Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
Mimi nadhani si kazi kubwa sana kubaini ni nani au akina nani behind this act – na hasa iwapo vyombo vya usalama havitaweza kuwakamata. Ni watu ambao hawakamatiki katika nchi hii – maana wako juu ya sheria – hufanya jinai yoyote watakayo na serikali ya Muungwana inabakia kuwa impotent.
Kwanza kabisa – ile kesi ya Kubenea kumwagiwa tindikali imefikia wapi? Hakuna chochote kinachoendelea na nimesikia mashahidi wanatishwa kwenda kutoa ushahidi – na waliokwenda wamepotea (disappeared) bila kunekana.
Pili kesi moja ya kubwa ya EPA (ile ya Kagoda) bado haijatinga mahakamani, pamoja na kuwepo ushahidi tosha – wa kutoka CRDB – wa nani (au akina nani) walilipwa yale mabilioni in cash – over the counter. Takukuru wameshindwa kupata ushahidi huo wa wazi kwa sababu walipwaji hao wako above the law kuliko Watanzania wengine. (Linganisha na watuhumiwa hawa wa wizi wa TTCL/TRA – kwa kuwa ni wale walio chini ya sheria.)
Tatu hivi karibuni gazeti hilo la Kubenea limemuanika waziwazi EL kuhusu suala la Richmond baada ya kuandika tuhuma mpya kabisa dhidi yake za kampuni ya CDC ya Canada ya kuzalisha umeme, kampuni ambayo EL alifuta tenda yake na badala yake kuiingiza Richmond!
Tuhuma hizi mpya bila shaka zimemuumiza sana EL ambaye siku chache tu zilizopita ‘alijitetea' katika TBC1 akimtumia swahiba wake Tido kuhusu kashfa ya Richmond inayojulikana. Kuja kwa hii mpya ya CDC ambay ilikuwa bado haijulikani bila shaka kumemuumiza sana EL – tena sana – maana alifikiri alikuwa amelimaliza suala zima la Richmond.
Kwa hivyo wana-JF mtajua ni akina nani wako behind this latest attempt on the life of Kubenea. Nadhani mwenyezi Mungu anamuweka ili amalize kile alichomtuma kuikomboa nchi hii kutoka kwa makucha ya mafisadi.