Mujuni2
Senior Member
- Jun 11, 2008
- 142
- 3
Kwa mtazamo wangu ufisadi ni ubinafsi na kwa kawaida wanadamu wote ni wabinafsi ila viwango vinatofautiana.Ila ukitaka kuona mizizi ya ubinafsi huu(ufisadi) inaanzia katika ngazi ya familia, mfano:
Baba anaona ni bora kuwa anaonekana kwenye starehe (kupata kinywaji) lakini anashindwa kuwatimizia watoto mahitaji muhimu kama ya shule, chakula na kadhalika, sasa kwa wengine watasema huu si ufisadi bali ni kushindwa kuwajibika.Lakini ukiangalia kwa makini ni misingi ile ile ya kutimiza mahitaji yako kwanza kabla ya wengine.Mbunge akichaguliwa, na hasa akapata uwaziri ama cheo chochote kikubwa watu wake wa karibu wanaanza "unajua mzee ni miaka mitano tuu,au pungufu sasa changamka".Kwa mantiki hiyo labda kwanza tujue tunapambana na nani?
Hao tunaowaita mafisadi ni kuwa tuu labda wana nafasi au uwezo wa kifedha lakini kuna mafisadi ambao wanasubiri tuu chance yao ifike waonyesha makucha, na hawa ndio wako mstari wa mbele kutuonyesha kuwa wanakerwa na ufisadi, ila wakipata upenyo ni wabaya zaidi maana wana dhamira ila hawana uwezo wa kutimiza hila zao.
Kwa hiyo ndugu zangu tuanze kujisafisha wenyewe kwanza, kama maneno matakatifu yanavyosema "Toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako".