Tunakusanya Kero Za Spika, Wabunge, Viongozi Tuwapelekee Wananchi

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,063
2,471
That's right. Baada ya kumsikiliza ndugu Spika Anna Makinda akiongea na watu wa jimbo lake kuwa hana nyumba na itabidi akope ajenge nyumba, nimeona tukusanye kero za viongozi wetu na tuwapelekee wananchi.

Inawezekana ufanisi wao ubovu unatokana na kuwa wanajitolea kwa muda mrefu na mapato yao ni duni kweli kweli.

Kama alivyosema Spika kuwa yeye ni mtu wa dini na haongopi. Kipato chake hakitoshi na itabidi hakope kama watu wengine ili aweze kujijengea kibanda.

Kama wewe ni kiongozi, mbunge, diwani, meya, rais, makamu, naomba utuletee kero zako. Au kama unamjua kiongozi yoyote yule mwenye kero, tunaomba utuletee kero zake. Na sisi kama wananchi tutazifikiria na kuzitafutia ufumbuzi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kutatua Kero za Viongozi,

Z-10
 
hivi kumbe watu wanagombea ubunge ili kukuza kipato? Sio kuwakilisha,kutetea wananchi na hatimae kutunga sheria na kuisimamia serikali utekelezaji?
kumbe ni high collar job za kumuwezesha mbunge kujenga?..kutoa misaada?... Kumbe ni daraja ya uwaziri na ukiikosa unatamani kujiuzulu??
Shame on she and the rest followers
 
Huyo mama nae mwongo, umri umekwenda na changamoto za uongozi wa sasa haziwezi ndiyo maana anataka kuachia ngazi. Tangu ujana wake anagombea ubunge, angeona hiyo kazi hailipi si angeacha miaka mingi huko nyuma?

Kero:
Makinda na Wabunge wa CCM - Posho hazitoshi
Rais - Mashinikizo kutoka kwa watu mbalimbali na safari za nje ni chache sana
Waziri wa Sheria na Katiba na AG - Mnawalazimisha kufuatilia uanzishaji wa katiba mpya
 
Back
Top Bottom