Tume ya Warioba kutafuna bil. 40/-

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Kwa mwaka kila mjumbe kuvuna zaidi ya milioni 300/-

Wasio wajumbe yaani watumishi kutumia bilioni 4.3/-

Sh bilioni 2.0 kulipia nyumba wafanyakazi wa Sekretariati


Serikali imefanya kufuru ya kutenga Sh. bilioni 40/- kwa ajili ya wajumbe 34 wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba. Kwa mujibu wa kasma ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoko kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/13.

Iliyopewa jina la Vote Number 8 (Fungu namba 8), wajumbe 34 wa tume hiyo wametengewa posho ya Sh. bilioni 10 watakayolipwa kwa kipindi cha mwaka mmoja jambo ambalo baadhi ya wabunge wamesema hawaridhiki na kuhoji serikali inatafuta kitu gani kwa tume hiyo.

Wajumbe wa kawaida wa tume hiyo kwa mujibu wa mchanganuo wa bajeti, watalipwa posho ya Sh. karibu 450,000 kwa siku lakini Makamu Mwenyekiti na Mwenyekiti wa Tume fungu lao ni kubwa zaidi ambalo limeongezewa viburudisho na takrima.
Kwa mujibu wa taarifa za uchambuzi wa posho hizo, kila mjumbe kuanzia mwaka wa fedha wa Julai 2012 hadi Julai 2013, atakuwa amejikusanyia zaidi ya Sh milioni 294 jambo ambalo baadhi ya wabunge waliohojiwa na NIPASHE Jumapili walisema ni maajabu ya Firauni.

Pamoja na kuhakikishiwa kuwa na ukwasi mkubwa, pia wametengewa Sh. milioni 10 kwa ajili ya matibabu kwa wale ambao wameelezwa kuwa hawapo kwenye utaratibu wa kugharamiwa tiba na serikali.
Dau kubwa ambalo lipo kwenye bajeti hiyo kwa mujibu wa wabunge hao ambao wameomba majina yao yasitajwe, ni kutengwa Sh. milioni 250 zinazodaiwa zitatumika kwa ajili ya usafi na ulinzi wa ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Wajumbe hao 34 kutoka Bara na Visiwani wametengewa Sh milioni 10 kugharamia mazishi na kuwasafirisha wajumbe wa tume hiyo watakaofariki dunia wakati wakiwa kwenye mchakato wa kukusanya maoni.
Sambamba na hilo, tume hiyo imetengewa zaidi ya Sh. bilioni 10 kununua magari 56 ambayo sita kati yake ni Land cruiser heavy duty zenye mikonga zitakazofungwa vipaza sauti ili kukusanya watu watoe maoni yao na mengine 50 yatakuwa ni mashingingi ya kisasa maarufu kama V8. Kwa sasa tume hiyo inadaiwa kuazimwa magari kutoka Wizara ya Sheria na Katiba.

Baadhi ya wabunge waliliambia gazeti hili kuwa bajeti na idadi ya magari imepunguzwa badala ya kutumia Sh. bilioni 10 zitatumika Shilingi bilioni sita na kwamba yatakayonunuliwa ni magari 26 badala ya 56 lakini idadi ya Land cruiser heavy duty zitakazofungwa vipaza sauti haijabadilika.

Ofisi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba pia inatarajiwa kutumia Sh milioni 256 kugharamia umeme na maji ambapo kila huduma imepangiwa kugharimu karibu Sh milioni 128, yaani umeme Sh. 127,992,000 kadhalika maji nayo yamepangiwa kugharimu kiasi hicho na kuwafanya wabunge wachambuzi kuhoji sababu za gharama za umeme na maji kufanana.
Tume hiyo imetengewa posho ya takrima iliyoitwa hospitality services ya jumla ya Sh. milioni 300 huku simu za TTCL pamoja na gharama za nukushi (fax) zikifikia karibu Sh. milioni 127 wakati zile za mkononi zitawagharimu walipa kodi zaidi ya Sh. milioni 91.2.

WAFANYAKAZI WA SEKRETARIATI YA TUME

Kundi hili sio la wajumbe bali hawa ni watumishi wa ofisini watawala, wahasibu, makatibu muhtasi, wafagizi, wataalamu wa kompyuta, madereva na wengine nao wametengewa mafungu kadhaa ikiwemo posho ya kujikimu wakisafiri nayo ni Sh bilioni 4.3.

Kingine ambacho wabunge waliochambua Vote No 8 ama fungu hilo walisema kilichowashangaza ni kutenga Sh bilioni 2.0 kwa ajili ya kulipia nyumba za wafanyakazi wa Sekretariati ya Tume na kuhoji hivi wafanyakazi hao hawana nyumba jambo lililoelezewa na wawakilishi hao wa wananchi kuwa ni ulaji ambao wanasubiri kuuhoji wakati serikali ikiwasilisha bajeti hiyo.

Pia wafanyakazi hao ambao watalipwa posho ya Sh. 50,000 kwa siku wametengewa Sh. milioni 300 kwa ajili ya kununulia vifaa vya chai ambavyo havikuelezwa ni vitu gani pamoja na vitafunwa. Tume ya Mabadiliko ya Katiba inaongozwa na Jaji Joseph Warioba ambaye ni Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Jaji Augustine Ramadhani.
 
Mkuu ulikiwa hujui kwamba kuingia kwenye Tume ama Kamati yoyote ni deal? Laki tatu kwa siku kwa miezi 18, nyumba ya serikali na gari lenye dereva na mafuta; deal or no deal?

Wabunge nao naona sasa watapata nguvu ya kudai nyongeza ya posho zao.
 
ww mtoa mada acha kuwadanganya watu wenye akili zao,apo kwenye 300,000 mi sjui lakini Wamenunuliwa magari 60 sio kweli,we sema una yako ya kunyimwa boom, jipange upya apo tunekushtukia.
 
wadanganyika sie jamani tutakuwa wageni wa nani ktk dunia hii sasa hiyo ni kuwakirimu ama kuwa ziba mdomo.
 
Tusipokuwa makini JF itakuwa kijiwe cha porojo wewe usipende kuokota maneno mitaani unaleta JF, unasema wanalipwa 300,000 kwa siku ni posho tu hiyo bado mshahara wanalipwa kiasi gan?
 
Hii inaweza kuwa kweli kabisa.
Lakini hii ni EPA nyingine. Ni kweli katiba ni ya umuhimu mkubwa kwa taifa, lakini hiyo bei wanayolipwa ni msalaba kwa taifa. hebu niambieni tume hii ina wajumbe wangapi ili tukokotoe kuwa hadi wanapomaliza kazi watakuwa wamekausha hazina bei ngapi.
 
Tusipokuwa makini JF itakuwa kijiwe cha porojo wewe usipende kuokota maneno mitaani unaleta JF, unasema wanalipwa 300,000 kwa siku ni posho tu hiyo bado mshahara wanalipwa kiasi gan?

tuambie wewe, wanalipwa ngapi?
 
Source muandaaji wa malipo.

Jamani watu wanapopewa madaraka katika serikali yetu huwa kuna kamsemo "KAULA" sasa ndo nazidi kupata picha ya kauli hiyo.

Je ni watanzania wangapi wanaweza kuamini kuwa wajumbe wa kamati ya katiba wanalipwa sh. 300,000/= kwa siku katika shughuri zao toka waapishwe?

Najua sio rahisi kuamini lakini ndo ukweli wa mambo.

Na mtoa taarifa kadai kwanza tume hii haikuwa kwenye bajeti na imechangia kukwamisha baadhi ya miradi na huduma kwa jamii kwa sababu lazima walipwe na watimiziwe wanayotaka.

My concern;
Sasa kama wanafunzi wanakosa mikopo na wafanyakazi wanakosa mishahara kwa wakati kwa manufaa ya wachache tunaenda wapi????


