Tumjadili Nape Nnauye

wakusoma

JF-Expert Member
Feb 25, 2008
1,085
1,049
ana umri gani?,amesoma wapi?,ana elimu gani?ameoa?anwatoto wangapi?,baba yake marehemu ukiachia sifa yake ya kuwa mzee wa totos je hakuwa fisadi?wnamiliki nini? habari za ndani zinasema mfadhili wake mkubwa nape ni mfanyabiashara 1 mkubwa hata bongo amabye alikuw anampa hela ili afyatue domo lake kuwasemea vibaya kina lowasa.

je nape si mchafu?hata kashfa yeytote hata ya kuchukua vibinti vya shule?kijiwe chake ni wapi?naombeni wadau hebu tumuanike huyu dogo janja mambo yake yote,ili jamii imjue.maana naona anakuja kwa kasi kama moto wa kifuu.

mjumbe hauwahi!!!nimewakilisha!!!
 
nape yuko hapa na anasoma hii!!!atupe taarifa yeye mwenyewe manake ni kinara wa kupanua mdomo!aghhhhhhhhhhhhhhh
 
ana umri gani?,amesoma wapi?,ana elimu gani?ameoa?anwatoto wangapi?,baba yake marehemu ukiachia sifa yake ya kuwa mzee wa totos je hakuwa fisadi?wnamiliki nini? habari za ndani zinasema mfadhili wake mkubwa nape ni mfanyabiashara 1 mkubwa hata bongo amabye alikuw anampa hela ili afyatue domo lake kuwasemea vibaya kina lowasa.

je nape si mchafu?hata kashfa yeytote hata ya kuchukua vibinti vya shule?kijiwe chake ni wapi?naombeni wadau hebu tumuanike huyu dogo janja mambo yake yote,ili jamii imjue.maana naona anakuja kwa kasi kama moto wa kifuu.

mjumbe hauwahi!!!nimewakilisha!!!

Kwanza tukujadili wewe?
 
Cha kujadili pekee ni impact yake kwa umma wa Watanzania, na haya mengine yatapatikana by the way!
 
Tunajadili kuhusu TANZANIA TUNAYOITAKA NA HATUWEZI KUMJADILI MTU
 
fanya kitu moja. Nenda jukwaa la siasa utafute threads zote zinazomhusu then uzichambue utapata unachotaka-wasifu
 
Edwin Mjwahuzi, Ruvuma
VITA ya maneno kati ya Chadema na CCM jana imechukua sura mpya baada ya Fred Mpendazoe kumtaja Katibu Mwenezi na Itikati wa CCM, Nape Nauye kuwa miongoni mwa vigogo sita walioanzisha Chama cha Jamii (CCJ) .Mpendazoe alitoboa siri hiyo jana alipokuwa akituhubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mbamba Bay kilichopo katika wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

Mpendazoe alijitoa CCM Machi 30, mwaka jana akiwa Mbunge wa Kishapu na kujiunga na CCJ Aprili 16, mwaka huo kabla ya kuhamia Chadema, baada ya CCJ kukosa sifa na kufutwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.Akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Mbamba Bay, mkoani Ruvuma jana, Mpendazoe alisema ameamua kuliambia taifa ukweli kuhusu Nape, ili umma uepuke kudanganywa na propaganda za kijana huyo

.“Kelele zote anazopiga Nape kuitetea CCM ni za kinafiki kwani aliwahi kukigeuka chama hicho na kushiriki katika mipango yote ya kuanzisha CCJ”.Hata hivyo, Nape alipoulizwa na gazeti hili jana kuhusiana na madai hayo ya Mpendazoe, hakukataa wala kukubali kushiriki kuanzishwa CCJ, badala yake alisema, "Cha msingi waeleze (Chadema) CCJ ilikufaje, wasiseme ilizaliwaje, maana kuzaliwa ni sherehe na kufa ni kilio.” Nape ambaye hakusema lolote kama kombora la Mpendazoe ni la kweli aliwageuzia kibao Chadema akisema, "Pamoja na hayo yote, waache (Chadema) kubaka demokrasia."

Alifafanua akisema "Watanzania walipiga kura kuichagua CCM iwaongoze kwa miaka mitano ijayo, sasa wanaposema tutaandamana nchi nzima ili serikali iondoke kabla ya muda huo, huku ni kubaka demokrasia na ni uhaini."Mpendazoe alisisitiza kuwa Nape alishiriki katika kuandaa na kuandika katiba na miko ya uongozi ya CCJ, kutafuta fedha za kukuza chama na jengo la kuweka ofisi za chama hicho.

Alisema: “ Huyo Nape anayepiga kelele za kuitetea CCM ni mnafiki mkubwa pengine kuliko wanafiki wote hivi sasa. Mimi na yeye pamoja na wanaCCM wengine wanne, ndio tulioamua kuanzisha CCJ.“Nape ndiye aliyepewa jukumu la kutafuta nakala za katiba za vyama tawala vya nchini za Afrika, ili kupata katiba nzuri ya itakayoigwa katika kuandika katiba ya CCJ.”

Alisema Nape alilitekeleza vizuri jukumu hilo na kufanikiwa kuipata katiba ya chama tawala cha Afrika Kusini cha ANC, ambacho ndiyo kilitumika kwa kiasi kikubwa kuandaa katiba ya CCJ.Alisema yeye, Nape na vigogo wengine aliosema atawataja muda ukifika walifanya vikao vyote vya siri hadi wakaanzisha chama hicho cha CCJ.

