Tunalaani kitendo hiki, hakivumiliki!

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Usiku wa kuamkia leo tumepata taarifa za kuvamiwa eneo ambalo alikuwa akiishi Said Kubenea wa MwanaHalisi huku waliofanya uvamizi wakiwalazimisha vijana wa eneo hilo kusema alipo Kubenea.

Taarifa hizi zinadokeza kuwa pamoja na vijana hao kuwafahamisha kuwa Kubenea kahama takribani mwezi mmoja uliopita wavamizi hawakuacha kuwatesa vijana wa mtaa huo na kisha kutokomea kusikojulikana.

Pamoja na kuwa Said katoa taarifa hizi Polisi nao kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, sisi kama JamiiForums tunapinga kwa nguvu namna yoyote ile ya kujaribu kuwanyamazisha waandishi wa habari na vyombo vyao vya habari (si MwanaHalisi pekee) ndani ya nchi yetu. Tunalaani kitendo hiki kwa nguvu zote na kuliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hili ili ukweli ujulikane (ukizingatia kuwa wavamizi walienda kwa lengo la Kubenea na imethibitika).

Tunaamini jeshi letu halitosita kuchukua hatua pindi wahusika watakapobainika na hata kuweza kutoa taarifa juu ya nini walifuata na nani aliwatuma na kwanini.
 
mimi hapo kwenye blue mkuu huwa hawa polisi wetu wananitatiza sana....hivi watasema kweli?
 
Naungana nawe kulaani kwa nguvu zangu zote majaribio yoyote yale ya kunyamazisha wanahabari na vyomba vya habari.
 
So, mafisadi bado wanamkaba koo mwanaharakati huyu, mpiganaji wa kikweli-kweli wa ufisadi hapa nchini! Mi nashangaa kwa nini wabaya wake wale wa awali (kesi ya tindikali) hawajanda jela hadi sasa. Hii inaonyesha nguvu za pesa za mafisadi na udhaifu wa vyombo vyetu vya sheria ambavyo vimewekwa mfukoni na hao mafisadi.
 
Kwenye red: Shame upon JK and his poor handling of the ufisadi war.
 
tena laana hii iangukie serikali ambayo ndiyo mdhamini mkuu wa mambo hayo ya
kighafdhuna, na kifirauni
 
Usiku wa kuamkia leo tumepata taarifa za kuvamiwa eneo ambalo alikuwa akiishi Said Kubenea wa MwanaHalisi huku waliofanya uvamizi wakiwalazimisha vijana wa eneo hilo kusema alipo Kubenea.

Taarifa hizi zinadokeza kuwa pamoja na vijana hao kuwafahamisha kuwa Kubenea kahama takribani mwezi mmoja uliopita wavamizi hawakuacha kuwatesa vijana wa mtaa huo na kisha kutokomea kusikojulikana.

Pamoja na kuwa Said katoa taarifa hizi Polisi nao kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, sisi kama JamiiForums tunapinga kwa nguvu namna yoyote ile ya kujaribu kuwanyamazisha waandishi wa habari na vyombo vyao vya habari (si MwanaHalisi pekee) ndani ya nchi yetu. Tunalaani kitendo hiki kwa nguvu zote na kuliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hili ili ukweli ujulikane (ukizingatia kuwa wavamizi walienda kwa lengo la Kubenea na imethibitika).

Tunaamini jeshi letu halitosita kuchukua hatua pindi wahusika watakapobainika na hata kuweza kutoa taarifa juu ya nini walifuata na nani aliwatuma na kwanini.

Watanzania tunalaani vitendo hivi vinavyoshamiri katika nchi yetu. Hata wauaji wa yule mwalimu wa chuo kikuu hawajapatikana wanatafuta roho ya Kubenea tena. Serikali ya Mafisadi ilaaniwe
 
Nionyesheni ni nani aliyewatuma hawa kufanya vitendo hivyo viovu ili niwashughulikie. I mean it!
 
Usiku wa kuamkia leo tumepata taarifa za kuvamiwa eneo ambalo alikuwa akiishi Said Kubenea wa MwanaHalisi huku waliofanya uvamizi wakiwalazimisha vijana wa eneo hilo kusema alipo Kubenea.

Taarifa hizi zinadokeza kuwa pamoja na vijana hao kuwafahamisha kuwa Kubenea kahama takribani mwezi mmoja uliopita wavamizi hawakuacha kuwatesa vijana wa mtaa huo na kisha kutokomea kusikojulikana.

Pamoja na kuwa Said katoa taarifa hizi Polisi nao kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, sisi kama JamiiForums tunapinga kwa nguvu namna yoyote ile ya kujaribu kuwanyamazisha waandishi wa habari na vyombo vyao vya habari (si MwanaHalisi pekee) ndani ya nchi yetu. Tunalaani kitendo hiki kwa nguvu zote na kuliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hili ili ukweli ujulikane (ukizingatia kuwa wavamizi walienda kwa lengo la Kubenea na imethibitika).

Tunaamini jeshi letu halitosita kuchukua hatua pindi wahusika watakapobainika na hata kuweza kutoa taarifa juu ya nini walifuata na nani aliwatuma na kwanini.

Invisible, do you really think polisi walikuwa hawajui nini kinaenda kutokea kwa kubenea. Am sure hata Kubenea alipoenda kutoa taarifa walikuwa wanamcheka tu. Na walitekeleza wajibu wao wa kuchukua rekodi lakini nothing is going to happen to them. Cha muhimu Kubene ajitahidi kumuomba Mungu.
 
hii ni kali, nafikir kubenea alionyeshwa kwa sababu hao walikuja kumtoa uhai. lakini siku moja ipo ambapo wote tutakuwa tunafurahia matunda ya uhuru wetu bila hawa mafisadi. vyovyote itakavyokuwa siku zao zimehesabika.
 
ati CCM wanadumisha amani...........bado nakumbuka maneno ya Rais kuwa atawashughulikia watu kimya kimya .
 
Shughuli za kupambana na wale wote wanaonekana wana nia mbaya na CCM zimeanza rasmi. Sijui wangempata ndiyo wangemuua au wangempa adhabu ipi. Inasikitisha sana kwa kweli, hawa jamaa ni lazima ukubaliane nao vinginevyo wanakuweka kwenye kundi la uadui na unaweza kupoteza uhai wako bila sababu za msingi. Bongo tambarare!
 
Uuuuwi Tz Mungiki in action. Yule Ss*aliyeandikwa vizuri/vibaya katika mwanahalisi, sii ni kiranja wa usalama wa viongozi Tz? Kupenea p/se take care.
 
hivi kweli tanzania imefikia hapa......sitaki kuamini.............
 
Back
Top Bottom