Tumeridhia muendelee kututawala lakini sio kutuona wajinga

Seif Kazige Mbambizi

Senior Member
May 7, 2016
135
92
Serikali zipo katika kila nchi hapa duniani isipo kuwa katika nchi chache zenye matatizo ya kisiasa na migogoro isiyo kwisha. kwa kiasi kikubwa nchi nyingi kwasasa zinajaribu kuhama kutoka katika mifumo ya kiimla na kuelekea katika kujenga mifumo ya kidemocrasia na utawala wa sheria ili kuzifanya serikali husika kufanya shughuli zake kwa kuheshimu misingi ya haki za binadamu kwa watu wake wote.
Mkataba wa maridhiano baina ya serikali na wananchi wake unafungwa kwa njia ya sanduku la kupigia kura katika kipindi cha uchaguzi mkuu. Ni kutokana na maamuzi ya wananchi ndipo tunapo pata serikali itakayo ongoza nchi kwa kipindi kilicho wekwa kisheria, kwa upande wa Tanzania uhai wa serikali moja ni miaka mitano tu baada ya hapo tunarudi tena kwenye uchaguzi na wananchi wanapata fursa nyingine ya kuchagua serikali mpya au waendelee na ile ile ya zamani.
Kitendo cha wananchi kufanya maamuzi ya kuchagua serikali na kuifanya iongoze dola yao hakiwafanyi wananchi katika nchi husika wapoteze uhuru wao, hakiwafanyi wananchi katika nchi husika wanyoshe mikono na kuiachia serikali iwaamulie kila kitu hata kama hakina maslahi katika maisha yao.
Ni wajibu wa wananchi kuendelea kuisimamia serikali yao na kuikosoa wakati wowote inapoteleza na kufanya maamuzi yasiyo sahihi ili iweze kurudi kwenye mstari. Kazi hii sio ya kuwaachia wanasiasa pekee, ni kazi inayopaswa kufanywa na wananchi wote na kwwa nguvu zao zote usiku na mchana ili kuifanya serikali yao iwe makini katika kutekeleza majukumu yake bila kuwa fanyanyasa raia wake. Niwajibu wetu kujua kama serikali yetu iko sahihi au inakwenda nje ya mstari ili tuweze kuishauri nini cha kufanya kwa maslahi ya taifa letu
 
Back
Top Bottom