Tunamkumbuka Mzee Rashid M. Kawawa - Simba wa Vita

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Wana JF;

Kwa ajili ya Kumbukumbu ya Picha ya Mzee Wetu Simba Wa Vita; Yeyote Mwenye Picha/story za kumbukumbu zinazomuhusu anaweza akazipost hapa:


Kawawa.jpg
 
Asanteni sana kwa picha hizi za hayati mzee wetu simba wa vita!Tumeweza kuwaona waasisi wengine kama Hayati Oscar Kambona,Paul Bomani Na Amir Jamal.Wengine siwakumbuki.Vilevile naivulia kofia Jamii Forum kwani ndio ilitupa breaking news kwa tukio hilo jana jioni!
 


Wakuu picha hii imenikumbusha mbali sana, inanipa matumaini ingawa hawa watu hawapo na sisi. Nimewajua watatu tu, Nyerere, Kambona ( nyuma ya nyerere) na Kawawa. wengine nani anaweza kunisaidia?

Kweli we had a real Tangayika president - manake not only handsome but also serious hebu mcheki hapo - kijana aggressive, smart mwenye mission na vision

Hawa wote wanaonekana kuwa na moyo wa uzalendo (very serious people) kwa taifa lao at that time Tanganyika - tungekuwa na viranja wanaofanana na hawa hadi leo basi tungekuwa mbali sana.

Sasa tumebakia na Vijicent, vijirichimound, vijirada, vijikagoda etc tunahangaika navyo.

Mi naona tupumzike tarehe 2th, 2010 tuomboleze msimba wa Kiongozi wetu shupavu - Simba wa VITA. Nakumbuka vita ya kagera alienda na mwalimu na walikuwa Front line... Ongoza kwa mifano like these guys, kuwa na uchungu na nchi yako, kubali kufa, jitoe moyo wako wote kwa watanzania, kuwa sehemu ya matatizo yao, huo ndiyo uongozi bora. hii ni mifano hai wakuu.

Tatizo kwenye maombolezo watu wataanza kumlilia na nyerere - maana kuwatenganisha ni vigumu hawa makomredi. duh inauma sana.
 
Asanteni wakuu kwa archives. Kama itawezekana tupate maelezo kidogo kwa kila picha itakayotundikwa angalao tujue matukio hayo kama ambazo chache zimeeleza.
 
Superman, you are really supper!!! Asante sana kwa kazi nzuri na ubunifu pia. At least tumeweza pia kuoana matukio ya kazi zake officially, politically and socially badala ya kutuma salam za rambirmbi tu. Keep it up man!
 
Kuuliza si ujinga kwakweli me na picha ila siju kupost munielekeze naomba msaada wenu. Thnks
 
..Superman, kwenye hii picha huyo aliyekaa wa pili kutoka kushoto ni Chifu Abdalah Fundikira au nani??


Ndiyo, huyo ni Fundikira. Wa kwanza ni Paul Bomani.

Naikumbuka miaka hiyo. Nilikuwepo katika Tanganyika ile ingawa nilikuwa bado kijana.
 
Back
Top Bottom