Tunamkumbuka Dr. Slaa

Nonda si kweli kushindwa kuungana kwa wapinzani kunawapa nguvu ccm,maana ni bora kuwepo wapinzani wachache wenye nia ya kweli ya kulitumikia taifa hili,ubora wa jeshi haupimwi kwa wingi wake bali uchache wenye nia ya kweli...
Saa ya ukombozi ni sasa

Pia anapaswa kujua kuwa vyama kusimamisha mgombea mmoja tukiwa na tume hii hii ya uchaguzi isingesaidia kitu
 
WANANCHI HATUKO SALAMA TENA NA MALI ZETU, KIIO KILA LEO NA MAYATIMA
KUONGEZEKA HIVYO SERIKALI NZIMA IJIUZULU HATA KABLA YA MAANDAMANO
YA KUTETEA 'UHAI WA WENZETU' KUANZA KOTE NCHINI


Mheshimiwa Kikwete kama amiri jeshi mkuu ajiuzulu pamoja na serikali yake.

Jukumu la msingi halijazingatiwa; kuna watu wanasinzia kwenye majukumu nyeti na sasa kutugharimu kiasi hini, wananchi hatuko salama!! Tusianze kuzungusha kiswahili hapa ni uhai umepotea kwa uzembe!!! Hawa mayatima wanahitaji sauti zetu!!

Hatutaki tena tume kwani hata kule Mbagala chombo kama hicho hakikutusaidia zaidi ya kuwapa wanasiasa na makampuni ya kibiashara kujinadi kwenye kioo cha televisheni mgongoni mwa msiba na damu kwa wengine.

Jukumu la kwanza la kuhitajika uwepo wa serikali katikati yetu NI KUHAKIKISHA USALAMA KILA MMOJA WETU NA MALI ZETU. Kwa mtaji hizi picha nilizoona, serikali nzima ya CCM ijiuzulu mara moja

Mauaji Arusha walitupuuza kana kwamba kuliuaua nzi tu. Kule kwenye mashamba ya mpunga wala hawakujishughulisha kitu kuwajibika mtu. Sasa kama kweli kuna JAMBO AMBALO KIUKWELI KABISA KINATUHITAJI KUANDAMANA MPAKA KUELEWEKE NI KATIKA KUTETEA UHAI WA WENZETU.

Kama tutaona vifo hivi kama vile ni ya 'akina wale' na kwamba sisi wengine hatuhusiki basi hapo ndipo kiama chetu kinapoanzia. Kwa vifo hivi vyote 17 taifa tumepata yatima wangapiii?????????????
 
Nonda si kweli kushindwa kuungana kwa wapinzani kunawapa nguvu ccm,maana ni bora kuwepo wapinzani wachache wenye nia ya kweli ya kulitumikia taifa hili,ubora wa jeshi haupimwi kwa wingi wake bali uchache wenye nia ya kweli...
Saa ya ukombozi ni sasa

kudos. Una busara sana
 
Ni miezi miwili imepita watanzania lazima mtaanza kumkumbuka DR.Slaa mtu makini na aliyekuwa na nia ya dhali ya kuibalisha tanzania ki uongozi na kuwakomboa ninyi kwenye wimbi la umaskini na kuporwa raslimali za nchi yenu.

Leo yote aliyoyasema wakati wa kampeni ndiyo hayo hayo yanatokea ni kama alikuwa amefuniliwa na mwenyezi mungu kuja kutuokoa sisi watu wake, leo hii mnaona tatizo kubwa mno la uongozi wa nchi yetu. Huhitaji elimu hata moja kujua kwamba tatizo hili sasa ni sugu na lilipofikia pahala halina matibabu (Donda ndugu), viongozi wanakataa kuwajibika hata kwenye makosa ambayo yapo wazi wazi ya kiutendaji na kibaya zaidi hakuna wa kuwawajibisha.


