Tumeshindwa Kupambana na UJINGA, UMASIKINI NA MARADHI, na sasa wameongezeka Maadui watatu

Ni jambo la kusikitisha kuwa raia wasio na hatia wanaendelea kupoteza maisha yao.Hii ni kutokana na kiburi cha CHADEMA kutotaka kutii amri halali za dola.
Hivi,CHADEMA mtaanza lini kuona uchungu kwa raia hawa kupoteza maisha yao bila sababu?
Mliambiwa sensa inaendelea,msimamishe M4C yenu hamkusikia.
Angalieni msije geuka chama cha mauaji.

Mjinga wewe!
 
Unyama huu unaofanywa na kuratibiwa na viongozi na wafuasi wa Cdm mpaka lini? Angalia walivyomfanya mwandishi wa Channel ten Iringa. Nimeona walivyomwaga utumbo wake sijaamini nikionacho"..........
Mbona hao viongozi wa chademawanaoratibu haya mauaji hawakamatwi?
 
Ni jambo la kusikitisha kuwa raia wasio na hatia wanaendelea kupoteza maisha yao.Hii ni kutokana na kiburi cha CHADEMA kutotaka kutii amri halali za dola.
Hivi,CHADEMA mtaanza lini kuona uchungu kwa raia hawa kupoteza maisha yao bila sababu?
Mliambiwa sensa inaendelea,msimamishe M4C yenu hamkusikia.
Angalieni msije geuka chama cha mauaji.

Unaf...rw.... Mods hupenda mada kama hizi ili wachukue 10% kutoka kwa wasira......:director:. Nasubiri ban........
 
Unyama huu unaofanywa na kuratibiwa na viongozi na wafuasi wa Cdm mpaka lini? Angalia walivyomfanya mwandishi wa Channel ten Iringa. Nimeona walivyomwaga utumbo wake sijaamini nikionacho"..........

Asante "Kipofu wa Akili"
 
Ni jambo la kusikitisha kuwa raia wasio na hatia wanaendelea kupoteza maisha yao.Hii ni kutokana na kiburi cha CHADEMA kutotaka kutii amri halali za dola.
Hivi,CHADEMA mtaanza lini kuona uchungu kwa raia hawa kupoteza maisha yao bila sababu?
Mliambiwa sensa inaendelea,msimamishe M4C yenu hamkusikia.
Angalieni msije geuka chama cha mauaji.
Dhambi hiyo haiwezi kuishia hapo, lazima watu wataendelea kufa sana huku, Jeshi la Polisi likitupiwa lawama, lakini ukweli ni kwamba, CDM wanahitaji kujitafakari na kuona umuhimu wa kutafuta njia mbadala ya kujiimarisha kwani hii ya maandamano itazidi kuwamaliza watanzania.
 
Mbona hao viongozi wa chademawanaoratibu haya mauaji hawakamatwi?

Hiyo ndiyo roho ya Shetani, siku zote shetani anajificha sana, Hawa viongozi wa CDM sasa wanaonekana kama mizimu fulani hivi, wanalianzisha wao, lakini wanakufa wengine.
 
Huku vita ikiwa mbichi ya Kupambana na maadui watatu, ambayo tunazidi kushindwa kadiri ziku zinavyosonga, sasa wameongezeka maadui wengine wabaya watatu. Maadui hao ni CCM, UFISADI na POLISI.

CCM wanajua siku zao zimekaribia ukingoni, kwa maovu waliowafanyia watanzania, na wanayoendelea kuwafanyia watanzani, wanaamini kuwa siku wakitoka madarakani hawatakuwa na kwa kukimbilia. Kutokana na hili sasa wameamua kuonyesha sura yao kamili. Wamegeuka sasa kutoka kutangaza sera na kuwahudumia wananchi na kuanza kupambana na wananchi na kuhakikisha kwamba wananchi hawana nchi tena, hawana pa kukimbilia. Wananchi hawana haki ya kuandamana, hawana haki ya kuonyesha hisia zao, hawana haki ya kukutana kuzungumza matatizo yao. Kama CCM wanafikiri wataweza kuzuia hili vugu vugu la mabadiliko wajue wamechelewa mno.

