Tumekwisha

Arsenal

Senior Member
Aug 12, 2008
190
71
wakuu hii imekaa vp? mana naona sasa serikali haitutakii mema!!uyu mtu mmoja akigoma au wafanyakazi wake wakigoma je? tutapata mafuta wapiiii???kwanini serikali nayo isiwe na taasisi mojawapo inayoagiza mafuta ili iwe kama backup ya sisi wanyonge???? someni below...TIPER mpo wapi???



MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA), imesema sheria mpya ya kudhibiti uingizaji wa nishati ya mafuta itaanza kutumika hivi karibuni.

Sheria hiyo mpya ya mafuta iliyopitishwa na Bunge mapema mwaka huu, inaainisha utaratibu mpya wa kuingiza na kuagiza mafuta nchini, ambao utakidhi mahitaji ya mafuta na kufuata sheria bila kuumiza mtumiaji wa bidhaa hiyo.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mdhibiti Uchumi kutoka EWURA, Felix Ngamlagosi, alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake mwishoni mwa wiki.

Ngamlagosi, alisema hatua hiyo inakuja baada ya Bunge kupitisha sheria mpya ya Mafuta ya mwaka 2008, ambayo itaruhusu serikali kuandaa utaratibu mzuri wa kuingiza bidhaa hiyo nchini kwa bei nzuri na kutangaza tenda kwa wafanyabiashara wa sekta hiyo.

Alisema bei ya mafuta inapanda kila mara kutokana na utaratibu mbovu wa uingizaji wake nchini. “Katika utafiti wetu tuliofanya tuligundua kuwa kuna upungufu kwenye ununuzi wa mafuta, gharama nyingi zinaweza kuondolewa kama kazi ya kuangalia utaratibu mpya itafanyika.

“EWURA ndio tunaoratibu mchakato huo, tupo kwenye hatua za kumleta mtaalamu na mshauri, tumeona hili suala la mafuta ni tete na lisilete shida tena, tumeshatangaza tenda ya kumtafuta mshauri,” alisema Ngamlagosi.

Aliongeza kuwa mfumo huo ni wakuboresha kuondoa na matatizo ya bei za mafuta katika soko na kufanya bei za mafuta kufanana sokoni. Utaratibu huo utawezesha serikali kutangaza tenda ya kuingiza mafuta nchini kwa kampuni moja itakayoshinda tenda na kuingiza mafuta kulingana na mahitaji ya nchi nzima kwa miezi sita.

Kutokana na hatua ya kuwa na mwingizaji aliyeidhinishwa, bei ya mafuta itakuwa wazi kwa sababu itajulikana kutokana na gharama za kutolea bandarini na itakuwa raihisi kwa serikali kudhibiti kupanda kwa bei za mafuta kila mara.

Aidha, kukiwa na meli moja ya mafuta nchini, itarahisisha kazi ya kupakua kwa wakati na kuondoa msongamano wa meli ndogo ndogo ambazo huleta mafuta kidogo na wakati mwingine kuchelewa kupakua kutokana na foleni.

Makampuni ya mafuta na wafanyabiashara watapaswa kuagiza mafuta kutoka kwa mwenye tenda hiyo na ataingiza kwa bei moja na kueleza nchi alikonunua mafuta hayo.

Alisema, utararibu huo utaisaida serikali kumsimamia mwingizaji kwenye suala la bei kwa sababu hivi imekuwa vigumu kutokana na kila kampuni ya mafuta kuingiza meli ya mafuta nchini.

“Tatizo la waletaji wa mafuta ni zaidi ya 25 na wasambazaji wa wanafikia zaidi ya 700 idadi ya watoa huduma ni kubwa na hata udhibiti wake ni mdogo kwa sababu kila mmoja anasema bei yake kulingana na anako yapata mafuta hayo.

“Mwingine anayapata Kenya, mwingine Uarabuni, wakati tunaweza kuwa na mtu anayeenda na meli kubwa ya kutosheleza miezi sita akaleta mafuta kwa bei nzuri na kusambaza kwa wateja kwa muda unaotakiwa na kufuata mengine kwa wakati,” alisema.

Aliongeza kuwa udhibiti mzuri wa uingizaji mafuta na usimamizi utafanya kuwepo kwa takwimu za kiasi cha mafuta kilichoingia na gharama zake.
 
Back
Top Bottom