Tunahitaji sindano za maji?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,876
2,744
Jana nimensikia mh Nahodha, waziri wa mambo ya ndani akiongea na waandishi wa habari akiwa pamoja na vyombo vyake vya usalama. Alikuwa akizungumza kupitia kipindi kilichorekodiwa cha Polisi na Jamii kinachorushwa na Channel Ten

Katika mazungumzo yake alizungumzia suala la kuwapa watu matumaini bila ya kuoyesha kuwakera na ndipo alipotumia mfano wa kuwachoma watu/watoto sindano za maji ili waridhike tu kuwa wamepewa tiba. Niliona kama waandishi waliguna katika kipengele hicho.

Tunahitaji kupewa ahadi hewa pamoja na kudanganywa kama watoto kwa kuambiwa kuwa matatizo yetu yatatatuliwa na kumbe anatukubalia tu ili tusimghasi?

Mko tayari kudungwa sindano za maji?
 
sindano za maji?

ni msemo au?

kama ni msemo, nini maana yake?

sijaelewa
 
sindano za maji?

ni msemo au?

kama ni msemo, nini maana yake?

sijaelewa

Ni msemo mkuu. Aliutoa mzenji Nahodha. Kwamba walipokuwa wadogo, wakipelekwa hospitali wakati wanaumwa ilikuwa hadi wachomwe sindano ndio wajione watapona. Vinginevyo wakipewa vidonge pekee huona kama hawatapona. So daktati kitu afanya ni kuchukua sindano na kuijaza maji kisha kuwachoma na ugomvi wao huisha hapo
 
Back
Top Bottom