Tumewagaragaza CCM

Uchaguzi mkuu wa wabunge na madiwani hutanguliwa na uchaguzi wa serikali za mitaa. Hapa ndipo tunapokua na kipimo kizuri cha kuangalia umaarufu wa chama na kukubalika kwa chama husika hasa ktk ngazi za chini kama dira ya mtazamo wa kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu. Mara nyingi chama kinachochukua hatamu ktkt serikali za mitaa yaani vijiji na mitaa kwa mjini kina nafasi kubwa kushinda ktk sehemu husika. Sehemu yenye wabunge wengi wa upinzani, walishinda pia viti vya vijiji na mitaa ingawa hii inaweza isiendane sana na mazingira ya sasa ya siasa hasa kwa chadema maana upepo mkubwa ulibadilika ktk kipindi kisichozidi miezi nane kabla ya uchaguzi. Ila ukweli ni kwamba huwezi kujihakikishia ushindi kwa kiasi kikubwa kama hukufanya vizuri ktk uchaguzi huu wa ngazi za chini.

Maelezo haya nikueleza juu ya umuhimu wa ushindi huu ambao wengine wameonekana kubeza na kuhisi si taarifa muhimu kushirikishana.

Tushirikishane na kushiriki kujenga mageuzi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya uongozi.

wenyeviti wengi wa mitaa na wenyeviti wengi wa vijiji ndio watakao tuhakikishia ushindi 2015.
 
Ha ha ha aaaaaaaaaaaaaa, craaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap hakuna kitu hapa. Hivi tukianza na kuweka matokeo ya vijiji humu JF patakalika humu ndani ?????. Hii thread haina mashiko ndio maana imekosa wachangiaji


Imekosa wachangiaji lakini wewe ni mchangiaji wa kwanza....tehteh teh
 
Kidogo kidogo hujaza kibaba. Hizi ni dalili nzuri za cdm kuota mizizi vijijini!
 
Ha ha ha aaaaaaaaaaaaaa, craaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap hakuna kitu hapa. Hivi tukianza na kuweka matokeo ya vijiji humu JF patakalika humu ndani ?????. Hii thread haina mashiko ndio maana imekosa wachangiaji


Mkuu, si ukubali tu kuwa mmeshindwa, na useme mtajipanga upya kwenye uchaguzi ujao? Kelele zote hizo za nini?
 
Hiyo ndio saizi yenu.
Sijui kama ni saizi yetu au ni saizi ya wote, kwani kwenye uchaguzi huo na CCM nayo ilisimamisha Mgombea ambaye alishindwa na wa kwetu. Kwa sisi tulioko "field" tunajua nini maana ya ushindi huu.

Kwenye uchaguzi huo rasirimali vitu na rasirimali watu kati ya CHADEMA na CCM ilikuwa ni tofauti kabisa. Uchaguzi huu uliingiliwa kwa kiasi kikubwa na dola na watendaji wa Halmashauri kwa kuipendelea CCM. kuna mahali tumepata Mwenyekiti (Wasa) wa kitongoji na wajumbe sita kwenye serikali ya Kijiji.

Matokeo haya nimeyaweka kuwapa taarifa watu waishio mijini kwamba hata vijijini watu wameshaamka. Mikutano yetu tunayoifanya huko hivi sasa inahudhuriwa na watu wengi sana kuliko ilivyokuwa zamani na ushiriki wao kwenye mikutano hiyo inatia moyo. Hivi sasa Lukuvi yuko kwenye jimbo analoliwakilisha la Isimani akieneza propaganda kwamba CHADEMA ikishinda 2015 itakubaliana na Ushoga kwa sababu ina ushirikiano na Conservative ya Uingereza. Haya mambo ya Lukuvi kutapatapa yasingeweza kufanyika au kuhangaika nayo miaka 5 iliyopita kwani watu wa vjijini waliamini CCM ni serikali na Serikali ni CCM.
 
Hongera. Operesheni Sangara na ile ya Nyanda za juu kusini zilikuwa za mafanikio. Operesheni sasa ipelekwe mikoa ya Pwani, Tanga, Tabora na Lindi...
 
Dua la kuku halimpati mwewe. Hivi mnafikiri ni rahisi ki hivyo. Oteni ndoto za mchana wa saa nane tu!! CCM GARI KUBWA. Ndio maana tunasema na nyie mnajua kuwa CCM Ni No 1.

Thanks and Regards,

Kada wa CCM.