Huu woga wa CCM umewafanya kuzalisha maadui wengine wawili wakubwa wa wananchi. Kwanza wamezalisha ufisadi, kila aliyeko kwenye serikali hii dhalimu ya CCM anahakikisha kwamba anajilimbikizia mali za kutosha ili mambo yakiharibika aweze kukimbilia popote duniani anapotaka. Wakumbuke dunia hii ni ndogo sana, hizo pesa wanazoficha huko uswisi na kwingineko zitajulikana tu na hivyo wasijidanganye kwamba zitawasaidia chochote.

Pili wamezalisha adui Polisi. Hii ni mbinu ambayo wameamua kuitumia ili kutisha wananchi wasishiriki vugu vugu la mabadiliko. Polisi badala ya kuamriwa kulinda raia na mali zao, sasa wameamriwa kuua raia na kuharibu mali zao. Hawana hata chemba ya huruma, wameua watu wasio na hatia, wameharibu na kupora mali za raia, wamejivika ujambazi huku wakilindwa na wakubwa zao, na ole wake atakaesema askari fulani ni jambazi, asubuhi atajikuta kajinyonga - ukistaajabu ya Musa utakutana na ya Firauni. Polisi wamekuwa walinzi wa mafisadi na wezi wa mali za nchi hii. Wameua watu migoni kulinda maslahi ya watu wanaotuibia rasilimali zetu. Sasa wamegeuka kuua raia wanaotaka kuonyesha hisia zao kwa jamii. Nchi yangu Tanzania unakwenda wapi.

Tutakimbilia wapi sisi. Bahati mbaya sana Dunia yote sasa imetugeuka. Mafuta yetu na gas yetu imewafanya Jumuiya ya Ulaya na hata Marekani kuvaa miwani myeusi na kuweka pamba masikioni wasisikie kilio cha watanzania, wasione mateso wanayoyapata watanzania kutokana na utawala huu dhalimu wa CCM. Serikali ya CCM inaingia mikataba ya kitapeli na hawa watu ili waendelee kuchukua rasilimali zetu zinazozidi kuongeza siku hadi siku, wasingependa nchi hii ichukuliwe na watu wenye uchungu na rasilimali zao. Nchi hizi zinajua mikataba hii ya kilaghai ikiisha hawatakuwa na sehemu ya kukimbilia kupata rasilimali hizi bure, kwani ni Tanzania tu ndio inazigawa kwa ujira wa 10% zinazofichwa Uswisi. Kwa hiyo wanajifanya hawaoni, hawasikii na wala hawaguswi na mauaji haya ya raia wasio na hatia. Nchi hizi za Ulaya hutasikia zikikemea hii dhuluma na ubakaji wa demokrasia, badala yake wataendelea kusifu viongozi hawa walevi wa madaraka na kutupa misaada feki inayozidi kutuangamiza kila siku. Misaada wanayolipa Jeshi la Polisi ni ya kuhakikisha hakuna mabadiliko nchi hii ili waendelee kuiba. Tutakimbilia wapi sisi. Nadhani Mungu yupo nae atatupigania, Ni yeye tu amebaki kimbilio letu. Bado sijaacha kuamini kwamba sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.

Mimi naamini damu za wote waliokufa kutetea rasilimali za nchi hii, zitaibadilisha nchi hii na kurudisha rasilimali za nchi hii mikononi mwa wengi, zitarudisha haki na kuondoa udhalimu, zitafanya tupambane vilivyo na wale maadui watatu wa mwanzo. AMEN.

Watanzania tusifanye mambo eti kutaka kuonesha dunia kuwa kuna uonevu. Hivi kufungua tawi la chama lazima kuitisha maandamano?
 
Tuongeze maombi na sala

Mkuu maombi na sala havisaidii kwa sasa, solution ni kuondoka nyuma ya keyboad na kuamua kwa vitendo. Misri na Libya hawakuhangaika na maombi, waliamua kuondoka na kufanya kwa vitendo. Acha woga
 
Back
Top Bottom