Tunajiandaa kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe?!

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,968
Tarehe mosi Septemba, CHADEMA wamepanga kufanya maandamano na mikutano ya kisiasa nchi nzima. Kwa mujibu wa katiba ya nchi hii na sheria za vyama vingi hayo wanayopanga kuyafanya yanaruhusiwa kisheria na ni haki yao na wala sio uhalifu.

Wakati CHADEMA wakijiandaa kwa hayo, rais wa Jamhuri amepiga marufuku mikutano ya siasa mpaka atakapomaliza muda wake wa uongozi. Marufuku ya rais haisemi ni kwa sheria ipi inayompa mamlaka rais kuzuia shughuli za kiisiasa au kupangia wanasiasa maeneo ya kufanyia siasa.

Kufuatia kauli ya rais, wakaibuka majemadari wengine wilayani na mikoani. Nao mishipa imewatoka wakisema hakuna maandamano wala mikutano kwenye maeneo yao kama rais alivyoagiza. Mmoja mwenye kihere here amekwenda mpaka kikosi cha kutuliza ghasia na kuwaagiza askari kuvunja Ukuta. Askari nao kama kawaida yao ya kutii amri wameibuka mitaani wakifanya mazoezi kujiandaa kupambana na raia wasiokuwa na silaha. Viongozi wa jeshi hilo wameibuka na kutoa kauli mbali mbali za vitisho kwa raia. Wamekuwa wakikamata tshirt zenye maandishi UKUTA kana kwamba kuvaa tishirt hizo ni uhalifu.

Mimi leo naliangalia hili suala kimataifa. Viongozi waliokosa busara na hekima wanafikiri kuingiza askari mitaani kwa kile wanachoita kufanya mazoezi ni ufahari na ni kuonesha maguvu ya vyombo vya dola hivyo kuwatisha raia. Katika hali ya kawaida hali hii inaifanya nchi ionekane haina amani kimataifa au inayokaribia kuingia kwenye machafuko. Madhara yake ni kuwa baadhi ya nchi zinaweza kuwataadharisha raia wake kuhusiana na kitakachotokea Tanzania hivyo kuwataka eidha waondoke au wajitenge na shughuli zozote zitakazowahusisha na raia wa nchi hii siku hiyo kwa maana ya kuwa wasije wakakumbwa na dhahama ya askari waliomwagwa mitaani kufanya mazoezi ya kukabiliana na raia.

Hali hii pia itawatisha wawekezaji ambao tunawatafuta kila siku kwani wataona hii nchi inakoelekea haitakuwa na amani hasa kutokana na msimamo wa kiongozi wake wa kutaka yeye tu ndiye awe kila kitu. Hakuna mwekezaji atapeleka mtaji wake mahali ambako kunaonekana hakuta kuwa na utulivu. Watalii ambao tunawategemea wanaweza kubadili uamuzi wa kuja Tanzania kwa kuwa wanaona maandalizi ya askari wetu wanaojiandaa kupambana na rais wasiokuwa na silaha eti kisa ni mikutano na maandamano ambayo siyo kosa kisheria.

Sielewi busara za viongozi wetu zimeenda wapi mpaka kuruhusu shughuli za kijeshi kufanywa mitaani na kuoneshwa na vyombo vya habari. Mimi naona kwa kukosa hekima na kutokuwa na uelewa wa teknolojia wao wanadhani yanayooneshwa kwenye TV. kutangazwa redioni na kuandikwa kwenye magazeti ikiambatana na picha za askari waliomwagwa mitaani eti kufanya mazoezi ni mambo watakayo yaona watanzania tu na hivyo kuiogopa serikali. Haya yanaonekana dunia nzima mpaka kule ICC. Na huu ni ushahidi unaowekwa wazi na serikali yenyewe endapo kweli siku hiyo kutatokea na umwagikaji wa damu kwasababu tu serikali haitaki wananchi wake kufanya shughuli zao halali za kisiasa na kijamii.

