Tunahitaji muuzaji wa duka

mipango

Member
Oct 16, 2011
5
0
Tunahitaji msichana kwa ajiri ya kazi ya kuuza bidhaa mbalimbali ktk duka letu.

Majukumu ya kazi husika ni kama ifuatavyo:-

1. Kukaribisha na kuhudumia wateja kwa ujumla
2. Kupanga bidhaa kwenye ngazi
3. Kuandika order za wateja
4. Kupokea simu za wateja
5. Kuandaa ripoti fupi ya mauzo ya kila siku nk.

Sifa za muombaji.
1. Awe mwaminifu.
2. Awe mchangamfu.
3. Awe mchapakazi.
4. Awe mwenye nidhamu
5. Awe anaishi Dar es salaam
6. Awe na kiwango cha elimu kuanzia kidato cha nne hadi kidato cha sita
7. Awe na uzoefu wa biashara au awe amepitia mafunzo ya biashara
8. Awe na umri kuanzia miaka 18 mpaka 30.


Maombi yote yatumwe kwa njia ya e-mail hii;
mipango2011@yahoo.com

Au unaweza kunipigia simu kwa maelekezo zaidi. Piga no.0779321400
 
Mkuu. umenikumbusha wimbo wa bongo F, usemao "kazi yangu ya dukani ohh oh oh yaniweka matataniii eh eh....
Lakini anyway ni fursa nzuri kwa anayehitaji kazi husika, basi akina dada changamkieni tenda.

Ila kazi ya kuuza duka inahitaji uaminifu sana maana ukiwa mkono mrefu huchelewi kupigwa chini.Na tatizo kwa wabongo wengi neno uaminifu ni msamiati mgumu, pia kauli nzuri kwa wateja ni tatizo sana kwetu wabongo, eti unakuta muuza duka anasoma gazeti tena la udaku wala hata karibu hakupi, tena nyie akina Dada ndo mmezidi mapozi sana.

​
 
Tatizo mpaka watoto wa kike kwani watoto wa kiume hatuwez, hebu mkuu tupatie ajira vijana wenye jinsia tofaut au sio wadau? Maana mi ni mmoja wa wataftaj kazi ni hayo tu naomba uunde kamati ufikirie ombi langu!
 
Tatizo mpaka watoto wa kike kwani watoto wa kiume hatuwez, hebu mkuu tupatie ajira vijana wenye jinsia tofaut au sio wadau? Maana mi ni mmoja wa wataftaj kazi ni hayo tu naomba uunde kamati ufikirie ombi langu!

mkuu.inkoskaz, ofisini kwetu tayari tumeajiri vijana wa kiume wengi tu, sasa tunataka kuleta uwiano wa kijinsia kwa kuajiri wasicha.

Asante.
 
Mimi niko tayari, au umeshapata mtu? Weka mshahara hapa kazi hizo ulizoweka hapo kila mtu anaweza kufanya labda kama ni mvivu kutoka tumboni mwa mamake.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom