Tumpe Rais Kikwete heshima yake

Mzee mwanakijiji inaonesha unataka kisa/mkasa na rais.

Kumbuka heshima kwa tamaduni zetu, kwamba wazee wetu hata vibabu dhaifu wakitufokea au hata wakitupiga huwa hatuwarudishii kwa kuheshimu ukubwa wao ilhali uwezo huo tunao. Huwa tunatafuta njia nzuri za heshima kukaa nao.

Jengine ikiwa ndio siasa,mbona kwa Kikwete zaidi!
Utamaduni gani unaousema, that is stupid traditional heshima haiendi upande mmoja it is a two way traffic kama mzee wako hajiheshimu anatembea na visichana vidogo vya kuzaa bado huyo anastahili heshima? kwa siasa na maisha ya siku hizi utamaduni wako (wa zidumu fikra za m/kiti) hautekelezeki mbona mahakamani hawana sheria za wazee pekee.

Rais mwenyewe ndiye kaanzisha matusi kwa wafanyakazi, yeye ni rais kuwaambia wafanyakazi(watoto) hata wakigoma kwa miaka minane haisaidii kitu, maana yake nini hata ukilia usiku kucha hupati chakula si kauli nzuri ile ni utovu wa nidhamu kwa watoto wake, kwa nini na yeye hakutafuta lugha nzuri au njia nzuri kama unavyosea kuongea na wafanyakazi(watoto)? Mbowe kumwambia ameshindwa kazi ni sahihi kabisa Mbowe ni kama anawakilisha kilio cha watoto, kama mzazi huwezi kulisha watoto wako hustahili kuitwa mlezi mzuri. He deserves tena nchi yetu inaheshimu sana viongozi wake kuna nchi zingine hutupiwa mayai viza au kuzabwa vibao.
 
Uwezo wa kufikiria ni mdogo sana.
Mbowe yupo sahihi kabisaaaaaaaaaa
JK kawatukosea heshima watz na thamani yetu kwake in sawa na bure.
kafanya madudu mengi mno kuliko maelezo
Inasikitisha sana kwa yote
Hana heshima hata kidogo hata kwa wale awaitao wazee alioongea nao
 
kwangu mimi naamini maneno yale aliyoyatamka JK, ingekuwa ni Rais wa South AFRICA, Kesho yake kusingekalika, kungewaka moto, hata ingekuwa Kenya...anamatusi sana huyu Mkwere, ingekua yeye kaambiwa maneno yale unadhani angevumilia.

Nyinyi si wakweli wa munayoyasema.Ni uwazi kuwa munatumika kama Mgaya.
Hii sio ahadi pekee aliyoivunja Kikwete, na si ya msingi kuliko walizoshindwa kuzitimiza waliomtangulia kabla yake.
Huenda mumehemkwa kwa vile tu hii ndio mara yake ya mwanzo kununa.Ndivyo mtu mzuri anavyotakiwa kuwa;afurahi mara nyingi lakini akiudhiwa hasa asione haya kununa na hata kupigana.
 
Mbona ukali huo na matusi hakuyatoa dhidi ya wale waliomfadhili kwa mabilioni wakati wa kampeni yake ya 2005 kwa mabilioni ya shilingi? Na wanaifisadi nchi yetu kila leo? Awatolee ukali basi na matusi akina Rostam, Jeetu, Subhash, Manji na mafisadi wengine waliomchangia mabilioni.
 
Kiongozi lazima aheshimiwe tofauti na watu wengine, huo ni ukweli halisi kumkebehi ni kujitukana wenyewe, mtu mzima haitwi muongo ataambiwa hukusema kweli!!
 
