafanya ambayo hayakuonekana kama ni mema machoni pa wengine.

vivyo hivyo hata wale tunaokumbuka mapungufu yake tufanye hivyo kwa kiasi. huu ni wakati wa maombolezo na kuwafariji wale walioguswa na msiba huu moja kwa moja.
 
Nyerere+1.jpg

Rafiki yake wa Karibu - A rare picture!!
 
Ama kweli tumepoteza mtu muhimu saana Tanzania. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi!!
 
Simba wa Vita: Mwanafunzi pekee wa Nyerere aliyefanikiwa kuhitimu

Na Midraji Ibrahim
1st January 2010

Rashid Mfaume Kawawa (80), maarufu kama Simba wa vita amefariki.
Unaposoma simulizi za historia ya mapambano ya uhuru wa nchi hii basi, Kawawa hakwepeki ni miongoni kati ya wanasiasa na Watanzania waliokuwa nguzo kubwa ya kutetea na kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kawawa ni mwanafunzi pekee wa Baba wa Taifa, Marehemu Mwalimu Julius Nyerere, wa kupigiwa aliyefanikiwa kuhitimu na ameondoka duniani akiamini yale aliyosimamia.
Wengine wanaweza kuhoji, lakini mfano mchukue mwanafunzi mfuasi kama Kingunge Ngombare-Mwiru yale anayohubiri sio anayotenda, tofauti na Kawawa ameondoka bila kusikia kujilimbikizia mali.
Wapo wanafunzi na wafuasi wa Mwalimu Nyerere wamestaafu, lakini wanaandamwa na jinamizi la ufisadi. Mzee Kawawa hayumo kwenye hiyo orodha.
Katika uhai wake, Kawawa alitumia muda mwingi kuhimiza umoja na mshikamano wa Watanzania.
Nadiriki kutamka kuwa, Kawawa alikuwa mtu pekee mwaminifu kwa Baba wa Taifa, Marehemu Mwalimu Julius Nyerere.
Unapoangalia orodha ya wapigania uhuru na lile Baraza la Kwanza la Mawaziri wa Tanganyika huru, ni mtu pekee ambaye amefikia tamati ya uongozi pamoja. Mwaka 1985, baada ya Mwalimu Nyerere kung'atuka na Kawawa aliamua kustaafu kazi serikalini.
Wapo watu kama akina Oscar Kambona, lakini hawakufika mbali na Mwalimu Nyerere. Hakika! Taifa limepoteza hazina kubwa.
Ukitaka kuandika vitabu vingi kuhusu wasifu wake, lakini kila maendeleo ya taifa hili ambayo hivi sasa yanatolewa mifano, msimamizi alikuwa Kawawa.
Mwaka 1962, baada ya Mwalimu Nyerere kujiuzulu Uwaziri Mkuu, Kawawa alishika madaraka hayo na kuhakikisha anatekeleza maamuzi kwa nguvu zake zote. Hapa unaweza kubaini jinsi alivyokuwa sio mroho wa madaraka kwa sababu, baada ya hapo alishushwa cheo na kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Kuna baadhi ya hatua za utekelezaji katika masuala mbalimbali ya kitaifa lawama nyingi zilitupwa kwake, na hiyo inanikumbusha wakati fulani, Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kuwa Kawawa alikuwa akilaumiwa kwa ajili yake (Nyerere).
Mathalan, utekelezaji wa Azimio la Arusha na operesheni vijiji, aliamua kuyatekeleza bila simile na lawama zikatupwa dhidi yake.
Utekelezaji operesheni vijijini ulipata upinzani mkubwa, lakini kutokana na kusimamia maamuzi alihakikisha inafanyika.
Itakumbukwa operesheni ya kuzuia uvaaji nguo fupi, mtekelezaji alikuwa Kawawa, ingawa lawama zilikuwa zikielekezwa kwake, ulikuwa ni uamuzi wa Baraza la Mawaziri.
Kwa upande wa dini, Kawawa ni miongoni mwa Wadhamini wa mwanzo wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) baada ya Mwalimu Nyerere kuvunja jumuiya ya Waislam ya East African Muslim Welfare Society.
Anaelezwa na watu ambao amefanya nao kazi kuwa, alisaidia sana serikali kuhusu dini kubaki suala binafsi na kutochanganywa na serikali. Kawawa amefanya kazi kubwa kuhakikisha anasimamia mpango wa kusomesha wazalendo baada ya uhuru, aliosimamia baada ya kukabidhiwa Uwaziri Mkuu na Mwalimu Nyerere.
Pia, alifanya kazi kubwa ya kuunganisha vyama vya wafanyakazi na alipata upinzani mkubwa kutoka kwa marehemu Kasanga Tumbo ambaye alikuwa kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli, lakini Kawawa alishinda.
Kawawa alikipenda chama ndani ya moyo wake, aliweza kuanzisha vyuo vya siasa na hata baada ya kustaafu, ulipokuwa ukipata nafasi ya kuzungumza naye alikuwa akionyesha kukerwa na mambo ya ovyo yanayoendelea.
Kawawa, tangulia kazi uliyotumwa umeitimiza.
Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amina.

