Tunahitaji Taasisi huru za kura za maoni sasa

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,523
4,991
Tumezoea kusikia REDET au SYNNOVATE wakifanya utafiti mara moja moja kuhusu kukubalika kwa JK na mambo kama hayo. wakati wa uchaguzi mkuu pia ni kawaida kusikia wadau hawa wakitoa tathmini yao juu ya kukubalika kwa wagombea. sasa hivi tunategemea sana waandishi wa habari kubeba ajenda za kitaifa. kwa kiasi fulani pia makongamano na midahalo inachukua nafasi kupeleka mbele ajenda hizi.

Naamini kwamba huu ni wakati muafaka wa wadau wa kura za maoni kuuliza watanzania wana msimamo gani kuhusu suala la malipo ya DOWANS, kupanda kwa gharama za umeme, kupanda kwa nauli, na hicho kinachosemwa na taasisi mbalimbali kwamba "uchumi unakua", "inflation inashuka", maendeleo ya elimu, nk. masuala haya yanahitaji kupigiwa kura za maoni nchi nzima ili kutoa mwelekeo wa nchi kama watanzania wanavyoona, badala ya kutegemea magazeti tu ambayo yanahoji watu wachache na pia yana uwezekano mkubwa wa kupindisha habari. kama tutakuwa na taasisi huru ambazo zitakusanya maoni ya wananchi kama yalivyo na kuyatangaza, naamini tutakuwa tumeongeza silaha za kupambana na hao wanaodai kuhodhi mamlaka na hatima ya nchi yetu

Najua kutakuwa na wachakachuaji pia, lakini kama ilivyo katika nchi za wenzetu, na kama ilivyokatika magazeti, redio au TV; ukiwa na mashirika mawili matatu ya kura za maoni, yale yaliyo makini yatajipambanua tu. kutakuwa na yale ambayo ni more authoritative kuliko mengine.
 
Back
Top Bottom