Hivi tunaenda wapi? kwa mfano: tulio la Juzi la Mabomu waziri kwenye dhamana ya Ulinzi anasema waziwazi hatawajibika, na wakati huo huo waziri mwenye dhamana na nishati na madini naye anakurupuka na kusema mgawo wa umeme Tanzania hauishi hadi 2033 hivi jamani hii nchi ina viongozi kweli? nchi yenye madini, gesi asilia na hadi uranium unasema mgawo mpaka 2033 na bado upo madarakani?


Haya mengine ndiyo simanzi zaidi yaani watu zaidi ya 30 wanakufa, mbunge anatoa hoja kutaka jambo hili kuongelewa as emergence katika bunge, hoja inapanguliwa - sasa emergency katika taifa hili ni ipi? kumlipa dowans?

Tutamkumbuka DR. Slaa kwa sababu maisha ya mtanzania yatazidi kuwa magumu na yasiyo na matumaini kabisa.

kwa hakikia inasikitisha sana, sijui kwa nini watanzania hatuoni?
 
Kwenye kafara unamaanisha nini mkuu?
CCM hawawezi kukubali vyama vya upinzani waungane kwa hiyo watatumia njia yeyote kuwarubuni...cuf ilionyesha dalili ya kutumika 2010.
Wapinzani wa kweli ni wananchi wachukia ufisadi na wapenda maendeleo ya kweli na haki. Ndio wapiga kura... naamini wengi walifanya kazi yao 2010 BUT NEC imefanya mambo yake.
Nani wa kulaumiwa?
Mkuu,
Ile nafasi aliyopata Mbowe bungeni ilikuwa ni nafasi ya Dr. Slaa.
Lakini Dr. Slaa kama angegombea ubunge basi ni 100% kuwa angerudi bungeni.
Pengine atafanya kama alivyofanya Mbowe na Mrema.

Nimesema kua Dr. Alitoa kauli ya "ninagombea Urais mara moja". Hii haikuwa kauli makini kwa mwanasiasa.

Lakini pia kama hakuna Katiba mpya mpaka tunaingia uchaguzi wa 2015 ni wazi CCM wataendelea na uchama dola wao na hivyo watarudi madarakani kwa kura au kwa kuchakachua.
 
Nonda japo maneno yako ni ya msingi na yana ukweli ndani yake lakini maelezo yako yana angalia upande mmoja wa shilingi. Umeongelea faida ya vyama kuungana lakini si hasara yake.

Mimi nadhani solution ni kuimarisha vyama vyetu viwe competitive. Hiyo inaanza na vyama hivyo kuwa na uongozi makini na wenye vision. Vyama vingi vya upinzani havi tumii fursa za kujiendeleza na kujiongezea umaarufu. Angalia kama mabomu ya Gongo la Mboto. Ni vyama vingapi vya upinzani vimeonyesha leadership? Vingapi vimetoa matamshi? Vingapi vime kuwa proactive na kujaribu kusaidia waathirika iwe kwa hali au mali?
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...lahi-ya-taifa-they-are-just-another-tool.html
Mkuu,
Pitia hiyo mada kwenye link, halafu uone kama ushirikiano wa vyama hauwezekani.
Kuungana kwa maana ya kuungana sio wazo langu ila kushirikiana inawezekana, sijui tuite alliance? Na sio muungano, union.

Kama ulivyosema kuna hasara ya kushirikiana kwa vyama lakini hasara hizi ni kubwa kuliko faida?

Mkuu, Kuna faida kubwa zaidi kwa vyama hivi zaidi ya kuibwaga CCM na CCM kuonja kukalia viti vya upinzani bungeni? Wananchi watajisikia vipi siku CCM wakiachia madaraka?

"Tatu ni swala la kwamba je hata wange ungana wange shinda? Ukiacha Chadema angalia kura za uraisi na hata ubunge walizo pata vyama vingine. Hata wange ungana isinge tosha kuiondoa CCM madarakani wala kuipa majority upinzani bungeni."

Kwa hiyo huamini kuwa Ushindi wa CHADEMA ulichakachuliwa?
Anyway, bado ushahidi haujawekwa hadharani…na mimi ni katika tunaosubiri kuona ushahidi huo.