Sababu za kushindwa kuwalipa kazieleza na nyinyi mwawajua wanaofilisi uchumi wa nchi,

Mkuu, sababu ya kutolipa kama ni uchumi kufilisiwa na hao tunaowafahamu itabidi ajue na yeye ni mmoja wao. Bahati nzuri kwake ni kuwa pamoja na kutambua hilo hatuna la kufanya kwani ni yeye ndiye kakamata mpini na sisi makali. Ingekuwa si hivyo, tungefanya kweli na si vinginevyo kwani sehemu ya wezi na mafisadi ni lupango, Ikulu hapangekalika !
mbona makucha yenu hamjayakunjua kiasi hicho kwao.
Tutakapoyakunjua makucha yetu tutaanza naye halafu ndio tuwashughulikie hao aliowateua na anaowalinda. Ukitaka kumwua nyoka unahakikisha umemponda kichwa !

Rais wetu akicheka mwanuna na akinuna kwenu ni nongwa. Nyinyii!
Hakuchaguliwa kucheka au kununa, kwani akicheka anamchekea nani na akinuna anamnunia nani. Aliikimbilia Ikulu sasa aonyeshe kwa nini alililia Ikulu na kama kumemzidi kimo, ajiuzulu. Hicho ndicho alichosema Mbowe, sasa wewe vipi - whatz up ?
 
Kiongozi lazima aheshimiwe tofauti na watu wengine, huo ni ukweli halisi kumkebehi ni kujitukana wenyewe, mtu mzima haitwi muongo ataambiwa hukusema kweli!!
So what is the difference muongo ni muongo tu hata upambe kwa maneno gani.
 
Very good answer, kuna watu wanaona bila CCM hawawezi kuishi, hawawezi kupata kazi, watoto wao hawawezi kwenda shule hawana mawazo mbadala, hufikiri watu wote tuko hivyo wanatushangaa sana wanapotuona tuko tofauti kabisa na wao, wanajiuliza tunawezaje kuishi bila CCM? kwa hiyo hawawezi kuisema vibaya CCM au kusema mabaya ya rais hata kama wanaona wazi anakosea, watajikomba waonekane wema kwa heshima ya woga, mimi naona huo ni utumwa wa kifikra na utumwa wa kifikra ni mbaya zaidi kuliko ule wa wakoloni maana unashambulia nafsi, nashukuru Mungu kuniepusha kwa hilo, na sometimes usikute mimi ninayemkosoa rais nafaidika na CCM kuliko yeye anayejikomba, if you cannot express your own views you are as dead as a slave one.

Huyo Mungu wa dini gani?
Nukuu na maneno yenu yawe "ndiyo ama hapana maana yakizidi hapo yatoka kwa yule mwovu" mwisho wa kunukuu.

Nanukuu tena"msiwe kama mfarisayo yule ambaye alifika ktk hekalu la Bwana na kuomba angalia Bwana mimi nikutolea zaka kubwa kila juma" mwisho wa kunukuu.

Nukuu" angalieni msiwe wepesi wa kuhukumu maana Bwana atakupa kipimo hichohicho, kwani wewe wawezaji ona kibazi ktk jicho la mwenzako yumkini ktk jicho lako kuna boriti?" mwisho wa kunukuu.

Heri yao wenye unyenyekevu maana wamekwishauona ufalme wa Mungu.
 
Nukuu" angalieni msiwe wepesi wa kuhukumu maana Bwana atakupa kipimo hichohicho, kwani wewe wawezaji ona kibazi ktk jicho la mwenzako yumkini ktk jicho lako kuna boriti?"
Sasa umerudi kwenye vitabu vitakatifu sio? Nitakusomea alibadili wewe! hahahahahahahaha haki ya Mungu watetezi wa Kiwete bwana mnanifurahisha sana!
 
Huyo Mungu wa dini gani?
Nukuu na maneno yenu yawe "ndiyo ama hapana maana yakizidi hapo yatoka kwa yule mwovu" mwisho wa kunukuu.

Nanukuu tena"msiwe kama mfarisayo yule ambaye alifika ktk hekalu la Bwana na kuomba angalia Bwana mimi nikutolea zaka kubwa kila juma" mwisho wa kunukuu.

