Tumsaidieni Hasheem Thabeet

Thabeet ngugu yangu, anayekulaumu anakupenda na anayekushauri anakutakia mema. Bado nafasi ya kurekebisha udhaifu wako unayo, unalopaswa kufanya ni juhudi, juhudi, juhudi. Kurudi kwako katika kiwango sio tu kutakubakisha hapo ulipo lakini kutawapa moyo na ari vijana wote hasa wa bongo ambao wamewekeza imani na matumaini yao kwako. Usiwavunje moyo. Jitahidi na utafanikiwa. KILA LA HERI THABEET
 
anakuja bongo kularaha tu
badala ya kujikalish ahuko marekani na kujiendeleza mara moja kwa mwaka break kubwa inamtosha

mtanzania huyo labda na kuchawiwa anachawiwa aanze kusali MUNGU tu ndie muokozi wake
 
huyo mademu wa kibongo wamenyonya damu mpaka kadata na mazoezi afanyi ndo faida yake bahati aiji mara mbili
 
i get so upset when i see this! Huyu jamaa amepata nafasi nzuri lakini anachezea tu! Haoni Kobe anavyopiga zoezi! Huyo jamaa seriously needs to get his game going!
 
Let us give him sometimes more am sure he will change if he is serious!
 
Huyo sina hata mda nae, Wanajamii naomba niwaulize "kama tunahangaika hv na huyu m2 m1, vp huko Senegal ambako masupa staa wao kama Diof, Diop, Fadiga, Kamala, Diao nk nadhani hawalali wakiwaza jinsi ya kuwarudisha HEWANI hawa?" Thabeet kiwango kimeisha na wakati ni ukuta huwezi kupigana nao.
 
Ni kweli huyu kijana anahitaji msaada, si wa kifedha bali mawazo. Ni kashfa kurudi D League kwa mara ya pili. Rockets wanataka kumrudisha huko. Yeye anafikiri NBA ni lele mama, vihela vyote vitaisha kwa ajili ya matanuzi wakati shule nayo haikupanda vilivyo.

Haya mambo ya kuruka Bongo kila wakati, mara Singapore, mara DC kwenye club za wa-West na kujitunisha "Oh do you know me" ndo yanamponza mtanzania mwenzetu. Angalia mtu kama Deng kutoka Sudan (Chicago Bulls) anavyofanya mavituzi kwenye playground. Naamini Thabeet bado ana muda wa kurekebisha, lakini kama akiendelea kuziba masikio na kuzidisha tanuzi......NBA ndiyo itakuwa BYE BYE.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom