"Tumekubali kuburuzwa kupitisha bajeti ya afya"-Dr.H.Kigwangalla

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
Yafuatayo ni maoni ya Mh Mbunge Dr.HAMISI KIGWANGALLA kama ilivyokutwa kwenye fb status yake tarehe 3 june 2011.

"Ni rushwa au upofu?kamati ya kupitisha bajeti bila kujadili kwa kina ndiyo kazi tuliyotumwa kweli?wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii jana tumekubali kuburuzwa kupitisha bajeti ya afya bila ridhaa ya baadhi yetu.

Mwenyekiti sijui alinunuliwa au ilikuaje? Kisha amegomea tusijadili hoja ya hatma ya madaktari bingwa waliohamishwa kihuni.

Kweli tutafika? Cha ajabu naye ni daktari mwenzetu.

My take:mh mbunge ajaribu kuangalia mgawanyo wa budget na hatimaye ataelewa kama kuna mianya ya rushwa.

Nawasilisha.
 
Kula 5 HKigangwala, ni busara sana kuhoji matumizi na mwenendo wa wizara husika, kuwa na uwakilishi wa kamati, tungependa mambo yachambuliwe kwa kina ili iwe ni faida kwa utendaji wa wizara husika

Mimi kuna rafiki yangu doctor kasoma uhamisho wake gazetini na mkwara mziito wa kumfuta kazi asiporipoti kituo kipya, ubabe huu si mzuri, habari za uhamisho wa mtumishi unatakiwa umfikie mlengwa kwanza na si public

Ninahimiza wajumbe wote wa kamati waendelee kuhoji mapato na matumizi, haiingii akilini , hospt kubwa kama muhimbili ni chafu! Unaenda pale unapata gonjwa jingine.....
 
Kwani kamati ikiburuzwa unachukua hatua gani zaidiya kulalamika? Kama tume haina cha kufanya inapoburuzwa basi haina haja ya kuwepo.
 
Dr.kigangwalla una wajibu wa kuwaeleza wananchi ni zipi hoja zako za msingi? Kama wamekataa kukupa nafasi wasemee kwa wananchi, natambua unaelewa matatizo yanayoikumba field yako ndio maana ulihitaji fursa ukaikosa.

Does it mean hata wabunge wa upinzani walikubali kuburuzwa?
 
Yafuatayo ni maoni ya Mh Mbunge Dr.HAMISI KIGWANGALLA kama ilivyokutwa kwenye fb status yake tarehe 3 june 2011.

"Ni rushwa au upofu?kamati ya kupitisha bajeti bila kujadili kwa kina ndiyo kazi tuliyotumwa kweli?wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii jana tumekubali kuburuzwa kupitisha bajeti ya afya bila ridhaa ya baadhi yetu.

Mwenyekiti sijui alinunuliwa au ilikuaje? Kisha amegomea tusijadili hoja ya hatma ya madaktari bingwa waliohamishwa kihuni.

Kweli tutafika? Cha ajabu naye ni daktari mwenzetu.

My take:mh mbunge ajaribu kuangalia mgawanyo wa budget na hatimaye ataelewa kama kuna mianya ya rushwa.

Nawasilisha.

Hawa ndo wabunge wetu bana! Nahisi hawajitambui na hawajui wajibu wao kwa waliowachagua! Sina imani nao kabisaa.
 
Ni akina nani basi wamo kwenye kamati hii muhimu kwa afya zetu ? Vibajaj vyetu wajawazito vimeshawasili?
 
Unafiki huu wa viongozi hauna tija hata kidogo kwa taifa letu! kiongozi unashiriki kwenye maamuzi ya kikao na hadi kikao chafungwa hujapinga hoja yoyote. Baada ya hapo unakimbilia kwenye mitandao kujiondoa kwenye maamuzi yaliyofanyika. Huu si uzalendo bali ni usaliti na unafiki wa hali ya juu.

Au anafanya haya kwa kuwa anajua yeye ni mbunge wa miaka 5 tu?
 
Dr hamisi amejitoa jf au anasubiri wakati wa bajeti ya wizara husika?

Ndg. bado nimo ndani ya JF na nitaendelea kuwemo!

Sikupenda sana kuja kujadili hapa. Lakini kwa kuwa nilifanya mgomo huu publically basi naomba nitoe maelezo kidogo.

