Hivi karibuni tumeshuhudia mijadala mbalimbali ya bageti ikiendelea bungeni. kitu cha kushangaza wabunge wengi wameonekana wakiwasahau wapiga kura wao na kujita ktk kutetea maslahi yao. Wabunge wengi wa sisi emu wamekuwa wakitumia wingi wao/nguvu kupinga hoja muhim zenye manufaa kwa taifa na wananchi wa hali ya chini. Hii inaonesha ni jinsi gani watu tuliowachagua si kwa ajili yetu. Katika hali wazi kabisa tazama akina Mnyika, Tundu Lisu,Zitto wanavyopambana. Watz tuamke tupambanue hoja na si ushabiki tu tuangalie maisha yetu tunapelekwa wapi.