Tunalishwa mchanganyiko wa sembe na vumbi. TBS, TFDA na serikali mko wapi?

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Haihitaji tume huru, wala uchunguzi wa kina. Hili ni jambo ambalo liko wazi bila shaka hata wanaohusika wanajua. Kumekuwa na idadi kubwa ya viwanda vya kusaga sembe mitaani kisha wanachapisha mifuko na nembo zao wanaingiza mitaani. Sembe ambayo haina ubora kutokana na jinsi inavyotengenezwa katika mazingira machafu. Ukifika Tandale na maeneo ya Manzese shughuli inafanyika bila kificho. TBS haitambui kuwa madukani kuna sembe chungu mzima ambayo haina nembo yao? TFDA hawajui kuwa kuna viwanda vinatengeza vyakula katika mazingira yasiyofaa? Serikali, hasa katika maeneo yanayohusika hawalitambui hili? Au ndio bado mambo yaleyale ya maigizo ya kisiasa?
 
Back
Top Bottom