Lekanjobe Kubinika
JF-Expert Member
- Dec 6, 2006
- 3,020
- 576
Najiuliza kama kuna watu wameanza kuwa kama mimi; vyama vyote vya kisiasa vilivyopo nchini haviwezi kutupatia kile tunachohitaji kama taifa. Siyo CCM, Chadema, CUF au TLP ambacho kilivyo sasa kinaweza kuwa tumaini la Watanzania. Je kuanzisha chama kingine ambacho kitatoka kwa wananchi na chenye ajenda ya mabadiliko ya kweli na kikiongozwa na watu wenye mwelekeo wa mabadiliko na wasiogopa political confrontation na ambacho hakitasita kufanya what is necessary to restore law and order and a constitutional rule kitaweza kuwa na nafasi.
Thanx Mzee, lakini hicho chama kipya sijui kitatoka Mbinguni? Hata hivyo vyama vilivyopo vinafanya kazi zao chini ya KATIBA ya CCM, maana yake mpaka CCM iridhie hicho chama kipya ambacho kitakuwa tishio kwa CCM yenyewe. Kwa maana hiyo ni kujitia kitanzi CCM. Katu kwa mwenendo huu hakuna chama kitakachofurukuta, hata kama kitakua na nguvu kama simba. Katiba iliweka kakipengele ya vyama vingi ili kumfurahisha Mwalimu JKN amalize maisha yake ya mwisho duniani kwa furaha, lakini hakuna katiba ya vyama vingi na kila chama kinachoonekana kukitingisha CCM wanapelekwa machekecheo huko wakachekeche maeneo nyeti kudistabilize strategies.
Tyson wa Las Vegas atagombanaje na Bwana Boramaisha wa Nyarugusu? Au Bill Gate agombane na Machinga? Timu ya kijiji cha msichoke haiwezi kupambana na Manchester United, bado ikang'ang'aniwa kwamba ni fair play.
Kama kweli tunataka mabadiliko yaliyokubaliwa kwa dhati, kila kitu kianze upya. Katiba Mpya, Mali za CCM ambazo zilikuwa za watu wote zamani ziende serikalini au kwa wananchi na kila chama kianze from zero level, halafu kila mmoja wao atueleze kwa nini yeye tumwamini zaidi ya mwenziwe.
Leka