Tunamkumbuka Dr. Slaa

Ni miezi miwili imepita watanzania lazima mtaanza kumkumbuka DR.Slaa mtu makini na aliyekuwa na nia ya dhali ya kuibalisha tanzania ki uongozi na kuwakomboa ninyi kwenye wimbi la umaskini na kuporwa raslimali za nchi yenu.

Leo yote aliyoyasema wakati wa kampeni ndiyo hayo hayo yanatokea ni kama alikuwa amefuniliwa na mwenyezi mungu kuja kutuokoa sisi watu wake, leo hii mnaona tatizo kubwa mno la uongozi wa nchi yetu. Huhitaji elimu hata moja kujua kwamba tatizo hili sasa ni sugu na lilipofikia pahala halina matibabu (Donda ndugu), viongozi wanakataa kuwajibika hata kwenye makosa ambayo yapo wazi wazi ya kiutendaji na kibaya zaidi hakuna wa kuwawajibisha.


Hivi tunaenda wapi? kwa mfano: tulio la Juzi la Mabomu waziri kwenye dhamana ya Ulinzi anasema waziwazi hatawajibika, na wakati huo huo waziri mwenye dhamana na nishati na madini naye anakurupuka na kusema mgawo wa umeme Tanzania hauishi hadi 2033 hivi jamani hii nchi ina viongozi kweli? nchi yenye madini, gesi asilia na hadi uranium unasema mgawo mpaka 2033 na bado upo madarakani?


Haya mengine ndiyo simanzi zaidi yaani watu zaidi ya 30 wanakufa, mbunge anatoa hoja kutaka jambo hili kuongelewa as emergence katika bunge, hoja inapanguliwa - sasa emergency katika taifa hili ni ipi? kumlipa dowans?

Tutamkumbuka DR. Slaa kwa sababu maisha ya mtanzania yatazidi kuwa magumu na yasiyo na matumaini kabisa.

mchango wake unaonekana!!!
 
Alikuja kwa walio wake wakamkataa,au waliladhimishwa kumkataa.yaani huku mby 2na ham na rais we2 mpaka bac!
 
E mungu ibariki Tanzania. Mambo yalivyo, afadhali mtu usiangaike kuyajua kwani ni wizi mtupu. The country is moving as if we don't have head of state?
 
hakuna hata anayemkumbuka slaa labda wewe tu na wenzio ambao mmepinda lakini watu wote wenye akili zao zilizotulia wala hata hawamkumbuki. Lako hilo unalo babuuuu

bora useme ukweli...wenye akili zilizotulia,a.k.a bongo lala au akili mgando au vilaza ndo hawana hata uwezo wa kufikiri,akili zimetulia wala hazifanyi kazi ndo mana hawawezi kukumbuka maneno ya dr wa ukweli,dr.slaa.
 
:hand: Kwakweli Dr.Slaa tutamkumbuka haswaaaaa. na sifikirii kama bado kuna mtanzania ambaye ajaona nia na sababu ya kwanini vijana wenye uelewa na mambo ya nyakati walitaka Dr. Slaa aongoze nchi. Kwa hali ya sasa hivi hata miezi mitatu haijaisha tumekua na kilio cha kufa na kusaga meno. kila kona maisha yamekua magumu, si kwa wafanyabiashara na wala si kwa wafanyakazi wa serikali kote hali ni mbaya. Walai 2015 tusifanye mchezo kama ilivyofanyika Novemba 31/2010. Tanzania ni nchi yenye utajiri wa hali ya juu ni ahibu kuona wananchi wanateseka kiasi hiki, leo hii nimesikia kupitia kwenye redio kwamba wazungu wamepata Tanzanite yenye uzito takribani kili mbili na nusu, wazungu wanaenda kufaidika Watanzania tunabaki kwenye giza.
Duh!! HAKIKA TUTAMKUMBUKA Dr.Slaa.
 
Wahenga wanasema ukimkimbiza kichaha watu watakuona kichaha....

Ikulu inasema Dr Slaa hana ubusara amechanganyikiwa
UVCCM inasema Dr Slaa hana ubusara amechanganyikiwa
Tendwa--Msajili naye inasema Dr Slaa hana ubusara amechanganyikiwa
TISS inasema Dr Slaa hana ubusara amechanganyikiwa

Hivi hao wote wanakimiza mtu wanayemjua ni kichaha..... wanataka sisi tuwaeleweje?

Na je wale watu 2milion waliompa kura?
Na hao wanaokuja kwenye mikutano yao vipi?
 
Back
Top Bottom