Tunamkumbuka Mzee Rashid M. Kawawa - Simba wa Vita

Kawawa.jpg
 
Asante sana Superman kwa picha hizi zinazotupa kumbukumbu ya mzee wetu.
RIP Mzee Kawawa.
 
Du! Mkuu; hapo alitoka photocopy ya Simba Wa Vita.

...naaam, umri nao unamchukua Mzee Salmin Amour.
Mw'Mungu amghufirie aloyatanguliza Mzee Rashid M Kawawa,
Mchango wake kwa Taifa uhidimiwe!
 
Kuuliza si ujinga kwakweli me na picha ila siju kupost munielekeze naomba msaada wenu. Thnks

Mkuu;

unaweza kucopy picha yoyote kwa "Right Click" the "Copy" kutoka kwenye sorce uliyonayo kisha njoo hapa kwenye blank screen ya JF na "Right Click" tena kisha "Paste".

Au tumia icon za hapo juu za JF ya "Insert Image" kisha fuata maelekezo.
 
Waungwana

Najua kila mtu alimfahamu marehemu Kawawa kwa namna moja ama nyingine, kuna ambao alikuwa bosi wao, wengine bosi wa wazazi wao au rafiki zao na wengine hata kupitia nyimbo kama za mchakamchaka nk. na hadithi za uongo na kweli za shuleni.

Sidhani kama wako waliofanya nae biashara kwani huyu alilinda maadili ya uongozi hadi mwisho wa maisha yake na hakuwahi kuchanganya siasa na biashara.

Sasa jamani kama sehemu ya maombolezo, unaweza kuweka hapa jinsi ulivyomjua marehemu mzee wetu Rashid Mfaume Kawawa.

Mimi naahidi nitaweka hapa post ya nilivyomfahamu Kawawa kesho.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina
 
When is it politically correct to asses somebody critically after his death?

Maana mimi nina some negative reviews of Kawawa's life na sijui kama mnaweza kuzi stomach hapa, na sikutaka kusema lakini naona watu wana solicit views.

Ninafikiri kuhusu "we dare speak open" but at the same time kuna issue ya cultural sensitivity.
 
dont worry mkuu, we sema ukweli tu unaoufahamu kumhusu huyu simba wa vita.
 
dont worry mkuu, we sema ukweli tu unaoufahamu kumhusu huyu simba wa vita.

Jamaa alichangia kufa kwa financial institutions za Tanzania, alichukua hela kama mikopo kwa sababu za "kichama" kutoka mabenk, hususan benki ya nyumba na shirika la bima, alipofuatwa na watendaji wa mashirika haya akawa anawazungusha, misho wake akawaambia "Kwani nyie hamna "bad debts"? andikeni madeni haya kama "bad debts" " wazee wa mabenki na mashirika haya wakashindwa kufanya kitu, ukizingatia hii ilikuwa ni enzi ya chama kushika hatamu na Rashid Mfaume Kawawa ndiye katibu Mkuu wa chama.

Sitaki kusema hana mchango mzuri katika nchi yetu, ila sipendi hii tabia ya kumsifia mtu kama malaika na kumuita mpiga vita ufisadi just because amfariki tu.

Huu ni ukweli nilioupata kutoka kwa wazee wenyewe waliofanya naye kazi kuhusu hii mikopo,hususan kutoka NIC.

Inayowika leo EPA, lakini kina Kawawa walishafanya yote haya kitambo, kulikuwa hakuna mitandao tu ya kuwaumbua siku hizo magazeti ya chama na serikali na radio RTD tu.
 
Huu ni ukweli nilioupata kutoka kwa wazee wenyewe waliofanya naye kazi kuhusu hii mikopo, hususan kutoka NIC.

Kama ni ukweli wataje basi hao "wazee" waliokupatia huo ukweli. La sivyo utakuwa mzushi tu na kuishia kusema huwezi kuwataja kwa kulinda anonymity yao. Wataje hao "wazee"...
 
Kama ni ukweli wataje basi hao "wazee" waliokupatia huo ukweli. La sivyo utakuwa mzushi tu na kuishia kusema huwezi kuwataja kwa kulinda anonymity yao. Wataje hao "wazee"...

akiwataja iweje sasa wakati wa kuendesha nae kesi ndiyo hivo tena kawahi kwenye makao mengine. Ni vema tuuu kasema kile anachokifahamu wala tusimtishie itakuwa kama tunalazimisha kila mtu awe anasifia tuu hata kama sifa sio za kweli
 
akiwataha iweje sasa wakati wa kuendesha nae kesi ndiyo hivo tena kawahi kwenye makao engine. Ni vema tuuu kasema kile anachokifahamu wala tusimtishie itakuwa kama tunalazimisha kila mtu awe anasifia tuu hata kama sifa sio za kweli

Akiwataja angalau tutaweza kujua kuwa hazushi. La sivyo kila mtu anaweza akaja akasema chochote kile hata kama ni cha uongo.
 
Kama ni ukweli wataje basi hao "wazee" waliokupatia huo ukweli. La sivyo utakuwa mzushi tu na kuishia kusema huwezi kuwataja kwa kulinda anonymity yao. Wataje hao "wazee"...

The names are preserved to protect the innocent, this is a standard rule honored by, for example, journalists all over the world.

We unafikiri CCM ilikuwa inaendeshwa kwa michango ya wanachama tu?

Huwezi kunilazimisha kutaja majina, hata New York Times na magazeti yanayo uphold the highest standards za journalism kila siku utaona wanaweka anonymous sources kwa sababu za kwalinda hao watu.

Unataka nimtaje mzee wa watu halafu kesho usalama wa taifa waende kumgongea mlangoni? Nitajuaje kama wewe nawe si usalama wa taifa unataka umtafute huyu mzee na kumpitia yeye unitafute mimi?

Pinga hoja kwa hoja, sema kwa nini Kawawa hawezi kuwa amefanya hivi, usiingie kwenye vihoja vya kutaka kuvunja uhuru wangu wa privacy.

Kawawa mwenyewe kakubali amechemsha mambo mengi na kuomba msamaha, wewe nani usiyetaka akosolewe?
 
Miye sina kasoro ya kumpa mzee Rashid Mfaume kawawa zaidi najua alikuwa mtu muaminifu sana na siyo Fisadi.....Bluray kama kosa lilishatokea na sasa amekufa let him rest in peace my dearest!....
Rest In peace RMK.
 
When is it politically correct to asses somebody critically after his death?

Maana mimi nina some negative reviews of Kawawa's life na sijui kama mnaweza kuzi stomach hapa, na sikutaka kusema lakini naona watu wana solicit views.

Ninafikiri kuhusu "we dare speak open" but at the same time kuna issue ya cultural sensitivity.

Nakubaliana na wewe 100%, kuna kumfahamu mtu kwa mazuri au mabaya. Ukiingia ndani zaidi utakuta na yeye alikuwa na mabaya yake tena yakiwekwa hapa hadharani tutaacha kumuombea kwa mwenyezi mungu amlaze mahali pema.

Nafikiri muda huu ni wa kuwafiriji wafiwa na watanzania kwa kuondokewa na mmoja wa aliyewahi kuwa mtawala wao. Ninamuombea mwenyezimungu amuepushe na adhabu ya kaburi na ampe maghafira hilo ndilo muhimu kwa hizi siku saba za maombolezi.
 
Back
Top Bottom