Tumuamini nani? Kikwete au Membe?

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, kuna viroja vingi vinatokea. Mheshimiwa Membe aliwahi kukaririwa na Watanzania akisema kuwa anawajua na atawataja watanzania wote waliohusika na rushwa katika ununuzi wa rada. Na akasema wabaya wake wote kisiasa wakae chonjo kwani akiupata urais, watamkoma.

Juzi tumemsikia waziri wa sheria na katiba na kauli yake kupigiliwa msumari na rais JK akisema hakuna rushwa na pia hakuna mtanzania hata mmoja aliyehusika na rushwa katika ununuzi wa rada hiyo. HAWA WOTE NI VIONGOZI WA SERIKALI, TUMUAMINI NANI NA TUSHIKE LIPI? Je, kulikuwa na rushwa ama hakukuwa na rushwa?
 
Kuna mkanganyiko gani? Chikawe kasema hakuna ushahidi wa kutosha kumtia mtu hatiani kwa tuhuma za rushwa ya rada. Hii haimaanishi kwamba hakuna watuhumiwa wa rushwa ya rada. Hapa suala ni sufficiency ya evidence katika standard za kijinai but Membe was right kwamba kuna watuhumiwa wa kashfa ya rada na sasa majina yao yako bayana hata kule simiyu wanawajua.

Ndo maana tunaunga mkono kwamba watu hao wanaweza kushitakiwa kwa makosa mengine ya jinai ambayo siyo ya rushwa.
 
Hizi ni porojo za viongozi wetu dhaifu wakulitumikia taifa na wakakamavu kuiba na kufilisi mali ya uma. Shame on them.
 
Kuna mkanganyiko gani? Chikawe kasema hakuna ushahidi wa kutosha kumtia mtu hatiani kwa tuhuma za rushwa ya rada. Hii haimaanishi kwamba hakuna watuhumiwa wa rushwa ya rada. Hapa suala ni sufficiency ya evidence katika standard za kijinai but Membe was right kwamba kuna watuhumiwa wa kashfa ya rada na sasa majina yao yako bayana hata kule simiyu wanawajua.

Ndo maana tunaunga mkono kwamba watu hao wanaweza kushitakiwa kwa makosa mengine ya jinai ambayo siyo ya rushwa.

Chikawe naye ni Jaji? Mbona Mahalu aliburutwa mahakamani? Kulikuwa na ushahidi wa kutosha au visasi?
 
Mkuu sana,

Kwanza nikupongeze kwa kuwa katikati ya maamuzi. Wanyamwezi huishia kusema 'kale wa lelo' yaani leo ndio leo. Ona mkuu, unaweza kuamua kutoamini kwamba mungu yupo ila ujue kufa ni mara moja na ukifa kwa kuamini hilo siku ukimkuta utalia kivyako, lakini pia ukiamini mungu yupo siku ukifa na usimkute utaishia kulaumu woga wako kuponda maisha.

Sie wapagani tunaishia ku analyze mambo ili wewe mwenyewe uchague bega. Vitabu vya dini havisemi ni lazima uamini lolote kwa kuwa suala la imani ni utashi wa mtu. Chagua leo unaamini nini... Kauli ya waziri ama msimamo wa mkuu wake.

Tabora hii, na
GKassanga.
 
Hiyo ndiyo kazi ya ccmwabepande! Kulindana tu!
 
Kuna mkanganyiko gani? Chikawe kasema hakuna ushahidi wa kutosha kumtia mtu hatiani kwa tuhuma za rushwa ya rada. Hii haimaanishi kwamba hakuna watuhumiwa wa rushwa ya rada. Hapa suala ni sufficiency ya evidence katika standard za kijinai but Membe was right kwamba kuna watuhumiwa wa kashfa ya rada na sasa majina yao yako bayana hata kule simiyu wanawajua.

Ndo maana tunaunga mkono kwamba watu hao wanaweza kushitakiwa kwa makosa mengine ya jinai ambayo siyo ya rushwa.

Mbopo, inawezekan sheria huifahamu ama unaifahamu na umeamua kuipindisha. Serikali imesema hakukuwa na rushwa bali ni makosa ya uchapaji tu. Membe akasema wahusika anawajua na akawa anasisitiza wafikishwe mahakamani "sijui kama alipokuwa anasema alijiridhisha na suala la ushahidi". Wewe mbopo unaibuka na kusema, wanaweza kushtakiwa kwa makosa mengine. Yapi hayo? Niambie, tujadili.
 
Tusiwaamini wote maana hakuna anayesema anachomaanisha zaidi ya kuangalia ulaji wake. Wote ni waongo wa kutupwa. Kikwete aliahidi maisha bora akaleta maisha balaa wakati Membe aliahidi angewataja mafisadi sasa ameishia kujikanyaga utadhani kogori. Membe angeelezea ule mghorofa wake wa mjini mtwara amepataje pesa ya kuuinua kirahisi ingeleta maana.
 
Suala la radar ni Waingereza wamezidisha bei ya radar kuliko thamani yake, sasa hapo rushwa inatoka wapi? Na ilipobainika Kikwete akasema atazidai hizo fedha mpaka zirudi, kafanya hivyo, sasa inakuwaje?

Rushwa watoe Waingereza, halafu hao hao warudishe fedha za ziada. Hivi hamna mawazo hata kidogo?
 
Back
Top Bottom