1+1=2015 over. Out
 
Jumapili ya tarehe 18/12/2011 kumefanyika uchaguzi kwenye Kijiji cha Magulilwa Kata ya Magulilwa kwenye Halmashauri ya Iringa Vijijini, na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:CHADEMA - Kura 475CCM - Kura 290Ni hayo tu wandugu.
BABA Allenkilewella, AKSANTE KWA HABARI HII, IMAGINE NDO NAFUNGUA JF NAKUTANA NA SUCH A GOOD NEWS, OH LORD THANKS ALOT, LEO YOTE NI RAHA PIA UTAMU, NATUMAI MSHIKAMANO PIA USERIOUS WENU NDO UMEKIPA CHAMA CHETU USHINDI, NASI KIGAMBONI KISIWANI TARATIBU TUNAJIANDAA KIMYA KIMYA KWA UCHAGUZI WA DIWANI NATUMAI TUTAIBUKA KIDEDEA KWANI NI DHAHIRI MOTO WA MAGEUZI YA KWELI ULIOWASHWA NA CDM HAUTAZIMIKA MPAKA 2015, MUNGU IBARIKI CHADEMA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
ccm wakileta kata walizoshinda jf itajaa, jiamini tu ndg yangu au ulikuwa hutegemei ushnd nn? Subri gharika la igunga likifika kg kwa kafulila, ndio utakitambua chama cha magamba.
kule igunga salama yenu si mlionga chakula cha msaada pia mlionga wali na nyama kwa wanavijiji na pia serikali yote ya haramu ccm ikaamia uko, mliogopa nini?? thread hii imeletwa kuwajulisha kuwa msemo wenu wa kuwa mko imara vijijini inafikia mwisho sasa magamba pia mafisadi wakubwa nyie
 
Sijui kama ni saizi yetu au ni saizi ya wote, kwani kwenye uchaguzi huo na CCM nayo ilisimamisha Mgombea ambaye alishindwa na wa kwetu. Kwa sisi tulioko "field" tunajua nini maana ya ushindi huu.Kwenye uchaguzi huo rasirimali vitu na rasirimali watu kati ya CHADEMA na CCM ilikuwa ni tofauti kabisa. Uchaguzi huu uliingiliwa kwa kiasi kikubwa na dola na watendaji wa Halmashauri kwa kuipendelea CCM. kuna mahali tumepata Mwenyekiti (Wasa) wa kitongoji na wajumbe sita kwenye serikali ya Kijiji.Matokeo haya nimeyaweka kuwapa taarifa watu waishio mijini kwamba hata vijijini watu wameshaamka. Mikutano yetu tunayoifanya huko hivi sasa inahudhuriwa na watu wengi sana kuliko ilivyokuwa zamani na ushiriki wao kwenye mikutano hiyo inatia moyo. Hivi sasa Lukuvi yuko kwenye jimbo analoliwakilisha la Isimani akieneza propaganda kwamba CHADEMA ikishinda 2015 itakubaliana na Ushoga kwa sababu ina ushirikiano na Conservative ya Uingereza. Haya mambo ya Lukuvi kutapatapa yasingeweza kufanyika au kuhangaika nayo miaka 5 iliyopita kwani watu wa vjijini waliamini CCM ni serikali na Serikali ni CCM.
Mkuu hongereni sana kwa kazi nzuri mliofanya ukanda ule,Nilipita mwezi jana njia ya Nyabula mission, Lupembe lwa Senga, Ng`enza, Mawambala hadi Winome, nikaona Bendera za CDM zinapepea, nikapata mashaka kama kweli wale watu wanamaanisha. Kumbe kweli wanamaanisha. Zile zilikuwa ngome za magamba miaka nenda miaka rudi.
 
..mimi nitapenda tufike mahali chama tawala, iwe CUF,CDM,CCM, etc kiwe na very slim majority bungeni.

..hali hiyo itaweka mazingira ya kuheshimiana baina ya vyama vyenyewe, na baina ya mhimili wa bunge na serikali.
 
Cha maana kwangu ni pale tunapoona sasa tumeanza kupata ushindi mkubwa kama huo huko vijijini. kwa taarifa yako hata kule tulikoshindwa tumeshindwa kwa tofauti ndogo ya kura!!
Mkuu sio tofauti ndogo,Magamba walichakachua
 
Dua la kuku halimpati mwewe. Hivi mnafikiri ni rahisi ki hivyo. Oteni ndoto za mchana wa saa nane tu!! CCM GARI KUBWA. Ndio maana tunasema na nyie mnajua kuwa CCM Ni No 1.

Thanks and Regards,

Kada wa CCM.
Hakika CCM ni # 1 lakini kwa RUSHWA na UFISADI
 
Back
Top Bottom