Tunakosea wapi katika kutafuta kazi

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
Watanzania tuna changamoto tunapaanza maisha ya kutaffuta ajira au kubadilisha ajira. Changamoto inatokana na uhaba wa ajira chache zilizopo. Ukiondoa matatizo ya mifumo, na taratibu za uajiri kwenye taasisi nyingi wengi wetu pia tuna matatizo. na wengine tsisi wenyewe tumekuwa ni kikwazo chetu wenyewe. Matatizo haya nitayataja kwa mtazamo wangu

  1. NJIA TUNAZOTUMIA KUTAFUTA AJIRA
VIjana wengi na zaidi hasa wa kike sio wasomaji wazuri wa magazeti.Na mara nyingi wanatumia informal way za kutafuta ajira. iformal way ni kama ofisi haijatangaza kazi lakini muombaji kazi anapeleka barua. style hii sio nzuri sana inaweza kukukatisha tamaa mapema sabbau utaaply ofisi kumi ambazo hazijatangaza kazi bahati mbaya wote wakijibu aksante hatuna nafasi wazi utajiona umefanya maombi 10 bila kufanikiwa.

NJIA nyingine amabyo sio nzuri kabisa ni kutegema baba, mjomba mama, mwanakijiji kwa kutiumia nafasi aliyonayo akusaidie kupata kazi fulani. Njia hii sio nzuri sababu itataua tatizo moja la kazi lakini unaweza usiwe huru kufanya kazi yako kisomi na kimaadili . Unaweza kudharaulika na wafanyakazi wenzako ikjulikana umepata kazi kwa njia za kona kona.Leo ii tunaona wafanyakazi wa BOT wengi wamesoma lakini labda kwa sbabu ya njia walizoapta kazi Image yao????? Anyway wengine wanasema bora pesa imeingia mfukoni

2.MATARAJIO NA AINA YA KAZI TUNAZOTAFUTA

a)Kila mtu ana ndoto ya kuwa na maisha mazuri na hili linachangia baadhi ya watu kuwa na ubaguzi na aina fulani ya kazi. SIo vizuri kwa kijana asiyekuwa na kazi kuwa selective sana. Mfano Serikali inatangaza kazi wahasibu daraja la kwanza Mshahara 210,000. Kijana atajiuliza ivi kweli nitaishi kwa mwezi kwa 210,000. Anajiuliza swali lingine hivi kwa mshahara huu itanichukua miaka mingapi kuwa na kagari kangu wachilia mbali nyumba? Unasahu kuwa kuna watu ofisi iliyotangaza kazi wana watoto wanawasomesha wamepanga ,nyumba wanakwenda kazini na kuridi kila siku na wanakula na kulala.
kwa hiyo watu wajue sio mara zote kiasi kinachotangazwa ndio net pay hasa kwa serikali. kutoaaply kazi kama hhizi unakuwa umejitoa kwenye short list mwenyewe

b) Kuna wengine sababu amesoma degree ya uhasibu anaona hawezi ku apply kazi iliyonadikwa cashier. au sababu ana Bsc ya Engineering hawezi ku apply kazi yenye title ya Techcnician

3. CV AND WRITING SKILLS

Katika maswali ya msingi kujiuliza ni ni kwa kiasi gani CV yako inakuuzakatika kazi fulani. NI kosa kutumia CV na barua ya maombi style ilele kwenye maombi ya kazi tofauti na kampuni tofauti. CUstmize barua na CV yako iendane na kazi iliyotanganzwa na iendane na dhima/ Mission/Vission ya taasisi husika. I mean ni vizuri kubadilisha achivemenet zako, sucesss zako,career history yako na Referee wako na apspect nyingine maelezo yake yafanane fanane na theme ya tasisi fulani ?

Ni hivi kama wewe ni mtoto wa mkulima usiandike CV ambayo ni kama na mtoto wa kibosile fulani( ie ana uhakika) . Kama unapigwa fimbo kwa kuwa huna contact wachape fimbo kwenye kuwa makini kwenye maelezo yako. Jiuze. I dont mean CV iwe na page 6 au barua ya maombi iwe na page 3. google ina majibu na mifano

4. KUJITAYARISHA KWA INTERVIEW /USAILI WA KAZI

Hata kama ni kichwa vipi ni vizuri kujiyaraisha kwa usaili.kujaribu kupata ABC za tasisi husika. Kusoma maswali ya msingi wanayouliza kwenye usaili na kujua wasaili wanategmea jibu gani . Unless unategema u godfather then matayarisho ni muhimu. Ukitumia intenet unaweza kujua maswali common yanayolizwa ingawa wording na syntax inabadilishwa maswali ni yale yale.

Mfano wa swali. Kwa nini tukuajiri wewe na si wengine?
hapa huwezi kuapyta jibu la swali wanalotegema wasaili kwenye mdaftari yako ya chuo. Jibu sahi laweza kuwa Uko Flexible, uwezo wa kujifunza kutoka kwa wenzako haraka, uko social, good team player. ( Dependning na aina ya kazi uliyoomba)

Ni kosa kusema una ozoefu wa kazi miaka mingi. sababu ujui washindani wako wana expernce gani au NI kosa kusema Unajua Programming kama ilikuwa ni requirement ya tangazo la kazi basi kila mshindani anajua kama wewe unajua.

Kwa ni jambo la msingi ku gugo neno kama prepataion for interview utapata nondo nzuri tu na interview yako itakuwa kama kumsukuma mlevi.

usiwape sababu nzuri za wao kusindwa kukuchangua

5. KUTOKUWA NA kUTOTAFUTA TAARIFA

Ingawa binafsi ni mtumiji mzuri wa mtanda laki siwei kubisha sina well infomed news kuhusu ajira za fani yangu. kuna watu wanajitaidi kutoa na kutangza nafasi hapa jf lakini sijui kama nasi tunajitahidi kuwafikishi walengwa wasikuwa na mitandao. Magazeti na kuna mtandao maalum ya kazi. tusaidiae kufahamishana

Kuna kazi za UN na taasisi zake za kujitolea/vlunterring ambazo ingawa malipo ni madogo kwa standard ya maisha yetu si haba. wale wenye dream za kufanya Internationa organisatin mnaweza ku gugo na kujisali kweny mashirak mbali mbali.

Nawasilisha kwa mjadala
 
Lay out your human resource recruiting credentials before advising on the foregoing subject.
 
Lay out your human resource recruiting credentials before advising on the foregoing subject.

Am not sure I got u right brother . I ve written this from my experince. am not A huma reource personnel but Iam a human resource. Iam an Accountant.

Do u think wote wanaaandika th read kwenye forum ya SIASA wana political credentials???Does someone need kuwa na taaluma ya sheria kuongelea au kutoa maoni yake kuhusu sheria fulani ? Je wabunge wote ni wanasheria.?

1. Baada ya kumaliza ka kozi fulani katika chuo kachuo fulani nakumbuka niliona tangazo kwenye gazeti then nikawashtua washikaji wakike na kiume . Cha kushangaza most wasichana walikuwa hawana taarifa kabisa. At least vijana wenzangu wa kiume kidogo wachache walikuwa tayari informed. Lakini hata hao vijana baadhi yao walibaki wanahoji hivi TGS D ni shilingi ngapi. Hivi kweli 210,000 inatosha kwa mwezi . Sasa fikiria mtu kamaliza chuo anatafuta kazi anauliza hivyo na bado anaona hiyo ofisi iliyotangza ina watu wanakwenda kazini kila siku. - This is an observation

2. Ukija issue nyingine wala haiitaji uwe Human resouce kwa nini unadhani tuna wasi wasi na wakenya au waganda kucukua kazi zetu. Sio kwa sababu hatuna uwezo ni kwa sababu wengi wetu hatuna taaluma ila ni wazi tunasindwa kwenye presentation na writing skills za ku kuwa convice wasahili we are right.Utatutmi nyezo gani kumwelza msaili asiyekujua uwezo wako. Ni lugha utayochagua maneno utayitumia na style utakaytumia ndo itakuuza. Unaweza kuwa na A++ zote kwenye cheti but if u lack njia sahihi za kujieleza ina maana huwezi kufanya hata interaction na communication vizuri na watu. Communication si a critical aspect of any job.

U dont have to be a human reource profession or personnel kujua haya. After all kama umesoma somo la Management hizi issue ni wazi kabisa

Other wise nashukuru kuonyesha duku duku lako juu ya maoni yangu. So waht do u think is obstacle inayochangia waajiriwa wategemwa wapate shida kupata kazi. Ukiondoa matatizo ya waajiri.?
 
Lay out your human resource recruiting credentials before advising on the foregoing subject.

Free advise... Your comment is very aggressive and depicts you static thinking... in today's world knowledge/education should help you to THINK!!! You need to change.
 