Mwanafsafa, kama upinzani ungesimamisha mgombea mmoja na kama hilo lingetangazwa mapema basi wananchi wangeamini kuwa sasa upinzani unastahili kupewa hatamu za utawala, kwa hiyo kura zao zingeongezeka maradufu, nina imani ya 99% kuwa wangeshinda majimbo mengi ya ubunge na hata kura za urais.

"siasa za unafiki na ugannga njaa kuchomana visu mgongoni"

Kutokana na sababu hizo ulizozitaja ndio hapo ninapoona kuwa wanasiasa wetu bado hawajakomaa vya kutosha. Na sijui ni lini chama kimoja kimoja vitaweza kujiimarisha na kuwa tayari na uwezo wa kuishinda CCM katika hali yake ya Chama dola.

Kwenye thread moja umesema haya
As much as I respect Dr. Slaa I don't think he will be the leader of changes in Tanzania. Sisemi kwamba hana nafasi yake. La hasha. Ila kwangu mimi naona ni mtu mwingine kabisa ambae ata kuja kuongoza ukombozi wa kweli. Si vibaya lakini kwa sababu hata kupigania uhuru hakuanza Nyerere japo historia inaonyesha yeye ndiyo kiongozi wa mkakati wa kudai uhuru.
Wengi wanaona CHADEMA watashinda 2015, sasa nani katika Chadema looks presidential material kama Dr. unamtoa hesabuni?
Kwa maneno mengine , unamaanisha tutaendelea kuwaona CCM kwa miaka mengine mingi?
 
Pia anapaswa kujua kuwa vyama kusimamisha mgombea mmoja tukiwa na tume hii hii ya uchaguzi isingesaidia kitu
Mbalinga.
Wazo lako ni kuwa kila chama chenye usajili wa kudumu kisimamishe mgombea? Hili litavisaidia vyama vya upinzani?

Ooopps. nimekumbuka kwako chama cha upinzani ni kimoja tu!!
 
Nonda si kweli kushindwa kuungana kwa wapinzani kunawapa nguvu ccm,maana ni bora kuwepo wapinzani wachache wenye nia ya kweli ya kulitumikia taifa hili,ubora wa jeshi haupimwi kwa wingi wake bali uchache wenye nia ya kweli...
Saa ya ukombozi ni sasa

Mkuu.
You are more than right. Kushindwa kuungana kwa wapinzani kunawafanya CCM kuwa dhaifu.
Sikuwa nimeliangalia hili suala katika mtazamo kama wako. Tuendelee kuwa mmoja mmoja, tusishirikiane.Tutaipunguza nguvu kwa kasi CCM.
Saa ya kupiga usingizi ni sasa.... nguvu ya umma.
 
kuungana upinzani sio suluhisho, kwani inawezekana kwa kuungana upinzani wengine wakrudi ccm. kila chama kisimame chenyewe na sera zake ndizo zitakazokipelekea kuchukua hatamu.
kama yapo aliyosema li pumba naomba utujuze kama tulivyojuzwa ya Dr Slaa.
Wakati tunamkumbuka Dr.Slaa tusisahau kushindwa kwa Upinzani kushirikiana na kumsimamisha mgombea mmoja kwa ajili ya kuunganisha nguvu kuitoa CCM ndiko kunakoifanya CCM kuwa na jeuri waliyonayo na watakayokuwanayo kwa muda mrefu.

Usisahau kuwa nchi nyengine wananchi wake wanapochukizwa na watawala na pale maji yanapowafika shingoni huamua kuwawajibisha wasiowajibika. Unamkumbuka Ben Ali? Mubarak?.....sisi bado tunalinda uchovu wetu...amani na utulivu.

Lakini usisahau pia kuwa Mbowe alijua kuwa si presidential candidate makini, kwa hiyo ujio wa Dr. Slaa ulikuwa ni chaguo zuri lakini pia ilikuwa ni kumtoa kafara. Pia uamuzi wa kukurupuka.Hata hivyo hili lilinogesha uchaguzi wa Rais.