CHANZO: NIPASHE
 
Jamaa alichangia kufa kwa financial institutions za Tanzania, alichukua hela kama mikopo kwa sababu za "kichama" kutoka mabenk, hususan benki ya nyumba na shirika la bima, alipofuatwa na watendaji wa mashirika haya akawa anawazungusha, misho wake akawaambia "Kwani nyie hamna "bad debts"? andikeni madeni haya kama "bad debts" " wazee wa mabenki na mashirika haya wakashindwa kufanya kitu, ukizingatia hii ilikuwa ni enzi ya chama kushika hatamu na Rashid Mfaume Kawawa ndiye katibu Mkuu wa chama.

Sitaki kusema hana mchango mzuri katika nchi yetu, ila sipendi hii tabia ya kumsifia mtu kama malaika na kumuita mpiga vita ufisadi just because amfariki tu.

Huu ni ukweli nilioupata kutoka kwa wazee wenyewe waliofanya naye kazi kuhusu hii mikopo,hususan kutoka NIC.

Inayowika leo EPA, lakini kina Kawawa walishafanya yote haya kitambo, kulikuwa hakuna mitandao tu ya kuwaumbua siku hizo magazeti ya chama na serikali na radio RTD tu.

Sikubaliani na wewe kuwa RMK alichangia kufa kwa taasisi zetu za fedha, kama katibu mkuu wa chama tawala aliweza kukopa ili chama kiendeshe miradi yake lakini kwa bahati mbaya miradi hiyo haikufanikiwa kwa sababu za kukosa utaalam. Sasa katika any business kuna risk ambayo kwa financial institutions is always provided for and provision for bad TANU/CCM debts was no exception!!

RMK na wenzie hawakukomba hela benki na kuzipeleka kununua nyumba Dubai/ South Africa; hawakuficha vijisenti kwenye off-shore accounts huko Ulaya kama mafisadi wa leo wanavyofanya! Kawawa alikuwa mzalendo halisi na aliwalea watoto wake kama watoto wa raia wananchi wa kawaida; nakumbuka binti yake Rehema baada ya kumaliza form six alikwenda Natinal Service pale Ruvu-operation Tumaini na baada ya hapo akaenda UDSM na sio Ulaya.

Mimi naamini kabisa Kawawa mpaka umauti unamfika hakuwa na bank account nje ya nchi unlike the likes of Lowassa, Rostam, Karamagi not to mention bwana vijisenti!!! RMK alikuwa kiongozi aliyekuwa na mtazamo wa kitaifa na wala hakuwa TRIBAL BARON; juu ya kuwa alikuwa waziri mkuu hakulpendelea sehemu aliyotoka katika mgawanyo wa rasilimali za Taifa; resouces were distributed nationally under his watch on the basisi of national needs and priorities unlike siku hizi resources zinapelekwa wanakotoka viongozi bila kuzingatia national priorites!! Uzalendo huo ndio unawafanya watu wamlilie na kumkumbuka.
 
