Tumechoka na zawadi ya mipira na Jezi, tunataka mtatue kero zetu

Whisper

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
502
207
Imekua ni tabia ya wabunge wengi siku hizi kutoa mipira na Jezi kwa vijana wa majimbo yao na kuanzisha ligi zenye majina yao kwa lengo la kujitangaza. Kwa bahati mbaya sana mipira hii na jezi ni low low low quality from China. Waheshimiwa, tunaomba mtatue kero zetu na hayo mengine tutafanya wenyewe. Ni viwanja vipi mlivyojenga mpaka mtuletee jezi na mipira? Vile mlivyotaifisha tu vimewashinda siku hizi tunachungia mbuzi.

Nashauri huu utaratibu ukome kwani hiki ni kizazi kingine. Tujengeeni mabweni, madarasa, majosho nk.
 
kwa kweli wanakera, ila ngoja tu, maana dawa yao tulishaipata, tunawasubiri tu waingie kwenye kumi na nane zetu tuwanyoe. tumeshawachoka. waende wakawadanganye wanawake huko na pakiti za sukari na chumvi.
 
Back
Top Bottom