Wanaosema unafiki, hawajui maana ya uwazi. Ningeweza kuamua kunyamaza na machungu yangu moyoni na nikaenda kuikosoa na kuikwamisha bajeti ndani ya Bunge, hapo ningekuwa mnafiki na msaliti mkubwa kwa kamati yangu. Ili hayo yasitokee nimefanya mgomo na nimedhihirisha wazi hasira zangu na kutokuridhika kwangu. Sasa tumekubaliana tutakaa tena kama kamati tukiwa huku Dodoma na kuweka mambo sawa.

Kilichotokea hakikuwa sahihi kwa kanuni za utendaji za kamati za Bunge - ambazo zikiwa kazini, zinafuata kanuni zote za Bunge, kwa sababu zinafanya kazi kwa niaba ya Bunge zima!

Kilichotokea ni kwamba; Wizara iliwasilisha Taarifa ya Utekelezaji ya mwaka unaoisha na kisha mapendekezo ya mapato na matumizi kwa mwaka huu unaokuja. Tukaanza kujadili, mimi, pamoja na mambo mengine niliibuka na matatizo mawili ambayo kwenye majibu ya wizara sikuridhika.

Haya yaliwahusu madaktari bingwa 61 waliohamishwa kwa njia ya tangazo gazetini bila kupewa barua, na sasa wengi wao wamezisusa ajira hizo, wameamua kwenda kufanya kazi kwenye private sector, ambako wanalipwa vizuri zaidi na hawanyanyaswi, na wengine wanajipanga kwenda nje ya nchi kwenye green pastures.

Wizara siku zote badala ya kuwa rafiki kwa wataalamu imekuwa ikiwasukuma waichukie na waikimbie. Wataalamu wakienda kwenye private sector, wagonjwa maskini wanatibiwa na nani? La pili lilikuwa ni la usanii unaofanywa kwenye kitengo cha figo Muhimbili, ambacho Mhe. Rais amekihangaikia sana kukianzisha, sasa pale kuna mtu anakwamisha, na mimi simjui na wala sikutaka kumtaja, nilitaka kujua kwa nini mtu huyo ana-frustrate wataalamu na wafadhili wa kutoka Norway, ambao ndiyo walitupa mashine za kuchujia damu (dialysis) na wako tayari kuleta nyingine (yeye anazikataa anadai anataka kununua nyingine kwa fedha za serikali).

Chuo hiki kinataka sasa kuvunja uhusiano na kitengo hiki na kuacha kuwafadhili wanafunzi wanaotaka kwenda kusoma huko. Huduma hii si itakufa?

Pia tulijigawa kwenye vikundi kazi vya watu wachache wachache na mimi nilikuwa na wenzangu 5 tukapewa kipengele cha matumizi ya kawaida (recurrent expenditures). tulivyoanza kuchambua subvote (kifungu) ya kwanza ya administration and general, tukagundua uozo mkubwa, kwamba activities zilizokuwa kwenye MTEF haziendani na fedha zilizowekwa kwenye Randama na kwenye budget book.

Kwa maana ya Budget book ina figure za ujumla jumla, pia na randama vivyo hivyo; ili uweze kunyumbulisha na kuelewa mambo ni lazima uone zile figure za ujumla jumla zinamaanisha nini?

Na hapo unarudia kinyume nyume kule kwenye MTEF, ambamo utakuta sasa activities imeelezewa in detail. Pia tukagundua kulikuwa na copy and paste nyingi. Kikundi kazi chetu kikashindwa kuendelea na subvotes nyingine baada ya kujiridhisha kwamba bajeti haikuwa serious kama inavyopaswa.

Wizara walipokuja kusikia ushauri wetu tukawaomba warudi wakaandike MTEF nyingine ambayo iko serious kidogo na inaendana na ukweli ili sasa tuweze kuja kuendelea na kazi ya uchambuzi.

Bila shaka hata wewe unayesoma hapo umenielewa vizuri kwamba baada ya kurudi kesho yake tungetakiwa turudi kwenye vikundi kazi vyetu tuianze upya ile kazi baada ya Wizara kurekebisha MTEF, au siyo?

Sasa kilichotokea sicho! Hatukurudi kwenye vikundi kazi na badala yake Mwenyekiti akishirikiana na wajumbe wachache walianza kutetea kwamba tuelekee moja kwa moja kwenye kusoma na kupitisha kifungu kwa kifungu, na kwamba eti kama kuna mtu ana marekebisho au swali basi atauliza na atapatiwa majibu na Wizara pale pale, na hivyo tutaipitisha bajeti na marekebisho.