Pia Dr. Slaa alitoa tamko ambalo naona kama "atakula matamshi yake" basi anaweza kuwa branded kiaina. Alisema anagombea urais mara moja tu. Sijui kwa nini alitoa kauli hii.
well, kama unavyosema hapa kweli tunamkumbuka Dr. Slaa.
Jee kuna anaekumbuka Prof. Lipumba alisema nini kuhusu kuichagua CCM?
 
kuungana upinzani sio suluhisho, kwani inawezekana kwa kuungana upinzani wengine wakrudi ccm. kila chama kisimame chenyewe na sera zake ndizo zitakazokipelekea kuchukua hatamu.
kama yapo aliyosema li pumba naomba utujuze kama tulivyojuzwa ya Dr Slaa.
Peck.
Soma post # 6 wanaojua wameshatujuza.
Halafu, mara moja hii umeshasahau yote ya kampeni zilivyoendeshwa?
Kweli nguvu ya umma.
 
kila chama kisimame chenyewe na sera zake ndizo zitakazokipelekea kuchukua hatamu.
kama yapo aliyosema li pumba naomba utujuze kama tulivyojuzwa ya Dr Slaa.
Peck
Hizo nyekundu umekosea? au dharau intended?
Kazi kweli kweli!!!!
Kwa taarifa yako tu ..mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa.
 
Mkuu Nonda,

As always I respect your views but most importantly I like that you argue respectfully. So heshima kwako mkuu.

Mkuu chukulia mfano wa mchakato wa Chadema kuwa chama kikuu cha upinzani Bungeni na kuunda baraza kivuli. Umeona jinsi walivyo kuwa wana sumbuliwa na vyama vingine? Umeona ilivyo kuwa ngumu kuvi shirikisha? Hapo ni kwenye kambi ya upinzani Bungeni tu je inge kuwa ni swala la wao kuunda serikali inge kuaje? Kama mkuu mmoja alivyo sema swala si kuungana tu bali kuangalia una ungana na nani. Hauwezi kuungana na mtu for the sake of it. Kwa mfano sasa unge shauri Chadema waungane na CUF?

Kuhusu uchaguzi wa 2015 it's too early to say mkuu. Miaka mitano ni michache ila kwenye siasa ni mingi. 2005 nani ange dhani Dr. Slaa ange pata umaarufu aliopata? In 2005 nani ange dhani Chadema wange shika nafasi ya pili? Change takes time. Factors nyingi sana zinaingia kwenye change. Sisi watu hatupa tayari kwa mabadiliko laa sivyo 2010 kinge eleweka. Kwa sababu haki kueleweka it shows we are not ready for change. Badp tupo kwenye early stage ya kuongea tu na si kutenda. By the time tukiwa tayari kutenda I assure you haita kuwa kumuingiza Slaa ikulu.

Kuhusu CCM kuchakachua matokeo mkuu that depends who you ask. Kama ulivyo sema mwenyewe ushahidi hauja tolewa wa kutosha. Unless sasa hivi wewe unipe figures zenye uhakika (si kubuni) kwamba fulani ali pata asilimia fulani. Ila hamna haja ya kubishana kuhusu hilo kwa sasa kwa sababu Watanzania wennyewe pamoja na huyo anaye dai kuibiwa wame kubali yaishe mpaka 2015.

Ila mkuu trust me Tanzania bado sana. We imagine Dowans, Richmond, 2009 Mbagala, madai ya uchaguzi kuchakachuliwa, Arusha, juzi Gongo la Mboto. Yote haya ndani ya miaka 6 wananchi hatuja fanya chochote ndiyo una taka kuniaminisha kwamba sisi ni jamii iliyo tayari kwa mabadiliko? Vyote hivyo vina tokea tunge kua nchi nyingine si tungesha anza kuandamana?
 
Dr slaa ana kazi maalum sasa hivi ya kutengeneza akina slaa wengi ndani na nje ya chadema, bado ni kiongozi wetu tunamtambua na tunamwamini, kwa chahcu ya chadema na slaa leo vijana wengi wa vyuo vikuu ni chadema damu, kwa chahcu ya chadema na slaa leo hii great thinkers wengi ni wafuasi wa chadema, kwa ajili ya chachu ya chadema na slaa leo hii wananchi wengi wakulima, wasomi, wafanyakazi, wanasiasa na wafanyabiashara matumaini yao yapo kwa chadema. Dr slaa bado tunaye na anaendelea kutufungua macho ni kiongozi imara.
 
Mkuu chukulia mfano wa mchakato wa Chadema kuwa chama kikuu cha upinzani Bungeni na kuunda baraza kivuli. Umeona jinsi walivyo kuwa wana sumbuliwa na vyama vingine? Umeona ilivyo kuwa ngumu kuvi shirikisha? Hapo ni kwenye kambi ya upinzani Bungeni tu je inge kuwa ni swala la wao kuunda serikali inge kuaje? Kama mkuu mmoja alivyo sema swala si kuungana tu bali kuangalia una ungana na nani. Hauwezi kuungana na mtu for the sake of it. Kwa mfano sasa unge shauri Chadema waungane na CUF?
Mkuu,
Pitia hizi links mbili
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-david-kafulila-walipaswa-kutumia-busara.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/110966-vyama-vya-upinzani-vyakubali-uamuzi-wa-mbowe.html

Change takes time. Factors nyingi sana zinaingia kwenye change. Sisi watu hatupa tayari kwa mabadiliko laa sivyo 2010 kinge eleweka. Kwa sababu haki kueleweka it shows we are not ready for change. Badp tupo kwenye early stage ya kuongea tu na si kutenda. By the time tukiwa tayari kutenda I assure you haita kuwa kumuingiza Slaa ikulu.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/111649-tukiamua-kuandamna-a-word-of-thought.html

Ila mkuu trust me Tanzania bado sana. We imagine Dowans, Richmond, 2009 Mbagala, madai ya uchaguzi kuchakachuliwa, Arusha, juzi Gongo la Mboto. Yote haya ndani ya miaka 6 wananchi hatujafanya chochote ndiyo una taka kuniaminisha kwamba sisi ni jamii iliyo tayari kwa mabadiliko? Vyote hivyo vina tokea tungekua nchi nyingine si tungesha anza kuandamana?
Mkuu,
WanaChadema wako tayari..ila wengine ndio wamelala bado..umeona hapo wanataka sasa tuandamane kama wananchi tukiwa kundi moja...Tukiweza kuwawajibisha CCM na serikali yake, watuambie kila mmoja ajitegemee kivyake vyake. Hivi kwani miujiza bado hutokea duniani, hasa sehemu hizi za Afrika Mashariki?
Good news, pandemic ya maandamano imeingia Djibout sasa, sasa sijui ndio inateremka kusini?
 
(1) Naamini alichotamka Dr. Slaa ni kwamba angekuwa Rais kwa kipindi kimoja, na sio kugombea kwa kipindi kimoja. Bado hajawa Rais kwa kipindi kimoja. Ni sala yetu kwamba atagombea tena, na atashinda. Wakati huu alishinda, wezi wakaiba kama ilivyo kawaida yao.

(2) Tunakumbuka aliyosema Dr Slaa na sio kwamba tunamkumbuka Dr Slaa. Si bado tunaye? Si bado ni kiongozi wetu? Hata leo angesema Watanzania fanyeni hivi au vile angeitikiwa zaidi ya Kikwete. Leo hii Kikwete angesema wananchi kusanyikeni Jangwani nina jambo la kuwaambia ni watu wachache sana watakwenda. Ila Slaa angetangaza hivyo pangejaa mno. Hata Mwema na Shimbo wakitishia watu na vigobole vyao bado pangejaa tu.

(3) Hali ni ngumu kweli kweli. According to the NBS (see reports at ippmedia.com) the combined annual rate of inflation is now 17.7%. Sasa hawa akina Kikwete walikabidhiwa uchumi wenye mfumuko we bei wa 4.9% na wameufikisha hapa! Na bado kabisa, they are not done!

