Tunajifunza nini Kushindwa kwa Brig Gen (Lit) Ngwilizi ujumbe wa NEC?

Fitinamwiko

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
4,803
1,416
Baada ya tuhuma za Rushwa dhidi ya wabunge wa Bunge la 10, Spika aliunda tume ya maadili chini ya General Ngwilizi kuchunguza tuhuma hizo. Kuna tetesi, report imekamilika, hata halmashauri kuu ya CCM ilitumia kuwakata baadhi ya wagombea. Tumeona wabunge wapambanaji na wapinga Ufisadi kama Mpina walivyokatwa NEC iliyokaa chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa. Pia tumeshuhudia, watuhumiwa wakuu ambao Katibu wa Itikadi ya CCM Mh Nape alitamka wazi kuwa lazima wang'oke, majina yao yakipitishwa.
Swali: Kazi aliyotumwa Ngwilizi ndio sababu kuu ya kushindwa kurudi NEC?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kazi ya ujenzi imekwisha, ndoo za kubebea zege za nini? Tupilia mbali kama kawaida yetu. Inawezekana pia hakufuata au hakutoa ripoti kama alivyoagizwa.
 
watu kama akina Ngwilizi hawakutakiwa tena kuwepo madarakani hadi leo hii kwani muda wao umeshapita na ndio maana baada ya kuwatumikia wananchi wameishia kutumikia status quo yaani business as usual. Ngwilizi mwenyewe ana kashfa kibao jamani wezi hawawezi kuwachunguza wezi wengine
 
Kwani Ngwilizi ni nani, au kuna ahadi ya CCM inayosema Ngwilizi atakuwa mjumbe wa NEC milele. Funzo ni kwamba mtu yeyote aweza kuchaguliwa kuwa mjumbe wa NEC. Hayo mengi uliyoanza nayo ni porojo tu.
 
Baada ya tuhuma za Rushwa dhidi ya wabunge wa Bunge la 10, Spika aliunda tume ya maadili chini ya General Ngwilizi kuchunguza tuhuma hizo. Kuna tetesi, report imekamilika, hata halmashauri kuu ya CCM ilitumia kuwakata baadhi ya wagombea. Tumeona wabunge wapambanaji na wapinga Ufisadi kama Mpina walivyokatwa NEC iliyokaa chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa. Pia tumeshuhudia, watuhumiwa wakuu ambao Katibu wa Itikadi ya CCM Mh Nape alitamka wazi kuwa lazima wang'oke, majina yao yakipitishwa.
Swali: Kazi aliyotumwa Ngwilizi ndio sababu kuu ya kushindwa kurudi NEC?

Hii hali ni nzuri sana kwa nchi...Maana ufisadi karibu utalipuka na kuungua kama jivu iwapo wazalendo tutajipanga vizuri, nasioni kwamba hatujajipanga the gud thing about this is tumejipanga....

Ukijaribu ku-conect the dots utagundua nguvu za watu fulani fulani zinapunguzwa hasa huko ndani ya magamba...Talk of Mkapa and the likes ili kusiwe na kizingiti chochote kwa mafisadi kutamalaki...Hawajali mambo ya kura kwani wanajua chakachua is the order of the day...Kwa upande mwingine nadhani is gud for us acha nisimalizie for our own benefits...
 
Back
Top Bottom