Wachache tuligoma na hilo zoezi likasonga mbele. Na kwa yale majibu mepesi mepesi yaliyotolewa kwa maswali yangu inakuwaje? Nikaambiwa itapangwa siku nyingine ya kusikilizwa! Sasa mimi nikashangaa imekuwaje, mbona huu si utaratibu wetu hata siku moja? Kunani?

Nikipewa muda wa kuongea, nikisimama na kuanza kujenga hoja zangu, siruhusiwi kumalizia sentensi hata moja, ilimradi tu inahusu maswali magumu! Nikaona huu si utaratibu wetu siku zote tangu nimeingia Bungeni na kwenye kamati yetu, imekuwaje leo???

Niliamua kususia kikao. Nikatoka. Maana sisikilizwi na siwezi kukaa kwenye kikao ambacho mimi haki yangu ya kusikilizwa inabanwa, sasa kwa nini mimi niwasikilize wengine?

Sielewi kulitokea nini, labda ni ugeni wa Mwenyekiti, ni upofu (sijui umesababishwa na nini), au ni nini?? Bado najiuliza.

Japokuwa wanakamati wameamua tukutane hapa Dodoma tuyaongee na kuyaweka sawa haya mambo.

Wakatabahu,
HK.
 
Unachosema ni sahihi. Hivi hawa wataalam mnawatoa wapi? hata kwenye Bajeti ya wizara mama ni madudu tu. Copy and paste na kucheza na vinamba kidogo. Bajeti ndefu inajirudirudia.
Unajua bajeti ya wizara ya afya imepungua si kama wanavyolazimisha kuonyesha imeongezeka? Hapa nazungumzia in real terms. Factor out inflation na exchange rates halafu sema hizo ajira mpya zinalipwaje? Tutafika? Zile hosp zinazojengwa itakuwaje?
 
mods naomba muongozo...hivi kanuni za facebuku zinasemaje mtu mkubwa kama hamisi kigwangala akisema uwongo kwa kujiita dokta?
Hamisi Kigwangwallah ni daktari qualified wa magonjwa ya binadamu (MD), hajiiti daktari, yeye ni daktari.
 
Ndg. bado nimo ndani ya JF na nitaendelea kuwemo!

Sikupenda sana kuja kujadili hapa. Lakini kwa kuwa nilifanya mgomo huu publically basi naomba nitoe maelezo kidogo.

Wanaosema unafiki, hawajui maana ya uwazi. Ningeweza kuamua kunyamaza na machungu yangu moyoni na nikaenda kuikosoa na kuikwamisha bajeti ndani ya Bunge, hapo ningekuwa mnafiki na msaliti mkubwa kwa kamati yangu. Ili hayo yasitokee nimefanya mgomo na nimedhihirisha wazi hasira zangu na kutokuridhika kwangu. Sasa tumekubaliana tutakaa tena kama kamati tukiwa huku Dodoma na kuweka mambo sawa.

Kilichotokea hakikuwa sahihi kwa kanuni za utendaji za kamati za Bunge - ambazo zikiwa kazini, zinafuata kanuni zote za Bunge, kwa sababu zinafanya kazi kwa niaba ya Bunge zima!

Kilichotokea ni kwamba; Wizara iliwasilisha Taarifa ya Utekelezaji ya mwaka unaoisha na kisha mapendekezo ya mapato na matumizi kwa mwaka huu unaokuja. Tukaanza kujadili, mimi, pamoja na mambo mengine niliibuka na matatizo mawili ambayo kwenye majibu ya wizara sikuridhika.

Haya yaliwahusu madaktari bingwa 61 waliohamishwa kwa njia ya tangazo gazetini bila kupewa barua, na sasa wengi wao wamezisusa ajira hizo, wameamua kwenda kufanya kazi kwenye private sector, ambako wanalipwa vizuri zaidi na hawanyanyaswi, na wengine wanajipanga kwenda nje ya nchi kwenye green pastures.