(4) JWTZ lina kipaumbele gani? Ni kununua tu magari ya fahari kwa ajili ya viongozi? Ni kupandishana vyeo tu? Mbona wanao sasa utitiri wa ma-Brigadier Generals? Iweje wadai munitions dump lazima iwe Gongolamboto? Ili kulinda uwanja wa ndege ni lazima mabomu yakae pale? Na iweje yasikae chini ya ardhi? Fedha mseme hamna na huku mnaongeza ma-vx tu?

Nahitimisha kwa kukumbushia jambo muhimu alilosema Dr. Slaa. Kukata tamaa ni kosa lisilosameheka. Watanzania tusikate tamaa.
 
Yes, kwa njisi mambo yanavyoenda hapa nchini ni lazima mtu ukumbuke maneno na DR. Slaa wakati wa kampeni yaani inauma sana, leo usiku wamevuja vibanda vya wamachinga pale mahakama ya ndizi wameharibu mali zao - hivi jamani tunaenda wapi? kulikuwa hakuna njia nyingine ya kutumia busara tu kuwaondoa hao wamachinga mpaka uvunje na kuharibu mali zao?

Watawala nawambia hivi kama mnafikiri hii nchi mtaongoza milele sahauni na siku zenu za kukaa madarakani zinahesabika - vilio vya wananchi lazima vije na suluhisho.

Mnaovunja amani ni ninyi na wala si CHADEMA, na wahaini ni nyie wala si CHADEMA - WANANANCHI TUMEWACHOKA. mnaiangusha serikali yenu wenyewe na malipo kawaida huwa ni hapa hapa duniani.
 
ni miezi miwili imepita watanzania lazima mtaanza kumkumbuka dr.slaa mtu makini na aliyekuwa na nia ya dhali ya kuibalisha tanzania ki uongozi na kuwakomboa ninyi kwenye wimbi la umaskini na kuporwa raslimali za nchi yenu.

Leo yote aliyoyasema wakati wa kampeni ndiyo hayo hayo yanatokea ni kama alikuwa amefuniliwa na mwenyezi mungu kuja kutuokoa sisi watu wake, leo hii mnaona tatizo kubwa mno la uongozi wa nchi yetu. Huhitaji elimu hata moja kujua kwamba tatizo hili sasa ni sugu na lilipofikia pahala halina matibabu (donda ndugu), viongozi wanakataa kuwajibika hata kwenye makosa ambayo yapo wazi wazi ya kiutendaji na kibaya zaidi hakuna wa kuwawajibisha.


Hivi tunaenda wapi? Kwa mfano: Tulio la juzi la mabomu waziri kwenye dhamana ya ulinzi anasema waziwazi hatawajibika, na wakati huo huo waziri mwenye dhamana na nishati na madini naye anakurupuka na kusema mgawo wa umeme tanzania hauishi hadi 2033 hivi jamani hii nchi ina viongozi kweli? Nchi yenye madini, gesi asilia na hadi uranium unasema mgawo mpaka 2033 na bado upo madarakani?


Haya mengine ndiyo simanzi zaidi yaani watu zaidi ya 30 wanakufa, mbunge anatoa hoja kutaka jambo hili kuongelewa as emergence katika bunge, hoja inapanguliwa - sasa emergency katika taifa hili ni ipi? Kumlipa dowans?

Tutamkumbuka dr. Slaa kwa sababu maisha ya mtanzania yatazidi kuwa magumu na yasiyo na matumaini kabisa.

hakuna hata anayemkumbuka slaa labda wewe tu na wenzio ambao mmepinda lakini watu wote wenye akili zao zilizotulia wala hata hawamkumbuki. Lako hilo unalo babuuuu
 
hakuna hata anayemkumbuka slaa labda wewe tu na wenzio ambao mmepinda lakini watu wote wenye akili zao zilizotulia wala hata hawamkumbuki. Lako hilo unalo babuuuu

mibange ya asubuhi asuhi so mizuri itakuharibu akili bado familia inakuhitaji bwana mdogo.
 
Back
Top Bottom