“Tulifungua mtandao maalumu wa kuwasiliana kwa internet, ambao baadaye wenzangu waliufuta baada ya kubadili mawazo dakika za mwisho. Lilipotulazimu kukutana mimi na Nape tulipendelea kukutana katika eneo la vinywaji pale Mlimani City, jijini Dar es Salaam”.Alisema walifanya hivyo ili wasitiliwe shaka na maafisa usalama wa taifa waliopewa kazi ya kupeleleza wanaCCM waliohisiwa kutaka kuanzisha chama kipya.

“Nape alibadili mawazo ya kutaka kuihama CCM baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi, kwa kuwa alikuwa na uchu wa madaraka ,” aliongeza. Alisema Nape aliisaidia CCJ kwa kukipa siri nyingi ikiwamo mambo yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mikutano ya Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) na hata vikao vilivyokuwa vikifanyika katika Ofisi Ndogo ya CCM iliyopo Lumumba.“Nape pia alitupa siri kwamba baadhi ya walioanzisha CCJ walikuwa wanakaribia kufukuzwa kwani katika mkutano wa NEC, majina ya baadhi yao yalitajwa na kujadiliwa kwenye kikao hicho.'

Tuhuma za Chadema dhidi ya Nape na majibu ya Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM, ni mwendelezo wa siasa za jino kwa jino za kurushiana makombora yaliyobeba tuhuma nzito ndani yake.

Mei 12 mwaka huu Nape alimtaka Dk Slaa kuliomba radhi Bunge, huku Chadema nayo ikimtaja Nape kwamba ni mtuhumiwa wa ufisadi wa EPA uliofanyika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo Sh133 bilioni zilikwapuliwa.
Tuhuma hizo kutoka kila upande, zimekuja baada ya Nape kutaja alichokiita unafiki wa Dk Slaa kwa kushinikiza kulipwa mshahara wa Sh7.5 milioni na Chadema, wakati alikataa mshahara wa Sh7 milioni alipokuwa mbunge akidai ni mkubwa na uliwanyonya Watanzania.

Katika mkutano wake wa hadhara siku hiyo Nape alimtaka Dk Slaa kuliomba radhi Bunge na wabunge kwa kile alichoeleza kuwa alipokuwa Mbunge wa Karatu, alichochea chuki kwa wananchi dhidi ya taasisi hiyo.
"Najua Chadema watakuwa wanajibu, lakini nasema msimamo wangu uko mbele zaidi kwamba Dk Slaa aliombe radhi Bunge na wabunge, kwani alichochea chuki kwa wananchi dhidi ya Bunge, halafu yeye anakuja kuchukua mshahara zaidi ya ule aliojidai kuukataa. Huu ni unafiki," alisisitiza Nape.

Nape alisema Dk Slaa ni Padre hivyo pia alipaswa kuungama kwa Mungu kwa kutokuwa mkweli ndani ya dhamira yake."Bahati nzuri Dk Slaa ni Padre, namshauri pia amwombe radhi Mungu, kwani amekuwa akipita mitaani kupandikiza chuki miongoni mwa Watanzania kumbe naye hana maadili yoyote," aliongeza Nape.

Wakati Nape akitoa shutuma hizo dhidi ya Dk Slaa, siku hiyo Mei 12, Chadema aliitisha mkutano na waandishi wa habari ambako licha ya kufafanua kuhusu mshahara wa Katibu Mkuu huyo na ununuzi wa magari, ilimwita Nape kuwa ni 'Vuvuzela' na kwamba hana sifa ya kuinyooshea kidole Chadema.

“Tuna ushahidi wa kutosha kuwa mmoja wa watu walionufaika na fedha za EPA kupitia kwa Jeetu Patel ambaye ameeleza vizuri jambo hili katika maelezo yake mbele ya kamati ya Rais,” alisema Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Anthony Komu
kutoka gazeti la mwananchi
 
kujadili maisha ya mtu ni umbea. jadilini huyu jamaa kwa mambo tyake anayofanya kuhusiana na taifa kwa ujumla.
 
nape ni mtoto wa mkulima tu, ila ni mjanja wa maisha kwa kuchagua njia sahihi ya kuishi vizuri.
 
kweli wewe huna mpya! baada ya kuandka mambo ya maana,unataka habari za watu ,wabongo bwana ndio maana hutuendelei!!!!
 
ana umri gani?,amesoma wapi?,ana elimu gani?ameoa?anwatoto wangapi?,baba yake marehemu ukiachia sifa yake ya kuwa mzee wa totos je hakuwa fisadi?wnamiliki nini? habari za ndani zinasema mfadhili wake mkubwa nape ni mfanyabiashara 1 mkubwa hata bongo amabye alikuw anampa hela ili afyatue domo lake kuwasemea vibaya kina lowasa.

je nape si mchafu?hata kashfa yeytote hata ya kuchukua vibinti vya shule?kijiwe chake ni wapi?naombeni wadau hebu tumuanike huyu dogo janja mambo yake yote,ili jamii imjue.maana naona anakuja kwa kasi kama moto wa kifuu.

mjumbe hauwahi!!!nimewakilisha!!!

inaelekea unampenda Nape, mtafute ukanywe nae chai
 
Back
Top Bottom