Wizara siku zote badala ya kuwa rafiki kwa wataalamu imekuwa ikiwasukuma waichukie na waikimbie. Wataalamu wakienda kwenye private sector, wagonjwa maskini wanatibiwa na nani? La pili lilikuwa ni la usanii unaofanywa kwenye kitengo cha figo Muhimbili, ambacho Mhe. Rais amekihangaikia sana kukianzisha, sasa pale kuna mtu anakwamisha, na mimi simjui na wala sikutaka kumtaja, nilitaka kujua kwa nini mtu huyo ana-frustrate wataalamu na wafadhili wa kutoka Norway, ambao ndiyo walitupa mashine za kuchujia damu (dialysis) na wako tayari kuleta nyingine (yeye anazikataa anadai anataka kununua nyingine kwa fedha za serikali).

Chuo hiki kinataka sasa kuvunja uhusiano na kitengo hiki na kuacha kuwafadhili wanafunzi wanaotaka kwenda kusoma huko. Huduma hii si itakufa?

Pia tulijigawa kwenye vikundi kazi vya watu wachache wachache na mimi nilikuwa na wenzangu 5 tukapewa kipengele cha matumizi ya kawaida (recurrent expenditures). tulivyoanza kuchambua subvote (kifungu) ya kwanza ya administration and general, tukagundua uozo mkubwa, kwamba activities zilizokuwa kwenye MTEF haziendani na fedha zilizowekwa kwenye Randama na kwenye budget book.

Kwa maana ya Budget book ina figure za ujumla jumla, pia na randama vivyo hivyo; ili uweze kunyumbulisha na kuelewa mambo ni lazima uone zile figure za ujumla jumla zinamaanisha nini?

Na hapo unarudia kinyume nyume kule kwenye MTEF, ambamo utakuta sasa activities imeelezewa in detail. Pia tukagundua kulikuwa na copy and paste nyingi. Kikundi kazi chetu kikashindwa kuendelea na subvotes nyingine baada ya kujiridhisha kwamba bajeti haikuwa serious kama inavyopaswa.

Wizara walipokuja kusikia ushauri wetu tukawaomba warudi wakaandike MTEF nyingine ambayo iko serious kidogo na inaendana na ukweli ili sasa tuweze kuja kuendelea na kazi ya uchambuzi.

Bila shaka hata wewe unayesoma hapo umenielewa vizuri kwamba baada ya kurudi kesho yake tungetakiwa turudi kwenye vikundi kazi vyetu tuianze upya ile kazi baada ya Wizara kurekebisha MTEF, au siyo?

Sasa kilichotokea sicho! Hatukurudi kwenye vikundi kazi na badala yake Mwenyekiti akishirikiana na wajumbe wachache walianza kutetea kwamba tuelekee moja kwa moja kwenye kusoma na kupitisha kifungu kwa kifungu, na kwamba eti kama kuna mtu ana marekebisho au swali basi atauliza na atapatiwa majibu na Wizara pale pale, na hivyo tutaipitisha bajeti na marekebisho.

Wachache tuligoma na hilo zoezi likasonga mbele. Na kwa yale majibu mepesi mepesi yaliyotolewa kwa maswali yangu inakuwaje? Nikaambiwa itapangwa siku nyingine ya kusikilizwa! Sasa mimi nikashangaa imekuwaje, mbona huu si utaratibu wetu hata siku moja? Kunani?

Nikipewa muda wa kuongea, nikisimama na kuanza kujenga hoja zangu, siruhusiwi kumalizia sentensi hata moja, ilimradi tu inahusu maswali magumu! Nikaona huu si utaratibu wetu siku zote tangu nimeingia Bungeni na kwenye kamati yetu, imekuwaje leo???

Niliamua kususia kikao. Nikatoka. Maana sisikilizwi na siwezi kukaa kwenye kikao ambacho mimi haki yangu ya kusikilizwa inabanwa, sasa kwa nini mimi niwasikilize wengine?

Sielewi kulitokea nini, labda ni ugeni wa Mwenyekiti, ni upofu (sijui umesababishwa na nini), au ni nini?? Bado najiuliza.

Japokuwa wanakamati wameamua tukutane hapa Dodoma tuyaongee na kuyaweka sawa haya mambo.

Wakatabahu,
HK.

mkuu najaribu kukuelewa.cha msingi ni kuendelea na mapambano bila kujali uko chama kipi?hoja ya msingi ni kuhusu hao madaktari ,kimsingi huu ni unyanyasaji unawapeleka specialist wilayani ambapo hakuna infranstructure ya kuwezesha kufanya kazi!MDs hawastahili kwenda huko kwani hakuna miundo mbinu
 
Sijui mh dr.hamis umeridhishwa na mwenendo wa budget ya wizara ya afya iliyopitishwa leo hii dodoma.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom