Tunakupongeza Askofu Shao kwa uzalendo wako, Padri Mapunda, Dr Slaa kuweni na huruma

Wewe Ritz hivi unajua unachokiongea??? unampeleka mgonjwa muhimbili kipimo cha CT scan anakipata wapi? dawa na vitendea kazi vya theatre na wardini anatoa wapi ?

Harafu akija call mnampa 20,000/= kwanini na yeye hasiende bungeni akale 330,000/= kwa siku tena kwa kukaa tu? mnadhani kuna mtu anapenda shida? maDr. wanawatumikia wananchi kwenye mazingira magumu sana tena kuliko wabunge, leo tanzania mwanasiasa anampangia Dr., Eng, watu proffessional walipwe shs ngapi. tutafika kweli?

bungeni kuna maDr, Eng, maprof wangapi ambao wameacha kufundisha hili nchi iwe na maendeleo wameenda kukaa bungeni. fukuza wote mole waje huku ndio tutaongea lugha moja.

Mkuu kama unaona ubunge unalipa bora utafute jimbo la uchaguzi ukagombee! Fani ya ya udaktari huwezi kuifanyia 'calculation of profit bases' kama wafanyakazi wa viwandani, sasa unapogoma wanaopata matatizo sio serikali ni Watanzania wasio na hatia, wanaendelea kufa wajawazito, vikongwe, watoto wa walala hoi, kwani hao ndio wamekataa kuboresha malahi yenu? Kwa nini basi wahukumie wao?
 
Kinapashwa kuogopwa katika mfano huu wa mgomo kwa wale wasioitakia mema nchi yetu kina Dr Slaa na Padri Mapunda, wanataka migomo indelee kwenye sekta zote za serikili ili mipango yao ifanikiwe nchi isitawalike.
 
Kurudi kwa madaktari kazini bila ya maelewano ya kweli na muajiri wake ni kazi bure. Sikuzote mtu hafanyikazi kwa lazima, ukimlazimisha akafanya kazi kwa woga, basi hiyo kazi haitakuwa naufanisi. Utapata mgomo baridi ambao ni mbaya zaidi. Angalia sekta nyingine kama Ualimu, Kilimo,Maji, Mahakama n.k hawagomi moja kwa moja huduma zake zikoje!

Hakuna anayepinga kuwa madaktari ni watu muhimu duniani, lakini umuhimu huo usichukuliwe vibaya na wachache, unaweza kuleta matatizo kama haya tunayoshuhudia sasa...kila idara wana umuhimu Majeshi yetu ya Ulinzi na Usalama, Walimu, Madereva, Manaodha wa meli, Marubani wa ndege, na wafanyakazi wengine wa serikali.
 
Kwenye ukweli uongo hujitenga,
Nakuunga mkono mkuu.

Kama sijakosea ndio wale viongozi wa dini waliofanya maombi
kwa ajili ya afya ya Dr. Ulimboka.

Wanabodi.

Kwa Watanzania wanaotakia mema nchi yetu wanampongeza Askofu wa Kanisa la (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Dr Martin Shao, kwa uzalendo wake alipowasihi madaktari waliogoma katika hospitali mbali mbali nchini ikiwemo hospitali ya KCMC kureja kazini huku wakiendelea na madai yao serikalini.

Wananchi wengi wamefedheheswa na kauli za Padri Babtiste Mapunda na Dr Slaa, kuunga mkono mgomo wa madaktari...Padri na Dr Slaa, waelezeni Watanzania kwa maoni yenu mgomo unamkomoa nani? Na kumuumiza nani? Je ni kweli migomo ya aina hii inawafikia walengwa na kuwaonjesha maumivu yatokanayo na mgomo?

Dr Slaa, tembelea muhimbili na kakae pale mapokezi walau kwa saa mbili tu ili uone mwenyewe wagonjwa wanavyoteseka na wengine wanavyokufa kwa kukosa huduma halafu uwaambie Watanzania mgomo uendelee hadi lini ama ujirudie mara ngapi ili kuwashikisha adabu hao unaodhani ndio wakosaji na wasiotaka kutoa stahiki ya madaktari..

Tunashindwa kuamini Dr Slaa na Padri Mapunda, wameshindwa kuwahurumia Watanzania wanaoteseka na huku wengine wakifa baada ya kukosa huduma ya kitabibu, miongoni wanaougua ni wanachama wa Chadema sasa watu hao wakifa si anapoteza wananchama.
 
Nasikia mke/demu wako wa UDOM anapenda kuliwa 0713 sana !
Mpungati; hapa ni pahali pa wastaarabu. Nmenisikita kuona kauli kama hii kutoka kinywani mwa The Great Thinkers! Ritz Mkuu; taarifa zilizopo ni kuwa mgomo umekwisha na hali ya huduma inaendelea vyema, kwa hivyo kwa nini bado tunaendeleza longolongo kwa kitu kisichokuwepo?
Taarifa ya Afisa Uhusiano wa hospitali ya Muhimbili kuhusu hali ya huduma ilivyo leo

03/07/2012

Taarifa niliyopata kutoka kwenye Kurugenzi ya Tiba, Kurugenzi ya Upasuaji, Kurugenzi ya Tiba Shirikishi na Kurugenzi ya Uuguzi ni kama ifuatavyo;

Kurugenzi ya Tiba: Huduma zimeendelea kutolewa kwa kiwango cha kati wagonjwa ni wachache wanaokuja kutibiwa.

Idara ya Tiba, Madaktari Bingwa wote na Registrar wote wamefika kazini na wanafanya kazi. Interns 11 wamefanya kazi. Major ward round zimefanyika. Kliniki zote za leo zimeendelea kufanya kazi pia cliniki za mchana zitafanyika.

Idara ya watoto, Madaktari Bingwa wote wapo na wanafanya kazi wapo wadini wanaona wagonjwa. Changamoto ni kwamba inabidi pia wafanye kliniki za wagonjwa wa nje na wanajitahidi kufanya hivyo.

Idara ya magonjwa ya nje.
Registrars na Daktari Bingwa wote wapo na wanafanya kazi.

Idara ya magonjwa ya afya ya akili
, Madaktari Bingwa wote wamefika kazini . Bada ya wagonjwa wote kupelekwa wodini, walionwa na madaktari. Wagonjwa katika kitengo hiki ni wengi ukilinganisha na idadi ya madaktari bingwa, lakini kliniki zimeendelea kufanyika kwa kiwango cha kati. Kiliniki ya wagonjwa wajidunga imefanyika.

Idara ya magonjwa ya dharura
, Registrar wote wamesaini lakini wliofanya kazi ni wawili tu. Daktari Bingwa yupo na anafanya kazi.

Idara ya mazoezi ya viungo
, Wafanyakazi wote wapo na wanafanya kazi.

Kurugenzi ya Upasuaji:
Huduma za upasuaji zinafanyika lakini siyo sawa na jinsi zilivyokuwa zinafanyika kabla yamgomo kwani wagonjwa ni wachache kwenye baadhi ya kliniki na baadhi ya kliniki wagonjwa wanakuwa wengi. Wagonjwa wa upasuaji walioko wodini wanaonwa japo ni wachache ukilinganisha na hali ilivyokuwa. Baadhi ya huduma za upasuaji (operations) zimefanyika ingawa wagonjwa ni wachache kwa vile idadi ya wagonjwa wanaokuja kliniki au waliolazwa kwa ajili ya upasuaji ni wachache.

Huduma za Tiba Shirikishi: Vipimo vya maabara na vile vya uchunguzi wa radiolojia vinaendelea kufanyika kama kawaida ingawa idadi ya vipimo vimepungua ukilinganisha na kabla ya mgomo. Idara ya famasia pia inafanya kazi kama kawaida. Idadi ya wagonjwa wanaoandikiwa dawa ilipungua ukilinganisha na kabla ya mgomo.