Watanzania tuna changamoto tunapaanza maisha ya kutaffuta ajira au kubadilisha ajira. Changamoto inatokana na uhaba wa ajira chache zilizopo. Ukiondoa matatizo ya mifumo, na taratibu za uajiri kwenye taasisi nyingi wengi wetu pia tuna matatizo. na wengine tsisi wenyewe tumekuwa ni kikwazo chetu wenyewe. Matatizo haya nitayataja kwa mtazamo wangu

  1. NJIA TUNAZOTUMIA KUTAFUTA AJIRA
VIjana wengi na zaidi hasa wa kike sio wasomaji wazuri wa magazeti.Na mara nyingi wanatumia informal way za kutafuta ajira. iformal way ni kama ofisi haijatangaza kazi lakini muombaji kazi anapeleka barua. style hii sio nzuri sana inaweza kukukatisha tamaa mapema sabbau utaaply ofisi kumi ambazo hazijatangaza kazi bahati mbaya wote wakijibu aksante hatuna nafasi wazi utajiona umefanya maombi 10 bila kufanikiwa.

NJIA nyingine amabyo sio nzuri kabisa ni kutegema baba, mjomba mama, mwanakijiji kwa kutiumia nafasi aliyonayo akusaidie kupata kazi fulani. Njia hii sio nzuri sababu itataua tatizo moja la kazi lakini unaweza usiwe huru kufanya kazi yako kisomi na kimaadili . Unaweza kudharaulika na wafanyakazi wenzako ikjulikana umepata kazi kwa njia za kona kona.Leo ii tunaona wafanyakazi wa BOT wengi wamesoma lakini labda kwa sbabu ya njia walizoapta kazi Image yao????? Anyway wengine wanasema bora pesa imeingia mfukoni

2.MATARAJIO NA AINA YA KAZI TUNAZOTAFUTA

a)Kila mtu ana ndoto ya kuwa na maisha mazuri na hili linachangia baadhi ya watu kuwa na ubaguzi na aina fulani ya kazi. SIo vizuri kwa kijana asiyekuwa na kazi kuwa selective sana. Mfano Serikali inatangaza kazi wahasibu daraja la kwanza Mshahara 210,000. Kijana atajiuliza ivi kweli nitaishi kwa mwezi kwa 210,000. Anajiuliza swali lingine hivi kwa mshahara huu itanichukua miaka mingapi kuwa na kagari kangu wachilia mbali nyumba? Unasahu kuwa kuna watu ofisi iliyotangaza kazi wana watoto wanawasomesha wamepanga ,nyumba wanakwenda kazini na kuridi kila siku na wanakula na kulala.
kwa hiyo watu wajue sio mara zote kiasi kinachotangazwa ndio net pay hasa kwa serikali. kutoaaply kazi kama hhizi unakuwa umejitoa kwenye short list mwenyewe

b) Kuna wengine sababu amesoma degree ya uhasibu anaona hawezi ku apply kazi iliyonadikwa cashier. au sababu ana Bsc ya Engineering hawezi ku apply kazi yenye title ya Techcnician

3. CV AND WRITING SKILLS

Katika maswali ya msingi kujiuliza ni ni kwa kiasi gani CV yako inakuuzakatika kazi fulani. NI kosa kutumia CV na barua ya maombi style ilele kwenye maombi ya kazi tofauti na kampuni tofauti. CUstmize barua na CV yako iendane na kazi iliyotanganzwa na iendane na dhima/ Mission/Vission ya taasisi husika. I mean ni vizuri kubadilisha achivemenet zako, sucesss zako,career history yako na Referee wako na apspect nyingine maelezo yake yafanane fanane na theme ya tasisi fulani ?
Ni hivi kama wewe ni mtoto wa mkulima usiandike CV ambayo ni kama na mtoto wa kibosile fulani( ie ana uhakika) . Kama unapigwa fimbo kwa kuwa huna contact wachape fimbo kwenye kuwa makini kwenye maelezo yako. Jiuze. I dont mean CV iwe na page 6 au barua ya maombi iwe na page 3. google ina majibu na mifano

4. KUJITAYARISHA KWA INTERVIEW /USAILI WA KAZI

Hata kama ni kichwa vipi ni vizuri kujiyaraisha kwa usaili.kujaribu kupata ABC za tasisi husika. Kusoma maswali ya msingi wanayouliza kwenye usaili na kujua wasaili wanategmea jibu gani . Unless unategema u godfather then matayarisho ni muhimu. Ukitumia intenet unaweza kujua maswali common yanayolizwa ingawa wording na syntax inabadilishwa maswali ni yale yale.

Mfano wa swali. Kwa nini tukuajiri wewe na si wengine?
hapa huwezi kuapyta jibu la swali wanalotegema wasaili kwenye mdaftari yako ya chuo. Jibu sahi laweza kuwa Uko Flexible, uwezo wa kujifunza kutoka kwa wenzako haraka, uko social, good team player. ( Dependning na aina ya kazi uliyoomba)

Ni kosa kusema una ozoefu wa kazi miaka mingi. sababu ujui washindani wako wana expernce gani au NI kosa kusema Unajua Programming kama ilikuwa ni requirement ya tangazo la kazi basi kila mshindani anajua kama wewe unajua.

