,Edo,alitaka cheo cha katibu mkuu wa CCM kipigiwe kura na siyo mtu kupewa bila ya idhaa ya wananchi! unajua wakati ule katibu mkuu wa ccm alikuwa mara mbili ya waziri mkuu kwa cheo. mshikaji wake Yona mwakasendo naye alipigwa sindano ya sumu ! nakuambia heri kufa kwa ukomunisti maana nchi hii ilikuwa inatisha kwa watu kupotea kisirisiri. wewe ona kifo cha kanali Andrew Shija mpaka leo hakieleweki! KIfo cha koliimba kutetetmeka katika spika wakati anajieleza! KIfo cha sokoine kupata ajali hakieleweki! Haya yote yatakuja eleweka tuu na wahusika kuanikwa wazi wapende wasipende!
wengine wanasema ni baba wa nation la tz, cjui wewe unasema ni naniwho is mchonga i don't him
...Hivi yule jamaa alisepa kurudi kwao bondeni baada ya ile movie?Dumisani Dube anaujua ukweli zaidi.
Vijana wengi hawamjui, na historia yake haitiliwi maanani. Hakuna hata ka documentary kamoja juu ya maisha yake?
Palikuwepo kikundi cha maigizo UDSM enzi hizo chini ya Prof. Penina Mhando, walikuwa na igizo la sokoinne, binafsi nilipata bahati ya kuliangalia kundi hilo Pugu sec school siku hizo nikiwa dent nakumbuka yafuatayo
1. Sokoinne akiwa kazini ofisini huku akisikia na kuona vitu vya kishirikina / kiuchawi ofisini mwake
2. Njama za kumwangamiza Sokoinne aliyekuwa na dira ya nchi inapoelekea
3. Baada ya kifo chake palikuwepo na wasafiri waliofika njia panda wakaanza kubishana wachukue njia ipi ya kulia au kushoto
4. Sokoinne akiwa peponi huku akihuzunika kwa vile wasafiri wale waliokosa ufahamu wa kujua ni njia ipi inawapeleka waendako.
5. Hitimisho la igizo lilikuwa walimuua Sokoinne kwa hila wakati wauaji wake hawana fikra wala ufahamu wa kutosha wa kuingoza tanzania
Kila ninapokumbuka igizo lile na jinsi ninavyoiona ccm inavyotawala tanzania hakika Prof. Penina Mhando na kundi lake walikuwa ni manabii, yote waliyolitabiria taifa hili katika igizo lile yametimia na kupitiliza
Tunaye Sokoine aliye Hai- EL, kijana, mchapakazi, mmasai. Anajua kutoa maagizo na kufuatilia. Huchukia mambo yakienda vibaya. Si unaona anavyosimamia ujenzi wa madarasa?
Sokoine mpaka wakati anafariki alikuwa na pea mbili za viatu, EL anamiliki nini hivi sasa mpaka tumlinganishe na Sokoine?Mzee Mwanakijiji,
Heshima yako kwanza,
......Katika mkutano huo, mwandishi mmoja wa habari ambaye hakutumia utaratibu wa kunyoosha mkono kuuliza swali, na alikuwa nyuma, aliamua kupaza sauti gafla, na kusema kuwa, miongoni mwa wagombea wa CCM kuna anayefaa kuongoza kwasababu ni mchapa kazi, kijana, na ni Mmasai kama alivyokuwa Sokoine.
Mwalimu.......Alisema Watanzania watafanya makosa kudhani kuwa wamasai wote ni kama Sokoine. Pamoja na madaraka aliyokuwa nayo, Sokoine alikufa na pair mbili za viatu.