umenigusa mnoo mkuuu, na huo ndiyo ukweliKila mtu hatakiwi kudharauliwa wla kukejeliwa.
Dharau na kejeli siyo nzuri kwa yeyote yule, awe kiongozi au raia wa kawaida.
Hii thread ilivyo inaonesha kuabudu viongozi zaidi ya watu wengine ambalo ni kosa kubwa katika jamii.
Wote hatuwezi kuwa viongozi ila utu wetu ni sawa.
Yawezekana kejeli zinatokana tu na hasira za kuona uzembe na ukosefu wa uelewa wa watu waliokabidhiwa dhamana ya kutuongoza na ni kiashirio kwamba sisi kama jamii kwa ujumla tuna kila sababu ya kulaumiwa kwa kutokuwa makini na kuchagua wenzetu ambao hawawezi post zao au kuruhusu upendeleo wa kirafiki na kindugu bila kuangalia uwezo.
Tunatakiwa kujiuliza kwa nini viongozi wakejeliwe?
kasyabone tall, mkubwa ni jalala, asipolaumiwa yeye, alaumiwe nani?.Wengi wa watanzania ni walalamikaji tu, hawawajibiki kwa makosa yao wenyewe. Mimi sioni sababu ya kumsema vibaya rais wetu Mpendwa JK. Kwani hana makosa.
Watanzania wengi wanatumia uchaguzi vibaya na hawataki kuwajibika kwa makosa wafanyayo katika uchaguzi. JK hakujichagua mwenyewe, wala hakuchaguliwa na CCM tu. Bali alichaguliwa na watanzania wote na hivyo mnapomlaumu ni sawa na kujilaumu wenyewe, lakini kumlaumu kikwete ni kumbebesha mtu mzigo usio wake. Hapa watu wenye kustahili lawama ni watanzania waliomchagua.
Kama huamini hii subili Uchaguzi ujao pamoja na haya yote bado kikwete atashinda kwakishindo. Hebu tujiulize ni nani atakayemchagua? Kama si hawa hawa wanaolaumu leo. Mimi sioni sababu ya kulaumu na tukimlaumu yeye tunamuonea, tuwalaumu waliomchagua. Sisi tunapaswa kuchapwa na hali ngumu ya maisha. Kwani hakuna mwalimu mzuri duniani kama Maisha.
Wengi wa watu wanaolaumu hata hawapigi kura, kazi yao ni lawama tu. Kitu ambacho ni sawa na kelele za chura ambazo hazimzuii Tembo kunywa maji. Mtu muhimu kwa mwanasiasa ni mpiga kura, mpiga kura si mtu tu aliye na akili timamu namwenye kitambulisho cha mpiga kura. Mpiga kura ni mtu anaye piga kura anayeshiriki kupiga kura toka ngazi ya chama mpaka taifa. Kwani viongoza wanatoka kwenye chama, sasa wewe unasubili chama kikuchagulie halafu ukiletewa mbovu, hupigi kura. Hapa unaishia kulaumu tu.
Kila mtu ukimuuliza uchaguzi ujao vipi? Pamoja na kumlaumu sana atakuambia kuwa kikwete anashinda tu, wanasahau kuwa maneno huumba. Wakiisha umba wanarudi tena kulaumu. Ni bora kukaa kimya tu. Maana hata unaposema kikwete atashinda tu ni kuumba tu, wanakatisha watu tamaa ya kuleta mabadiliko. Utasikia CCM wanaiba kura, Je unapiga kura? Ni swali la kwanza kujiuliza.
Uchaguzi mwema.
jk ni mtendaji mzuri tu wakazi, wanaomsakama wana lao jambo
Nafikiri hukumwelewa alichokuwa anamaanisha, usikurupuke hakuzungumzia masuala ya utendaji.jk ni mtendaji mzuri tu wakazi, wanaomsakama wana lao jambo
Nakubaliana na wewe. Nimekuwa nikisema kwa muda mrefu kuwa tatizo la Tanzania lipo kwa wananchi wenyewe kwa kuchagua viongozi wabovu, wanaowasaliti, miaka nenda rudi. Utakuta viongozi wanavurunda, hakuna maendeleo, wanaibia nchi, lakini utakuta bado wanapewa wadhfa wa kuwa madarakani. Ni wakati umefika kwa kuacha kulalamika na kutimiza wajibu na haki yao ya kuchagua viongozi bora. Uwezo huo mnao na uko katika mikono yenu. Msidanganywe na kofia, t shirts, kanga, pilau na pesa. Mkipewa chukueni, lakini siku ya kupiga kura ukiwa peke yako, piga kura yako ya SIRI, kwa kumchagua kiongozi atakuyekufaa.
Bilicanas inahusika vipi na Kikwete kushindwa kufanya kazi? bro be proactive to what is on the table, hapa maada ni kikwete's failure to provide good and better life to Tanzanians na si Bilicanas-------
Mzee mwanakijiji inaonesha unataka kisa/mkasa na rais.
Kumbuka heshima kwa tamaduni zetu, kwamba wazee wetu hata vibabu dhaifu wakitufokea au hata wakitupiga huwa hatuwarudishii kwa kuheshimu ukubwa wao ilhali uwezo huo tunao. Huwa tunatafuta njia nzuri za heshima kukaa nao.
Jengine ikiwa ndio siasa,mbona kwa Kikwete zaidi!
Siipingi hoja yako, unao uhuru wa kujieleza. I strongly feel that you should intelligently demonstrate that what you are saying is valid and true. Ulivyoileta ni kama hoja ya kijiweni, hakuna facts. Kwa maana hiyo hapa utazomewa tu na wana haki hiyo. Pole sana.
Mnamo Mei 9 mwaka huu 2010 mwenyekiti wa CHADEMA bwana Freeman Mbowe alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Wasso huko Ngorongoro alimtaka raisi Jakaya Mrisho Kikwete ajiuzulu na kuondoka Ikulu mara moja. Kisa kushindwa kuwalipa wafanyakazi kiwango cha chini cha sh.315,000!
Kila siku za uchaguzi zinavyokaribia yaonesha watanzania wanazidi kukosa heshima kwa raisi wao. Kumfukuza rais aliyechaguliwa namna hii pia ni kuwakosea heshima mamilioni ya watanzania waliomchagua.
Sababu za kushindwa kuwalipa wafanyakazi kima cha chini Kikwete alizieleza na nyinyi mwawajua wanaofilisi uchumi wa nchi, mbona makucha yenu hamjayakunjua kiasi hicho kwao.
Rais wetu akicheka mwanuna na akinuna kwenu ni nongwa. Nyinyii!
Watumishi wa CHADEMA, BILLICANAS wanalipwaje?