Tumuombee apone na kurudi salama nyumbani!

hii kitu ya kubadilisha damu ipo, lakini nisingependa kuingia kwa undani zaidi. Lakini nafahamu watanzania ambao wanafanyiwa hii kitu.

Jmk ana safari nyingine ya us kama salmb atakuwa hajapata nafuu ya kutosha anaweza kumpandisha 'cheo' mmoja wa mafirst ladies watatu waliobaki ili aende naye us.

ha ha haaaaaaaaaaaa hii ni kali
 
hivi hatuwezi kuwa na hospitali 2 au tatu za kimataifa kwa maana madaktari watoke nje [ikiwemo watanzania wanaotibu watu wa mataifa mengine] na kuwepo na vyombo vyote ila vile tu visivyoweza kuzuia mtu kufa tena vya kisasa ili tutoe huduma kwa nchi zote zinazotuzunguka na za mbali hasa zile ambazo kama sisi zinaamini kuna wagonjwa muhimu wa kutibiwa nje ya nchi na wagonjwa wa kawaida ambao hawastahili kutibiwa nje ya nchi.

Suala zima ni biashara tu au mnataka kusema kuwa hali ya hewa ya majuu pia ni sehemu ya tiba ya mgonjwa basi hospitali zijengwe mporoto, mbeya, ilula, iringa au monduli, arusha yaani kule kwenye bardiiii kama ulaya ulaya vile!

Vinginevyo mimi waziri kalala natilia mashaka uwezo wangu na uwezo wako wa kubadili nchi hii na maisha ya walalahoi japo walalahai kadhaa wananufaika na mfumo uliopo tena kwa mapana na marefu.

Sera zinazoweza kutuponya na makali ya utandawazi ni hizi za kuwa na hospitali za kisasa, shule za kisasa, vyuo vya kisasa, mahoteli ya kisasa, miji ya kisasa ambayo kwayo lazima watu wa nje watakuja tu kutumia hela zao hapa wakiwa hai au wamekufa!

Kazi kwenu!

itawezekana vipi wakati viongozi wetu wamekufa akili, kila mmoja anataka kupiga umachinga, kwa kufungua saloon au kaduka ka dawa au kagrosary au kuuza kitimoto au kadaladala?tunahitaji fikra hai mpya
 
Wako binadamu wengine wanapata faraja wakiona mtu/watu wako kwenye matatizo..it make them feel much better knowing that there is someone else suffering apart from them. Pole first lady


Na bahati mbaya ndio tabia ya watanzania tulio wengi,Na hiki nacho ni chanzo cha kusua sua ktk uchumi wetu.

Watanzania wengi wanafurahia zaidi na wanapata cha kuongea unapokua unabahatisha mlo mmoja kwa siku na mlo wenyewe wa dagaaa wa maji wasio na chumvi Na itawauma sana siku ukionekana una vinjari na kuku ama shangingi.
 
MNANISHANGAZA! Mnasema kubadilisha damu ni unscientific! Mnaishi wapi nyie? Nasita kusema, lakini nalazimika kutamka kuwa mimi mwenyewe nilishawahi kubadilisha damu! Sema sasa!

Hongera zako..
Kwa hiyo ulipobadilisha hiyo damu..virusi viliondoka..?? maana sijakataa kuna tiba za kubadili damu ila..hapa kuna insinuations za kubadili damu kutibu ukimwi!
 
Wako binadamu wengine wanapata faraja wakiona mtu/watu wako kwenye matatizo..it make them feel much better knowing that there is someone else suffering apart from them. Pole first lady

Mapambano,

Umeogea kitu very seriouse hapa.

Na kama matatizo = BURUDANI, inspiration and good feelings kwa baadhi ya viumbe wengine.

Ona kitakachotokea.

Je siku matatizo/maumivu kwa watu yakipungua au kwisha watatoa wapi burudani?

Itabidi wafanye kila kinachowezekana kupatikana matatizo hata ya kuforce na kuzua....kwani watapata wapi burudani?

Ni kama mtumia madawa ya kulevya! Atapata wapi burudani siku dunia ikiwa perfect with no drugs? Kweke hiyo perfection ni tatizo.

Mwanaburudani wa Matatizo hawezi kuishi bila matatizo...huu ni ugojwa...!!

Omba asije kuwa...Kiogozi ...atatuogoza kwenda kwenye maatizo simply yeye anaburudika...na hawa ndio mafisadi...that is their nature!!

Hawa ndio madictetor...burudani ni kupata matatizo..hata kama ni kuumiza wengine..kwenye ngazi ya juu kabisa...ni kula nyama za watu....kuumiza na kuona matatizo ...ni burudani...

We should be very carefull on what gives us HIGH!!!!
 
MNANISHANGAZA! Mnasema kubadilisha damu ni unscientific! Mnaishi wapi nyie? Nasita kusema, lakini nalazimika kutamka kuwa mimi mwenyewe nilishawahi kubadilisha damu! Sema sasa!

Hivi kweli wewe ulibadilishwa damu au uliongezewa damu? Kuna blood transfusion ambayo ni process ya kawaida ya kuwaongezea damu wagonjwa walio na upungufu wa damu (anemic) kutokana na sababu mbalimbali kama vile sickle-cell, ajali iliyosababisha damu kuvuja sana, kutopata mlo unaoongeza damu kwa muda mrefu, na aina nyingine za magonjwa ambazo huweza kumpunguzia mtu damu. Blood transfusion huwa inamuongezea mgonjwa damu juu ya ile aliyo nayo, haibadilishi damu ya mgonjwa.


Unapozungumuza ku-flush damu yote halafu mgonjwa apewe damu mpya kabisa hapo ndipo nisipokuelewa. Unajua ukisha-flush damu yote ikaisha mwilini hata kwa sekunde moja tu unaweza kuua ubongo wa mgonjwa na kumfanya asipone tena; ubongo hatuakiwi ukose damu hata kwa sekunde moja.
 
MNANISHANGAZA! Mnasema kubadilisha damu ni unscientific! Mnaishi wapi nyie? Nasita kusema, lakini nalazimika kutamka kuwa mimi mwenyewe nilishawahi kubadilisha damu! Sema sasa!

In medical field hicho kitu hakipo lazarosmtindi nadhani uliongezewa damu si kubadilishiwa kuna organ haziwezi kukosa supply ya O2 ambayo hutoka kwenye damu, uliza mtu yeyote wa medical acha kuleta hadithi za alinacha hapa, alfu lela ulela.

Ushi
 
Kama vile hii nimeisikia kwa wagonjwa wa Leukemia! Si kwamba wanatoa damu iliyomo kwanza na kuingiza nyingine la hasha! Nadhani wanatoa huku wakiingiza mpaka inabaki damu mpya! Lakini kabla ya kunirushia madongo, mimi si daktari!!!!
 
Na mimi nazidi kuhoji, huyu kwa siku za karibuni alikaribia kupewa cheo cha kikatiba! Alitembelea mkoa fulani akapokewa na mkuu wa mkoa! Sasa iweje aumwe tusielezwe! Kwenye kuumwa Low profile, ila kwenye mengine....

Low profile si kwenye kuumwa tu. Kwani hata akilala na mumewe huwa mnaambiwa? Na akienda kupimisha nguo mpya kwa fundi wake? Akienda saluni kusuka? Akienda kuoga? Sasa kila kitu kisemwe kwa sababu gani? Binadamu wote wanayo haki ya faragha, kama kweli yu mgonjwa basi hao wengine ambao wanayo nafasi katika faragha zake nyingine wanajua, haitoshi?
 
Labda siku zenyewe zimekaribia maana tuliambiwa hapahapa ukumbini kuwa Mama wa 1 anatarajia mtoto. Waliomwona hivi karibuni vipi bado?
 
Labda siku zenyewe zimekaribia maana tuliambiwa hapahapa ukumbini kuwa Mama wa 1 anatarajia mtoto. Waliomwona hivi karibuni vipi bado?

Hii kama ni kweli itapendeza sana. Natamani kujua huyo mtoto ataitwaje. Ninavyowajua wakwere (na wazaramo nk) huwa wanampa mtoto jina kutokana na matukio, nimeshakutana na kina Siasa, Kilimo, Azimio, Chaupele (mama aliugua upele), Chuki, Fitina (mama alifanyiwa chuki au fitina na wifize), nk. Wenzetu wamachinga (kabila ya Salma) wanatoa majina kwa kuangalia kitu kilicho karibu, kama Nyundo, Msumari, Panga, Sahani, Kijiko, Reli nk. Sasa huyu mtoto, kama mtoto kweli yupo, baba akitoa jina linaweza kuwa Epa, Fisadi, Rais, AU, Ikulu na mengine ya matukio. Mama anaweza kumchagulia jina kama Airport, Cheki (ya hela), Benzi (anayopanda daily) nk. Natamani ingekuwa kweli (and hope everybody understands I'm joking!).
 
Kama kungekuwa na umuhimu wa maombi wananchi wangetaarifiwa!hivyo basi hapa hakuna haja ya maombi!
Mwanaadamu yeyote humuombea mwenzake kheri.Sasa kama anaumwa muungwana humuombea mwenzake apate ahuweni.Kila mtu anyemuembea mwenzake kheri mungu naye humpa muombaji kheri ndivyo viongozi wa dini wanavyotueleza upo?
 
Namuombea mke wa Rais mama Salma Kikwete ambaye yuko nje ya nchi (jina na hospitali vimehifadhiwa hadi serikali wakiamua kuwaambia!) kwa matibabu apone hima na kurudi nyumbani salama. Tunakutakia kila la kheri chini ya mikono ya madaktari ili Mnyezi Mungu akupe uzima na afya ya mwili.

M. M.

Mkuu hapa JF huna haja ya kuficha kitu, sema yuko wako na anaumwa nini? sasa hapa JF tunapokuwa tunafichana details za habari ina maana gani, ni bora usituambia kitu kuliko ulivyofanya.

baadae utaona mnatumia kwenye PM kama ilivyokuwa habari ya shujaa wa ngono wa BOT nk.

Kwa mtindo huu neno "JF WHERE WE DARE TO TALK OPENLY" Sioni kaMA INAMAANA
 
Pole mama Salma. Najua utapona mapema na utarejea katika majukumu yako mapema. Tunakuombea


KUUMWA NDIYO UBINADAMU
 
Back
Top Bottom