Nukuu" angalieni msiwe wepesi wa kuhukumu maana Bwana atakupa kipimo hichohicho, kwani wewe wawezaji ona kibazi ktk jicho la mwenzako yumkini ktk jicho lako kuna boriti?" mwisho wa kunukuu.

Heri yao wenye unyenyekevu maana wamekwishauona ufalme wa Mungu.
Unaweza kusema tena ulichotaka kumaanisha infact I didnt get you
 
Unaweza kusema tena ulichotaka kumaanisha infact I didnt get you

Nilitaka kusema hivi.
Kupanidshiana hasra ama kupeana maneno makali na kuwa jeuri dhidi ya muharifu wako mara nyingi kama si zote yanatoka kwa kwa muovu na si Mungu. Na kama Kikwete amewaudhi vya kutosha ni kumsubiri oct na kusema NDIYO ama HAPANA.

Na hata hivyo huwezi mhukumu mtu kwamba anajipendekeza maana sie tunaohukumu yawezekana tu waouvu zaidi kuliko anayehukumiwa. Kingine kuhusu mfarisayo, wewe mwenyewe huwezi jitolea pointi kwamba unachofanya ni sahihi.
 
Kama anafanya madudu lazima aambiwe tu kwani yeye amekuwa nani kuna marais wenye heshima zao kuliko yeye wanaambiwa wazi wazi, kama umeelimika huwezi kusema ndiyo au hapana tu bila kutoa sababu hapa tunasema na tunatoa sababu kwamba kama anataka kuheshimiwa lazima na yeye awaheshimu wadogo si kwa kuwatukana kama alivyofanya Diamond.

Kuhusu puppets wake lazima tuwaseme mtu anashangilia hata pasipostahili kushangiliwa, mfano wazee wa Diamond ambao wengi wao walikuwa kwenye ile EAC iliyokufa leo ukiwauliza walikuwa wanashangilia nini hawatakujibu ndio hao ma puppets ninaowasema wa kupewa alfu na kofia na kusahau matatizo yao.
 
Aisee, naona huyu jamaa aliyeianzisha mada hii si tu ni mwanachama mpuuzi wa chama cha mapinduzi bali ni kibaraka ambaye anadhani Tanzania ya leo inaweza kuendeshwa kwa mawazo ya juzi na jana! Nadhani hata wanachama wazalendo wa kweli wa CCM wamemshtukia kwamba kama Raisi ni gari, basi limeshakosa breki na dereva amashalikimbia muda mrefu uliopita. Ama pengine huyu jamaa ni mmojawapo wa wale ambao the current system ambayo ni mbovu imemkuta yupo kati ya wale wanaofaidi 30% ya bajeti, so He wants nobody to upset the apple cart.
na kama ndivyo, nasikia harufu ya UBINAFSI na UVIVU WA KUFIKIRI
 
Msimshambulie Masoud wandugu......Jibuni hoja kwa hoja(tutashindwa kuwatofautisha hapa)..............JF:Where we dare to talk openly...............hahaaaaaaaaaaaaaa
 
Kikwete ndiye kawakosea watanzania wote heshima. Kwa rais ambaye ameshinda kwa asilimia 80 ni aibu kuwatosa mamilionn ya watz na kuwakumbati mafisadi wachache. Kwa udhaifu wa kiuongozi alioonesha jk hastahili heshima yoyote. Na kuonyesha utovu wa nidhamu kwa waajiri wake yaani wapiga kura ameamua kuwatukana kwa kuwaita waongo,wanafiki na wazandiki. Jk aelewe kuwa mgomo siyo hoja ya mgaya bali ni hoja ya wafanyakazi wote ambao ndiyo wapiga kura. Na jk ataendelea kudharaulika hadi oktoba. Huo uzandiki na unafiki wa redet usimvimbishe kichwa mpaka kutukana wapiga kura na walipa kodi anayotumbua usiku na mchana yeye na genge lake
 
Back
Top Bottom