Tunaibiwaaaaaa! Jamani wateja wa Vodacom someni hapa!

Mchekechoni

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
279
19
Kwa muda mrefu nimekuwa nafuatilia na kuchunguza kinachoendelea katika mitandao mbalimbali ya simu hapa nchini. Leo naona ni siku mwafaka kuweka bayana jinsi Vodacom inavyoibia wateja wake kama ifuatavyo: Leo asubuhi saa 10:48 salio langu lilikuwa shs.278.21 - saa 11:33 ni shs.278.17 - saa 12:29 ni shs.278.15 na saa 12:43 ni shs.278.13. Yaani salio linajipunguza lenyewe automatically bila ya kuitumia simu yako kwa rate ya shs.0.08 kila baada ya masaa mawili. Ndani ya masaa 24, tayari nakuwa nimeibiwa na Vodacom toka kwenye salio langu kiasi cha shs.0.96. Hivyo basi ukichukulia kwa uchache tu, kiasi cha wateja milioni mbili wa Vodacom ni kwamba tunaibiwa jumla ya shs.1,920,000/= ndani ya siku moja tu! Ukichukulia kwa mwaka mzima, wateja hao hao milioni mbili tunaibiwa jumla ya shs.702,720,000/=. To prove this; hakikisha salio lako kwenye laini yako ya Vodacom, kisha usipige simu wala kutuma sms ila angalia salio kila baada ya masaa mawili utaona kinachoendelea. Wanasheria tuungane kuwafikisha kortini Vodacom kwa wizi huu! Mitandao mingine (Airtel, Tigo, Zantel) hainyonyi wateja wake kwa mtindo wa aina hii!
 
Nikifanya uchunguzi leo, siwezi pata jibu, kwani ushawastua tayari.

Kwasababu wao hujua watanzania ni mabwege na wasahaulifu, baada ya wiki 1 au mbili, wataaendelea na wizi wao.
 
Kuna mwingine alikuja na wizi wa tigo akadai usiku hela inakatwa nikachunguza ila haikuwa kweli. Ngoja tucheki hili la voda.
 
achana na vikombi bana njoo huku kuna marcopolo linakusubiri..
 
unatumia simu aina gani na je ina applicatoons ambazo zinahitaji internet connectivity/zinaji-update auto? Natumia Ideos na inafanya background updates na nashindwa kuthibitisha
 
kaa wabongo noma. Eti ka tsh. 0.08 kwa masaa 2 ndo kanawsumbua? Voda inajathd sana kusaidia jamii, nyie mnataka pesa watoe wapi? Mnaacha kuwashambulia mafisadi wakubwa ie mapacha watatu mnaanda voda ambayo haikumalizii hata tsh. 1.0 kwa siku. Acheni hzo jamani.
 
Back
Top Bottom