Kwa upande wa askari wa vyeo vya chini ambao ndio wanaotegemewa kutekeleza unyama dhidi ya raia wasiokuwa na hatia, mimi nawaasa kuwa pamoja na kuwa kazi yao ni kutekeleza amri za wakubwa, watumie busara kubwa kwani wanakwenda kupambana na raia wa nchi hii sio wageni, wanakwenda kupambana na dada zao, mama zao, kaka zao, baba zao na pia wadogo zao. Wajue ukitokea umwagikaji wowote wa damu au mateso kwa raia au ulemavu wowote watakousababisha, watajikuta mwisho wa siku wanabaki peke yao na wale waliowamrisha kutenda unyama huo wanapandishwa vyeo na wao askari wadogo kushia magerezani. Tukio la mauaji ya mwandishi Mwangosi kule Iringa liwe funzo kwao. Askari yule kijana hakwenda mwenyewe kwenye mkutano wa CDM ila alipelekwa kwenda kuzuia mkutano halali ambao haukuwa na vurugu yoyote mapaka pale amri ilipotolewa na mkubwa kuuvunja mkutano ule. Alitekeleza amri ya mkubwa wake bila kuchukua tahadhari na mwisho wa siku yeye ndiye aliyekamatwa na kushitakiwa hatimaye kufungwa wakati mkubwa wake licha ya kuhamishwa lakini pia akaongezwa cheo!

Kwa upande wa mtukufu rais mimi sioni kwanini anashupaza shingo kwa kitu ambacho si haramu na wala hakilengi kumuondoa yeye madarakani. CHADEMA wakiandamana au kutoandamana yeye atabaki kuwa rais wa nchi hii. Na kwakuwa sheria za nchi zinaruhusu, hakuna haja ya kupambana au kupingana na sheria ulizoapa kuzilinda. Kwanza tukio lenyewe ni la masaa yasiyozidi manne. Watu watatembea kuelekea kwenye uwanja wa mikutano kwa makundi kama tunavyotembea tukienda kuangalia mpira wa Simba na Yanga pale taifa halafu baada ya mkutano watatawanyika kurudi makwao sawa sawa na sie tunapotoka uwanja wa taifa. Wewe utakuwa zako ikulu wala hakuna mtu atakaye kusumbua lakini huenda ukapata ujumbe utakao kusaidia kufanya kazi vizuri. Nimeambiwa katika nchi za wenzetu zilizostaarabika na kuheshimu haki za raia wakati wa maandamano kama haya serikali hutuma watu wake ili kurekodi na kusikiliza kila kitu na yenyewe hufanyia kazi kwani maandamano na mikutano ni sehemu ya kufikisha ujumbe fulani kwa serikali na hata kwa Mungu.

Mtukufu rais anaweza kujitofautisha na watangulizi wake Benjamini Mkapa na Jakaya Kikwete ambao kwa nyakati tofauti chini ya tawala zao wamemwaga damu za raia katika shughuli za kisiasa za amani. Mkapa historia imesha mrekodi kwa tukio la mauaji ya waandamanaji wa CUF kule Zanzibar ambapo zaidi ya watu 20 waliuawa. JK naye hatasahaulika kwa matukio mbali mbali ya raia waliopoteza maisha katika shughuli za kisiasa katika mikoa mbali mbali kubwa la yote ni yale mauaji ya mwandishi wa habari kule Iringa. Magufuli anaweza kujitofautisha na hawa kwa kuamua kuwa katika utawala wake hatamwaga damu ya raia wasiokuwa na hatia hasa katika shughuli halali za kijamii na kisiasa kama hizi za upinzani. Nina wasi wasi kwa jinsi anavyo ongea na kujiapiza, ataanza mapema kunawa damu za raia wake hata kabla haja maliza mwaka. Naomba sana Mungu ampe hekima za kujua kuwa, kuwa rais ni zaidi ya cheo chenyewe cha urais. Anapaswa kuomba sana hekima yeye mwenyewe kutoka kwa Mungu badala ya kutaka kila wakati aombewe. Aombe hekima kama mfalme Suleimani ili aweze kutawala kwa haki.

Kwa upande wa msajili wa vyama vya siasa, nakushauri acha kuuma uma maneno. Kama ambavyo huwa unaibuka mapema kukemea vyama vya upinzani hata pale ambapo huwa hakuna ulazima, ni wajibu wako sasa kumwambia rais anapambana na sheria ambayo ameapa kuilinda hivyo anaonekana ni mvunja sheria. Mwambie wazi kuwa vyama vyote ikiwa ni pamoja na CCM vina haki ya kufanya maandamano na mikutano ili kueneza sera zao na kupata wanachama au washabiki wapya.

Kwa upande wa mwanasheria mkuu wa serikali, mimi nakuomba hebu msaidie mtufu rais kuwa kisheria anachofanya kinakiuka kiapo chake cha kuilinda na kuitetea katiba. Nyerere alisema hata kama tunampenda rais vipi na kama kabla ya mkutano tunakunywa nae kahawa au whisk lakini kama hatetei na kuilinda katiba, huyo hatufai! Itakuwa ni mapema mno kuanza kuona rais wetu hatufai.

Viongozi wa dini wasiokuwa wanafiki wanaweza kusaidia kuepusha dhahama hii kama wakiwa wakweli na wawazi. Bahati nzuri rais amekuwa akiwafuata huko huko. Ni wakati wao sasa kumweleza rais kuheshimu haki za raia kama vile ilivyoelezwa uhuru wa kuabudu na kutangaza dini katika katiba na vyama vya siasa navyo vimeruhusiwa na katiba hiyo hiyo ikiwa ni pamoja na uhuru wa kujumuika na kutoa mawazo. Tuna siku saba za kuepusha fujo zisizokuwa za lazima katika nchi hii. Na bahati mbaya sana mtu anayetakiwa kuepusha fujo hizi ni mmoja tu, naye ni rais wa nchi kwa kuwa haya yote yanatokea kutokana na amri zake. Kutengua amri siyo kushindwa il ni kujifunza na kupata ushindi mpya.

Mimi nimetimiza wajibu wangu kama raia mwema wa nchi hii kusaidia kuifanya nchi iwe na amani muda wote. Sitaki kushuhudia watu wakiuliwa, wakiteswa, wakijeruhiwa na kupelekwa magerezani kwa sababu tu ya kiburi cha madaraka. Madaraka huja na kwenda. Ndio maana wahenga husema Waliotangulia wako wapi? Kuna siku hata uwe na mabavu ya kutisha na kutetemesha dunia nzima utakuja kutoweka na kufutika kabisa katika uso wa dunia. Mwanadamu ni kitu gani?!
 
tema mate chini na wala usitamke maneno kama hayo! yashindwe milele!
MWENYE ENZI MUNGU IBARIKI NCHI YETU TANZANIA MILELE....TUBARIKI NA WATANZANIA TUNAO LILIA AMANI, UTUJALIE AMANI SISI NA VIZAZI VYETU NA ANAELILIA MACHAFUKO UKAMPE MACHAFUKO YEYE NA KIZAZI CHAKE....mtu anakula maneno ya kinywa chake, na watu huvuna walilopanda....NA IWE HIVYO MILELE YOTE....AMEN
 
Amani ya nchi hii ipo mashakani, leo asubuhi yalipita magari ya Polisi takribani kumi sokoni, wako kivita vita kabisa, bunduki na maji washa na mabomu.

Kilicho nisikitisha wananchi sokoni kila mtu yupo na shughuli zake km Ni kawaida.
Woga au kushangaa km zamani hakuna .

Lazima tutafakari ??wamekata tamaa kabisa au la???
 
Kwa hali ilivyo na hari zilizopo kwa pande mbili za ukuta na ant ukuta busara zinaitajika na hekima ya hali ya juu...leo nimeckia viongozi wa dini,shekhe mkuu,askofu kkkt,na wengineo wameonesha kwenda kinyume na maamuzi ya serikali coz kinaxhombwa kufanywa na ukuta ni haki kisheria na kikatiba so sinzonje angalie hilo na hekima na busara ixhukue mkondo wake.
 
Umeandika mareefu, lakini kwa ufupi sana kichwa cha habari siyo sahihi. Hapa TZ vita ya wenyewe kwa wenyewe hiyo sept 1 haiwezekani. Kinachowezekana ni vita kati ya wenye UKUTA na Jeshi la Polisi. Usipotoshe Watanzania ambao hawana wazo la kushiikishwa ukuta sept 1.
Wenye UKUTA wanatoka India au Somalia? Si ni watanzania hao hao ikiwa ni pamoja na polisi? Kilichotokea Zanzibar si kile kile? Raia wa Tanzania kuuawa na polisi wa Tanzania? Sasa hapo mkuu si wenyewe kwa wenyewe? Hicho kichwa cha post ni kuwa wewe hujatulia na kusoma vizuri. Kimeishia kwa kiulizo na mshangao. Wajuzi wa lugha wanajua maana yake!
 
Madaraka kitu kibaya Sana wanajiandaa kupiga ndugu zao kisasa mtu Fulani hataki kitu fulani
 
Hata uongozi wa sasa ulete maendeleo ya ulaya...bila uhuru na uongozi wa sheria kwa watu wake...ni buure kabisa...bureee...kwanin tuongozwe kibabe?sherria ziliwekwa za nini?
 
Umejuaje hao raia hawana silaha wakati tarehe 1 bado?
kwa akili ya kawaida tu haihitaji kwenda chuo kikuu utatambua kuwa raia hawana silaha. Swali lako linamsukumo wa KIMAHABA na chama fulani. Mahaba hayatusaidii siku askari wakianza kuwasaka hao wataoandamana na kukimbilia kwenye nyumba yenu usidhani wewe utakuwa salama. tukemee nguvu inayotumika badala ya kushabikia
 
ulishawai kukaa sehem ya kivita....?

ulishawai kushuhudia watu wakilushina risasi na si maneno

je unajua mlio wa mlipuko wa mabomu upoje ( achana na rocket ranger )

ulisha wai kupigwa risasi AK47 je maumiv yake yakoje

By ze way vita ni gharama kubwa sana mpaka uje usikie Tanzania imeingia vitan ujue kuna mataiafa yatakuwa yanadhamin iyo vita

Yan upande wa serikali itakuwa inadhaminiwa na mataifa mengine

Na waasi watakuwa wanadhaminiwa na mataifa mengine

na hayo mataifa lazma yanufaike na iyo vita
 
kwa akili ya kawaida tu haihitaji kwenda chuo kikuu utatambua kuwa raia hawana silaha. Swali lako linamsukumo wa KIMAHABA na chama fulani. Mahaba hayatusaidii siku askari wakianza kuwasaka hao wataoandamana na kukimbilia kwenye nyumba yenu usidhani wewe utakuwa salama. tukemee nguvu inayotumika badala ya kushabikia
Kilicho muhimu ni kuwakataa wote wanaotaka wananchi kuvunja sheria. Serikali imeshatoa maelekezo lakini kuna watu bado wanasema watakaidi. Kama Serikali imekosea, kwa nini huyu anayetaka kukaidi asiende mahakamani kudai hii haki? Kwa nini udai haki kwa shari wakati utaratibu upo wa kudai haki hiyo mahakamani. Inadaiwa katiba inasiganwa, inawezekana ni kweli lakini kwa nini usiidai kwa njia ya kimahakama? Unless kama kuna jambo linafichwa kwenye haya madai.
 
...Katika hali ya kawaida hali hii inaifanya nchi ionekane haina amani kimataifa au inayokaribia kuingia kwenye machafuko. Madhara yake ni kuwa baadhi ya nchi zinaweza kuwataadharisha raia wake kuhusiana na kitakachotokea Tanzania hivyo kuwataka eidha waondoke au wajitenge na shughuli zozote zitakazowahusisha na raia wa nchi hii siku hiyo

US Embassy tayari walishatoa advisory note kwa staff wao na yeyote anayepanga kutembelea nchi yetu kutokea kwao. Tayari tumeshaipaisha CV yetu kwa mambo ya kitoto kabisa.
 
Kwa hali ilivyo na hari zilizopo kwa pande mbili za ukuta na ant ukuta busara zinaitajika na hekima ya hali ya juu...leo nimeckia viongozi wa dini,shekhe mkuu,askofu kkkt,na wengineo wameonesha kwenda kinyume na maamuzi ya serikali coz kinaxhombwa kufanywa na ukuta ni haki kisheria na kikatiba so sinzonje angalie hilo na hekima na busara ixhukue mkondo wake.
Mkuu jaribu kuandika vizuri maana....
 
ulishawai kukaa sehem ya kivita....?

ulishawai kushuhudia watu wakilushina risasi na si maneno

je unajua mlio wa mlipuko wa mabomu upoje ( achana na rocket ranger )

ulisha wai kupigwa risasi AK47 je maumiv yake yakoje

By ze way vita ni gharama kubwa sana mpaka uje usikie Tanzania imeingia vitan ujue kuna mataiafa yatakuwa yanadhamin iyo vita

Yan upande wa serikali itakuwa inadhaminiwa na mataifa mengine

Na waasi watakuwa wanadhaminiwa na mataifa mengine

na hayo mataifa lazma yanufaike na iyo vita
Nauliza mm hapo, vita ni nini, na ukubwa wa vita ni upi,na mwisho, madhara ya vita ni yapi (vipimo ili tulinganishe na taswira iliyopo mbela yetu)
 
US Embassy tayari walishatoa advisory note kwa staff wao na yeyote anayepanga kutembelea nchi yetu kutokea kwao. Tayari tumeshaipaisha CV yetu kwa mambo ya kitoto kabisa.
Tayari athari, tena yenye ukubwa unaozidi tukio husika
 
Back
Top Bottom