Tumejifunza nini kutokana na mafuriko?

king11

JF-Expert Member
Jun 7, 2010
327
79
Je tumejifunza nini kutokana na mafuriko yaliyotokea wiki hii katika taifa letu hasa Dar es salaam?
 
Hakuna lolote tulilojifunza kwa sababu yote yale ambayo watu tumekuwa tukiyazungumzia miaka nenda rudi yametokea. Na tushukuru kuwa hili janga la mafuriko si la maangamizi makubwa kulinganisha na tuseme Tsunami au tetemeko kubwa la ardhi nchi kavu. Haya mawili na yatupitilie mbali la sivyo tutafutika kabisa katika ramani ya dunia.

Kwa ujumla hatuko tayari kukabiliana na majanga, serikali yetu haijitambui wala kujielewa ipo madarakani kwa madhumuni gani, vipaumbele vyetu havieleweki (wametumia mabilioni kusherehekea Uhuru wakati mambo muhimu yanayogusa maisha ya watu moja kwa moja wameyatelekeza), baada ya muda na sisi wananchi wa kawaida tutasahau kila kitu, na ifikapo mwaka 2015 tutazidi kuwachagua watu wale wale watuongoze tena.
 
watu waliyafuata maji,wakayadharau maji...wakasahau maji ni hatari kuliko moto na ndio maana maji huzima moto...hebu tuache mikondo ya maji tusiizibezibe kwa kujenga kuta za kuyadivert kama yule jamaa pale kigogo sambusa!
sio kila mtu lazima ajenge dar maana mengine ni ya kujitakia kujenga kwenye ponds
Ujenzi wa madaraja uzingatie uimara wa ziada kuepuka madhara ya nature disasters kama hizi!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom