Tumpe Rais Kikwete heshima yake

"Jana mwenyekiti wa CHADEMA bwana Freeman Mbowe alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Wasso huko Ngorongoro alimtaka raisi Jakaya Mrisho Kikwete ajiuzulu na kuondoka Ikulu mara moja. Kisa kushindwa kuwalipa wafanyakazi kiwango cha chini cha sh.315,000!"

Mambo hayo, kweli mh. Mbowe alitegemea maneno yake hayo yamfanye JK ajiuzulu? Kwanini hakuelekeza nguvu zake zote katika kuwashawishi wananchi wasimchague JK kipindi kijacho kwa sababu ya hayo madudu yake anayoyafanya. Tatizo hapa ni elimu yakutosha kwa wananchi wengi iwezekanavyo ili waweze kutambua pumba na kuiondoa kwenye mchele. Mh. Mbowe alisema anavyotaka yeye lakini hiyo haitusaidii sana kuleta mabadiriko tunayo yategemea. Wakati
huu sio wakupoteza kwa kufanya/kusema yasiyowezekana.
 
Mheshimiwa raisi !,nisikilize raia wako.
Hawa jamaa wametumwa wakuondoe madarakani.Sijui umewakosea nini?.Hii ni hadithi ya mwana wa kondoo na mbwa mwitu.Hata ukiwafanyia nini watakuzushia jengine.
Nakushauri utekeleze ahadi zako na za chama chako zote ili uondoke madarakani kwa heshima tushuhudie uongo wao.
Anza na ahadi za mwanzo kama vile matatizo ya Muungano,mahakama ya kadhi na OIC na muda ukiruhusu uje kwa hawa TUCTA.
 
Sasa Masoud mbona umeanza kumgeuka rais wako, kumbe hata wewe unajua hajatekeleza ahadi zake hata ile ya kwanza, basi si aondoke awaachie wengine.
 
JK anajuwa wasio na kazi ndo wengi na hivyo anataka kura zao,kazi itakuwa kwa wenye kazi kuwashawishi wasio na kazi kui vote out ccm....Ndo siasa
 
Mheshimiwa raisi !,nisikilize raia wako.
Hawa jamaa wametumwa wakuondoe madarakani.Sijui umewakosea nini?.Hii ni hadithi ya mwana wa kondoo na mbwa mwitu.Hata ukiwafanyia nini watakuzushia jengine.
Nakushauri utekeleze ahadi zako na za chama chako zote ili uondoke madarakani kwa heshima tushuhudie uongo wao.
Anza na ahadi za mwanzo kama vile matatizo ya Muungano,mahakama ya kadhi na OIC na muda ukiruhusu uje kwa hawa TUCTA.

We Masoud
Kumbe si mara zote unamwaga pumba. Walau hapa kidogo umeonyesha uelewa. Mwambie huyu Mkwere atekeleze ahadi kama raisi wa TZ. Pia asikilize matatizo ya wananchi wake.

Kinyume na hapo ataonekana kichekesho tu: bwana chekacheka.
 
Msimshambulie Masoud wandugu......Jibuni hoja kwa hoja(tutashindwa kuwatofautisha hapa)..............JF:Where we dare to talk openly...............hahaaaaaaaaaaaaaa

Mkuu wewe ndo mfano mzuri wa "great thinkers", ingekuwa wengi humu JF tuna mtazamo kama wako, JF ingekuwa mbali sana.
 
Wewe ndiyo zum....kuku kweli yaani Balantanda kusema hivyo ndiyo amekuwa greti sinka angechangia mada basi, ngoja nisubiri inawezekana na mimi ukaniita greti sinka kwa hii post.
 
Wewe ndiyo zum....kuku kweli yaani Balantanda kusema hivyo ndiyo amekuwa greti sinka angechangia mada basi, ngoja nisubiri inawezekana na mimi ukaniita greti sinka kwa hii post.