In the wake of hii ya kutaka kumtakasa Kawawa kama shujaa vile vile si vibaya tukakumbusha jinsi alivyokuwa LOYAL kwa Mwalimu mpaka akataka kubadili dini awe Mkristo kama Nyerere.

Na mwalimu kwa kujua kuwa Kawawa has aloways been loyal kwake akamwambia 'huna haja ya kubadili dini kuwa Mkristo ndio uonekane kuwa ni Mwaminifu'

Naam huyo ndiye al Marhum Bwana Rashidi Mfaume Kawawa ambaye alikuwa mume wa Mama Sofia Kawawa.

Kama kama hiyo haitoshi watawala wameamua kuwa time ya kuswali Sala ya Ijumaa leo ndio twende kuuaga mwili wa mzee Kawawa!

Na kutwa nzima wameamua kumparade kama walivyomfanyia Mwalimu bila kuangalia sensitivities kuwa Marehemu kama ni muislam na kafariki katika mazingira yasio na utata basi azikwe mara moja. If anything ilitakiwa leo watu wana fanya Khitma lakini wapi!

Mwenyezi Mungu amlaze pale anapostahili.

kawawa1.jpg
 
GT,
Huo ni uwongo wa mchana. Naona ninyi mafundamentalist will grab at anything to try to destroy the legacy of a great leader.
 
GT,
Huo ni uwongo wa mchana. Naona ninyi mafundamentalist will grab at anything to try to destroy the legacy of a great leader.

Inaelekea hata hotuba za Mwalimu ulikuwa husikilizi wewe

And speaking of Greatness what was so great about Rashidi?

Come on man, najua sasa hivi Taifa liko sedated na kutaka kumfanya Rashidi Mtakatifu ili hali alikuwa na madhaifu kama binadamu mwingine.

Editorials za magazeti ya leo ni aibu tupu.
 
Jamani hata mkiangalia TBC they just show the moments when Rashid Kawawa was a General Secretary and prominent member of CCM and not as as a National Figure!
 
the question is, Je hatuombei lakini je kama akitokea Mzee Aboud Jumbe anafariki haya maparade ya kudhalilisha maiti yatafanywa au?
 
Inaelekea hata hotuba za Mwalimu ulikuwa husikilizi wewe

And speaking of Greatness what was so great about Rashidi?

Come on man, najua sasa hivi Taifa liko sedated na kutaka kumfanya Rashidi Mtakatifu ili hali alikuwa na madhaifu kama binadamu mwingine.

Editorials za magazeti ya leo ni aibu tupu.
Kawawa as a trade unionist, brought to TANU his organisational skills. Nitajie hiyo hotuba ya Mwalimu aliyosema Kawawa alitaka kubadili dini then I will take back my retort.
 
And speaking of Greatness what was so great about Rashidi?

Come on man, najua sasa hivi Taifa liko sedated na kutaka kumfanya Rashidi Mtakatifu ili hali alikuwa na madhaifu kama binadamu mwingine.

Editorials za magazeti ya leo ni aibu tupu.
.
GT, kama heshima kwa marehemu, we always speak good of him, hata mimi/wewe ukifa leo, watu watasema P or GT was a good man. Kila mtu ana utdhaifu wake, ili baada ya kuitwa mbele ya haki, sio busara kuyazungumza inakuwa kama una mdespise marehemu.

Please give him a break kipindi hiki ambacho bado hajapumzishwa, ili apumzishwe kwa amani, wakati wa kuzungumza legacy yake, ndipo tumwage kila kitu.

RIP MZEE RASHIDI MFAUME KAWAWA 'SIMBA WA VITA'.
 
Back
Top Bottom