Kurugenzi ya Uuguzi
Huduma za uuguzi zimeendelea kutolewa kwa kiwango cha kawaida.

Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha

Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 3, 2012
 
Last edited by a moderator:
Wale wote waliounga mkono mgomo wa madaktari ni punguwani wa akili vipi binaadam mwenzako anateseka kitandani au anakufa wewe unafurahia ati tu kwa sababu za kisiasa ionekane serekali haijali watu wake huo ni ujinga wa kutojitambua na mwisho wa ubaya aibu
 
padri slaa mzee wa kushadadia mambo yule ili apate covarage kwenye magazeti

Dr Slaa anahitaji coverage gani tena kwenye magazeti wakati anajulikana Tz nzima mpaka nje ya nchi? Kote anakofahamika bosi wake JK na Dr Slaa pia anafahamika- hahitaji magazeti yamtangaze upya. Ok!
 
Ritz;
Padri Shayo ni mtumishi wa Mungu; kila ilivyo mtu wa Mungu hangependa kuwaona watu wakiteseka; Dr. Slaa kazi Mungu ilimshinda zamani yale yaliyokatazwa na Mungu yeye ndiyo aliyapa kipau mbele; ikiwa kama swala dogo tu la kuoa lilimshinda atawaonea huruma watu asiowajua? Huyu Padri Mapunda ni mganga njaa anayetumia jina Mungu kuendesha maisha yake; Dr. Slaa na Mapunda wasikuumize kichwa hata kidogo ni wanafiki tu.

Chama
Gongo la mboto DSM[/QUOTE

Kwani uongozi wa Dr Slaa unahusiano gani na Ndoa yake. Mbona Mandela ana mke wa tatu sasa hivi na wa SA na dunia nzima inamheshimu sana kuliko mtu mwingine ye yote? Kama Josephine Mshumbuzi na yeye wameridhika kukaa pamoja wewe kinakuumaje mkuu?
 
Nasikia mke/demu wako wa UDOM anapenda kuliwa 0713 sana!

HIVI UMEONA HUNA SEHEMU YOYOTE YA KUTOA UPUUZI KAMA HUO MPAKA UJE UUTOE HAPA JF?HAPA NI SEHEMU YA KUELIMISHANA NA KUTOA MADA ZENYE KUELIMISHA KATOE MATUSI HUKO MTAANI KWENU ULIPOZOEA.
 
wewe ni kama chizi aliyetoroka milembe na mavazi ya hospitali, hujui a wala B, hivi nani ana huruma kati ya madaktari na serikali? hili vuguvugu limeanza lini? watu wamekufa wangapi kutokana na hali mbaya ya hospitali? SERIKALI INAKJALI NINI IWAPO INATENGA SHS BILION 8 KWA AJILI YA MAWAZIRI NA MARAIS WASTAAFU HALI SERIKALI TANO ZA RUFAA ZINATENGEWA SHS BILION 6? NANI ANA HURUMA?wangapi wanaambukizwa na magonjwa yasiyo yao kisa vifaa haba? nani anajali serikali au madaktari? uwe unaongea vitu unavyovjua na si kukurupka¬

95% Maslahi binafsi 5%Maslahi ya Wagonjwa.
 
Watu kama Dr Slaa, walitakiwa kuonyesha uzalendo wake kuwasihi madakatari kusitisha mgomo wao wakati maongezi na serikali jinsi ya kuboresha maslahi yao , kinyume chake Dr Slaa anaunga mkono mgomo na kuchochea eti serikali inashindwa kuwalipa madaktari huku inatenga bilioni 15 kwa chai tu..

Inashangaza Slaa analeta ushabiki wa kisiasa wakati athari za mgomo huu ni kubwa watu wanazidi kupoteza maisha..sina maana kwamba naunga mkono mishahara ya wataalamu kuwa midogo, hapana ninachotaka kusema ni kuwa hakuna haki isiyokuwa na wajibu, Madaktari wawajibike kwanza kutibu watu kisha wadai hicho wanachokiita haki yao.