Ha ha! wewe kweli Luteni,inabidi tukupe rank ya juu sasa....Something like generel ha ha!
 
kusema ukweli watanazania tumeshikilia sana suala la heshima bila ya kulielewa ipasavyo!! wenzetu wazungu walishasema " respect can only be earned" , sasa kama mtu anacheo cha heshima kama cha urais, halafu anabehave kama mtoto mdogo, bado heshima yake ibaki pale pale? Ukimkuta mzee mwenye mvi anaiba au anatongoza binti mdogo wakati yeye ana mke na wajukuu, bado utamheshimu? kua serious mzee mzima, kama huna la maana la kusema, tuliza ball, hadharani hapa, watu wanapima IQ yako!! mimi naona watu bongo hawana heshima za kweli, wana heshima za uoga!! na kumtaka rais kujiuzulu na kumfukuza kazi rais ni vitu viwili tofauti kabisa. Pia kumbuka kuwa katika watanzania waliopiga kura, sio wote lazima walimpigia JK, sauti zao pia zina haki ya kusikika!! hehe
 
Jana mwenyekiti wa CHADEMA bwana Freeman Mbowe alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Wasso huko Ngorongoro alimtaka raisi Jakaya Mrisho Kikwete ajiuzulu na kuondoka Ikulu mara moja. Kisa kushindwa kuwalipa wafanyakazi kiwango cha chini cha sh.315,000!

Kila siku za uchaguzi zinavyokaribia yaonesha watanzania wanazidi kukosa heshima kwa raisi wao. Kumfukuza rais aliyechaguliwa namna hii pia ni kuwakosea heshima mamilioni ya watanzania waliomchagua.

ababu za kushindwa kuwalipa kazieleza na nyinyi mwawajua wanaofilisi uchumi wa nchi, mbona makucha yenu hamjayakunjua kiasi hicho kwao.

Rais wetu akicheka mwanuna na akinuna kwenu ni nongwa. Nyinyii!

Kwani kumwambia mtu ukweli ni kukosa heshima?Sijaona tatizo lolote kwenye hotuba ya Mbowe kwani kweli jk Kashindwa kutimiza ahadi zake za maisha bora kwa kila mtanzania.
Natamani wa TZ tungekuwa tunaona mambo na kuyatekeleza kama UK.
 
Tabia ya watu kuchangia humu kwa kuweka chapisho lenye kejeli, dharau na lisilokuwa na chembe ya heshima kwa viongozi wetu haipendezi hata kidogo.

Wote tuna hasira, lakini hasira zetu lazima zibebe Busara na Hekima kidogo ndani yake. Maneno yanayotumiwa na baadhi yetu kwa viongozi mfano Raisi si mazuri hata kidogo.

Kuna wachangiaji wanaleta mada moto na kali sana humu, zenye hasira na kutia hasira lakini ndani ya mada zao huwezi kabisa kuona tusi au dharau ya wazi. huu ndio ukomavu na huku ndiko kuwa Great thinker.

Haimfurahishi yeyote humu kuona kauli ambazo hazina heshima kwa viongozi wetu na hata kwetu sisi wenyewe.

Respect.
 
Wakati nakubaliana na wewe kuwa heshima ni muhimu kwa watu wote napingana na wewe vikali kwa kuwa biased. The way ulivyoweka statement yako ni kama vile hiyo heshima inapaswa kutoka kwetu sisi kwenda kwa viongozi tu na si pande zote mbili. Nikukumbushe sisi kama wananchi pia tunapaswa kuheshimiwa. Hakuna yeyote akiwemo rais mwenye haki ya kututukana kwa kuwa yeye rais si binadamu zaidi wala mtanzania zaidi yetu. Yeye sio master wetu ila he is supposed to be our servant and that's what we elected him to be period.
 
hao viongozi wenyewe hawatuheshimu sisi wananchi kama mabosi wao tuliowaweka madarakani, can you tell us why we should respect them? they are corrupt, thieves, bossy, without vision and alot more, why should i respect them? why? kama ni baba zako pole, but to me they are all fisadiz......
 
Hekima wewe umeona tu matusi na dharau kwa viongozi, lakini matusi na dharau hizohizo viongozi wanapotoa kwa wananchi hukereki nazo! that is weird? Hivi wewe kiongozi anaposema hata mkigoma miaka nane kima cha chini cha 315,000 hatulipi, wakati wao wanalipana mamilioni ya shilingi kwa kukaa bungeni miaka mitano tu, sio dharau hiyo! Kiongozi kuwatunukia wacheza ngoma shilingi 500 kila mmoja sio matusi hayo! Kiongozi anapohamishia ikulu ndani ya ndege na kuruka kila mara kama mbayuwayu huku wananchi wajawazito wakijifungulia njiani kwa ubovui wa barabara sio matusi hayo? kujisifia kuwa tumeongeza vyumba vya madarasa wakati the so called shule hazina walimu na vitabu, while their kids wako abroad wakisoma sio dharau hiyo?
 
Tabia ya watu kuchangia humu kwa kuweka chapisho lenye kejeli, dharau na lisilokuwa na chembe ya heshima kwa viongozi wetu haipendezi hata kidogo.

Wote tuna hasira, lakini hasira zetu lazima zibebe Busara na Hekima kidogo ndani yake. Maneno yanayotumiwa na baadhi yetu kwa viongozi mfano Raisi si mazuri hata kidogo.

Kuna wachangiaji wanaleta mada moto na kali sana humu, zenye hasira na kutia hasira lakini ndani ya mada zao huwezi kabisa kuona tusi au dharau ya wazi. huu ndio ukomavu na huku ndiko kuwa Great thinker.

Haimfurahishi yeyote humu kuona kauli ambazo hazina heshima kwa viongozi wetu na hata kwetu sisi wenyewe.

Respect.
Umekuwa biased sana.Go and tell viongozi wajiheshimu kwanza na sisi watuheshimu pia.
 
Spain Prime Minister Zapatero just anounced that the govt will cut civil service salaries by 5 % in 2010 and freeze them by 2011. I'm wondering .. siku JK akitamka hivi itakuwaje?
 
Tabia ya watu kuchangia humu kwa kuweka chapisho lenye kejeli, dharau na lisilokuwa na chembe ya heshima kwa viongozi wetu haipendezi hata kidogo.

Wote tuna hasira, lakini hasira zetu lazima zibebe Busara na Hekima kidogo ndani yake. Maneno yanayotumiwa na baadhi yetu kwa viongozi mfano Raisi si mazuri hata kidogo.

Kuna wachangiaji wanaleta mada moto na kali sana humu, zenye hasira na kutia hasira lakini ndani ya mada zao huwezi kabisa kuona tusi au dharau ya wazi. huu ndio ukomavu na huku ndiko kuwa Great thinker.

Haimfurahishi yeyote humu kuona kauli ambazo hazina heshima kwa viongozi wetu na hata kwetu sisi wenyewe.

Respect.

Mtetezi wa fisadi ni fisadi!
Kama wewe yanayoendelea hayakuumi waachie wahusika watoe madukuduku yao!!:angry:
 
Mheshimiwa Hekima Ufunuo, jambo unalolisema ni sahihi kabisa. But, the issue is a two way traffic. Viongozi/watawala nao wanapaswa kuwaheshimu wananchi/watawaliwa. Nitakupa mifano miwili: Kwanza, kejeli alizotoa Mungwana pale Diamond Jubilee kwa viongozi wa TUCTA na wafanyakazi kwa ujumla ndio sinazofanya wananchi wamdharau. Pili kejele ambazo Ben Nkapa alishatoa "kwamba watanzania ni wavivu wa kufikiri" ndio zinazofanya watu wamdharau kuhusu maamuzi yake mengi ambayo yamelitia Taifa hasara.
 
Back
Top Bottom