Kwa ni jambo la msingi ku gugo neno kama prepataion for interview utapata nondo nzuri tu na interview yako itakuwa kama kumsukuma mlevi.

usiwape sababu nzuri za wao kusindwa kukuchangua

5. KUTOKUWA NA kUTOTAFUTA TAARIFA

Ingawa binafsi ni mtumiji mzuri wa mtanda laki siwei kubisha sina well infomed news kuhusu ajira za fani yangu. kuna watu wanajitaidi kutoa na kutangza nafasi hapa jf lakini sijui kama nasi tunajitahidi kuwafikishi walengwa wasikuwa na mitandao. Magazeti na kuna mtandao maalum ya kazi. tusaidiae kufahamishana

Kuna kazi za UN na taasisi zake za kujitolea/vlunterring ambazo ingawa malipo ni madogo kwa standard ya maisha yetu si haba. wale wenye dream za kufanya Internationa organisatin mnaweza ku gugo na kujisali kweny mashirak mbali mbali.

Nawasilisha kwa mjadala

Ongezo 1: Himiza washikaji kutumia mitandao na njia zingine za mawasiliano... Binafsi nikiona tangazo la ajira popote huwa nalitawanya kwa kila ninayehisi anatafuta ajira na inaishia hapo. Bahati nzuri kuna huduma ya matangazo ta kazi kwa kupitia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi.. kama sijakosea wanatoza Tshs 150. unajisajili...unapewa huduma,ukijisikia huhitaji tena.. unajitoa.

Ongezo 2:Unapopata nafasi ya Usaili... Una kazi kwa asilimia 50.. ukiachilia waajiri amabao wengi wanaandika maswali yatakayoulizwa ktk usaili... mashirika ya kimataifa huwa yanatoa maswali kulingana na maelezo ya CV yako...kuwa MKWELI ktk CV...vinginevyo UTAUMBUKA..!kitu hujui.. kubali hujui ila waweza ukajifunza.JIAMINI..kukosea kujibu swali haimaanishi umekosa kazi... hata waajiri wenyewe hawatarajii mfanyakazi mtarajiwa kukidhi asilimia 100 ya mahitaji ya kazi. Wanaangalia viashiria(potentials) ambazo zitakusaidia kufanya kazi uliyoomba!!

Kwa sasa ni hayo..Nakubali kusahihishwa!!!!
 
Free advise... Your comment is very aggressive and depicts you static thinking... in today's world knowledge/education should help you to THINK!!! You need to change.

Thank you kwa kuona hii

Hii inaonyesha hulka na tabia nyingine ya viongozi tulionao. Kwa kuwa wana elimu na ni wasomi wa elimu ya juu wanadhani hawawezi kupokea ushauri mzuri kwa watu walio chini yao. Akili yao inawaambia huyu naye elimu yake ndogo atanipaje ushauri au atawezaje kuotoa wazo ambalo ndio suluhisho sahihi zaidi.

Bosi anauliza subornidate wake hili hii ulifundishwa wapi?

Kumbe watu walio chini ndio wako front end wanakutana na wateja. So sometime sio vizuri ku under value views za mtu just bcs uselfish wako unakufanya uamini kuwa hawezi kuwa na mchango wa maana.
 
Hatufanyi yafuatayo: 1. hatusomi tangazo la kazi kwa makini - dhumuni la kazi/ au nafasi ya kazi, majukumu yake, ujuzi (skills), kiwango cha elimu; 2. kwenye usaili maswali yote utoka kwenye majukumu ya kazi, knowledge na skills, nasi hatuzingatii hilo - maandalizi hafifu; 3. tunasahau kwamba usaili unaanza wakati unapoandika barua yako ya maombi ya kazi - kwani kwa kutumia barua yako ndipo shortlisting ufanyika - poor Englishi/ Kiswahili, not comprehensive, not concise and precise (in short poor self expression) na haya yote ni matunda mabovu ya darasani - kusoma ili kufauli lakini sio kukabili mazingira baada ya shule.
 
Tatizo kubwa katika sekta ya ajira, tunafanya kazi kwa mazoea na si kwa ushindani... mwajiri hatengenezi mazingira ya ushindani na mwajiriwa anafanya kazi kwa ajili ya mshahara... watafuta kazi wengi wanapenda aijra za umma kwa vile ataweza toroka na kufanya mambo mengine...ANAIBA MUDA WA KAZI KUFANYA MAMBO BINAFSI.. na wisho wa mwezi anakinga mkono alipwe mshahara... TUNAJILEMAZA wenyewe..

Ajira za serikali zingekuwa za mikataba ya muda wa miaka 2 hadi mitatu na baada ya hapo mwajiriwa atathminiwe kabla ya kupewa makataba mwingine wa ajira!..wantu wangeamka..

Nakubali kusahihishwa!!!!
Dunia hii tuliyomo... ubora wa utendaji wako unapimwa kwa mafanikio yako. Haijalishi una majukumu makubwa au madogo kiasi gani!!
 
Nimekungea Thanks kuonyesha nakubaliana na wewe hasa vipengele vilivyofuata badala ya kipengele cha kwanza, kile kwangu naona sikubaliani na wewe kwani zipo kabisa namna za uandishi wa barua za kuulizia kama kuna kazi kwani kunakazi nyingine huwa hazitangazwi nje ( Yaani nje ya kamouni/organization) hivyo ni namna njema ya kuweza kupata hiyo kazi, mfano UDSM juzi wametangaza nafazi za kazi kibao kwa mara ya pili ambazo hazipo kwenye magazeti.

Labda tuseme wanakosea kuandika hizo barau za kuuilizia kazi, wanasahau kuuza CV badala yake wanauza Sura zao..
By The Way

MUNGU akubariki sana kwa thread nzuri, Sema AMEN
 
Ndugu umefanya vema uwashauri wanaosaka kazi au fursa japo wapo wanaokubeza pia. Usijali maana penye wengi hapakosi mengi.
Naomba niongezee kidogo nilicho nacho.
1. Kutafuta ajira/fursa ni mchakato - mtu usiridhike na skill moja tu .Jaribu kuwa multi-skilled wakati wote kwa kujiendeleza kielemu na kujitolea ( volunteerims ili upate uzoefu.
2. Kabili soko la ajira na akili iliyo wazi ( open-minded) usitafute tu kufanya kazi unadhani akuwa ndio inayokufaa kwa vile taaluma yako ndivyo inavyokuambia. Ukiwa mwanasheria kwa mfano usijione ukiwa kwenye nafasi hiyo tu.Fikiria kufanya kazi kwenye NGOs nk.
3. Jiandae siyo tu kujibu maswali bali hata muonekano wako. Vaa nguo safi zinazofaa for the occassion.Kama ni mwanamke vaa mavaz ya heshima yanayokupendeza lakini yasiwe ya kutishia sana! Usipake manukato makali sana! Wenye kunuka vikwapa - hakikisha unaoga vema - chukua muda wa kutosha bafuni jisugue barabara na usijirashie maji na kutimka.

4.Jipe muda wa kutosha kufika aneo la usaili. Kama hupajui kwa uhakika, hakikisha a day before unafanya utafiti kujua ni wapi. Wahi, usichelewe ikiwezekana fika muda kabla ya saa ya usaili.Kuna jamaa alikurupuka amevaa suti yake.Anafika eneo kaloa jasho chepechepe.Akakaribishwa chumba cha kusubiria - kilikuwa na sofa very comfortable na air condition.Jamaa alichukuliwa na usingizi.By the time anakurupuka time yake ilishapita.Walichofanya ni kumshukuru tu kwa kufika. Hapo alijiondosha kwenye kinyang'anyiro kwa kuoenyesha how irresponsible he is!
 
Nakubaliana na wewe kabisa katika ongezeko lako la 2.Wiki iliyopita niliitwa somewhere kwa interview na wazungu fulani,waliokuwa wananihoji walikuwepo wazungu 3 na Mtanzania 1,interview ilikuwa nzuri sana niliifurahia kwa kweli,sikuweza kujibu maswali yote lakini jamaa wanakuuliza mulemule kama mdau ulivyosema hapo kwenye ongezeko.

Sijui idadi ya walioitwa lakini nilitoka na matumaini-70%.So nilijifunza vitu kadhaa;
1.Andika barua na cv kulingana na kilichotangazwa,imenisaidia sana hiyo kwani majibu ya maswali mengi nilisha yajibu kwenye barua na CV
2.Jiandae,hiyo ngoma niliipigia msuli wiki nzima kana kwamba ni paper ya mwisho
3.Usiseme uongo.Waliniuliza maswali mengi kutoka kwenye cv yangu,niliwajibu bila kubabaika,nadhani kwa sababu sikudanganya.

So,ni kwelin tunatakiwa kuwa serious wakati tunaomba na wakati hatujaenda kwenye interview.
 
Back
Top Bottom