Dr Slaa hakuna asiyefahamu kuwa Madaktari na wasaidizi wao ni kati ya watumishi wa umma wachache wanaolipwa vizuri zaidi ya wengine.
 
madaktari warudi na wasirudi miundombinu kwa maana ya vifaa teknolojia na madawa ni tatizo hispitalini kiasi kwamba huduma hakuna.Mngechunguza kuona kwamba Maaskofu kwa ujumla na Dr Martin SHAO wanatibiwa wapi?ni yale yale ya viongozi wa nchi hizi,wanahubiri MAJI wanakunywa WINE!
 
Wanabodi.

Kwa Watanzania wanaotakia mema nchi yetu wanampongeza Askofu wa Kanisa la (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Dr Martin Shao, kwa uzalendo wake alipowasihi madaktari waliogoma katika hospitali mbali mbali nchini ikiwemo hospitali ya KCMC kureja kazini huku wakiendelea na madai yao serikalini.

Wananchi wengi wamefedheheswa na kauli za Padri Babtiste Mapunda na Dr Slaa, kuunga mkono mgomo wa madaktari...Padri na Dr Slaa, waelezeni Watanzania kwa maoni yenu mgomo unamkomoa nani? Na kumuumiza nani? Je ni kweli migomo ya aina hii inawafikia walengwa na kuwaonjesha maumivu yatokanayo na mgomo?

Dr Slaa, tembelea muhimbili na kakae pale mapokezi walau kwa saa mbili tu ili uone mwenyewe wagonjwa wanavyoteseka na wengine wanavyokufa kwa kukosa huduma halafu uwaambie Watanzania mgomo uendelee hadi lini ama ujirudie mara ngapi ili kuwashikisha adabu hao unaodhani ndio wakosaji na wasiotaka kutoa stahiki ya madaktari..

Tunashindwa kuamini Dr Slaa na Padri Mapunda, wameshindwa kuwahurumia Watanzania wanaoteseka na huku wengine wakifa baada ya kukosa huduma ya kitabibu, miongoni wanaougua ni wanachama wa Chadema sasa watu hao wakifa si anapoteza wananchama.

Muulize baba Mwanasha easily kuwa ambavyo hataki kutafuta suluhu na Madktari ni kwa faida ya nani?
 
Ritz;
Padri Shayo ni mtumishi wa Mungu; kila ilivyo mtu wa Mungu hangependa kuwaona watu wakiteseka; Dr. Slaa kazi Mungu ilimshinda zamani yale yaliyokatazwa na Mungu yeye ndiyo aliyapa kipau mbele; ikiwa kama swala dogo tu la kuoa lilimshinda atawaonea huruma watu asiowajua? Huyu Padri Mapunda ni mganga njaa anayetumia jina Mungu kuendesha maisha yake; Dr. Slaa na Mapunda wasikuumize kichwa hata kidogo ni wanafiki tu.

Chama
Gongo la mboto DSM[/QUOTE

Kwani uongozi wa Dr Slaa unahusiano gani na Ndoa yake. Mbona Mandela ana mke wa tatu sasa hivi na wa SA na dunia nzima inamheshimu sana kuliko mtu mwingine ye yote? Kama Josephine Mshumbuzi na yeye wameridhika kukaa pamoja wewe kinakuumaje mkuu?

Aweda;
Hapa unaongelea mke au kimada? Dr. Slaa anaishi na kimada na kumbuka Mzee Mandela hajawahi kuasi kazi ya Mungu ya upadri na kuingilia anasa za dunia; ngono ndiyo iliyomtoa kanisani Dr. Slaa; credibility yake Dr. Slaa ni 0
Siku nyingine usifananishe mwanapinduzi wa kweli ambaye aliyatoa maisha yake mhanga kutetea wanyonge na kituko kama Dr. Slaa ni matusi makubwa sana

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Back
Top Bottom