Tuko kwenye enzi ya kujuana na kupendeleana bila kuangalia maslahi ya wengi na kizazi kijacho. Wewe kama mwanafunzi endelea kwenda makao makuu ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kudai kucheleweshwa mkopo wako ambao unatakiwa kuulipa na riba yake mara tu utakapoanza kufanya kazi. Kama hutubadilishi ukosefu wa vipau mbele vyetu tutarajie mambo ya hovyo hovyo mengi zaidi siku za usoni.
 
Huu ni ufisadi mwingine mkubwa kuwahi kutokea! Nadhani bunge lijalo viongozi wetu hasa kijana mpinga posho, Mh. Zitto atusaidie. Nchi inakamuliwa hadi utumbo!!?
 
Unashangaa nini lazima ujue kuwa hiyo ni specific assignment associated with high risk.Hii kazi ndugu ni ya hatari na ndiyo maana wamewekewa hadi walinzi.Leo ukiajiriwa na UN ukapelekwa Darful dau lake si mchezo sababu ni mazingira hatarishi.
Labda nikukumbushe tume ya Chacha Wangwe ya kukusanya maoni ya kujiunga EA kwa tanaznia walilipwa tzs.600,000.

Acha porojo subiri watutengenezee katiba ya kuja kumshitakia KIKWETE FASTAAAAA
 
Hizi tetesi zinatokana na mfumo wetu wa serikali kutokuwa na uwazi. Mi nadhani malipo na marupurupu ya hii tume yangewekwa wazi.
Nakataa kuiminisha nafsi yangu kama kweli wanalipwa TZS 300,000 kwa siku. Haingii akilini hata kidogo. Kwanza hizo hela za kila siku wanalipwa kwa majukumu gani? Ina maana hawana mshahara wa mwezi?
 
Tusilalamike wakati sisi wenyewe ndio tunaolea mfumo huu wa kulipana hela nyingi kiasi hiki kwa kazi ambazo zinahitaji uzalendo zaidi!
Inawezekana kabisa kuna malipo zaidi ya haya ambayo mtoa mada ametuambia na siku ambayo tukija kujua itakuwa tayari tumechelewa na hakutakuwa na la kufanya zaidi ya kunufaisha watu wachache ambao wanachukua kile ambacho wengi wangekipata.
 
NAmshangaa mtu anayesema kuwa kazi ya kukusanya maoni inaandamana na risk kubwa. Waweza eleza ni risk gani ambayo wajumbe hao wako prone to?
Mi kwa mtazamo wangu risk hiyo ni huko kulipwa hela nyingi kiasi hicho, na maVX ya bei mbaya waliyonunuliwa.
 
Unashangaa nini lazima ujue kuwa hiyo ni specific assignment associated with high risk.Hii kazi ndugu ni ya hatari na ndiyo maana wamewekewa hadi walinzi.Leo ukiajiriwa na UN ukapelekwa Darful dau lake si mchezo sababu ni mazingira hatarishi.
Labda nikukumbushe tume ya Chacha Wangwe ya kukusanya maoni ya kujiunga EA kwa tanaznia walilipwa tzs.600,000.

Acha porojo subiri watutengenezee katiba ya kuja kumshitakia KIKWETE FASTAAAAA

Risk haipungui kwa kulipwa hela nyingi! Tena inaongezeka maana zinaamsha hasira za wananchi!
 
ww mtoa mada acha kuwadanganya watu wenye akili zao,apo kwenye 300,000 mi sjui lakini Wamenunuliwa magari 60 sio kweli,we sema una yako ya kunyimwa boom, jipange upya apo tunekushtukia.
Only in Tanzania ambako mtu anaweza kubisha kitu asichokijuwa!!.....interesting.
 
Kumbeee, ndiyo maana yule mzee anaanguka
na kuibukia kwenye vikao anajua anachokipata.
Hujaelewa ni kwa nini mpaka leo Ezekiel Maige analalama kwamba ameonewa? je Mwakyembe hukuona alivyotoka India haraka haraka kabla hata hajamaliza matibabu ili asitemwe Uwaziri na akawashushuwa viherehere wote waliokuwa wanashabikia kwamba kawekewa sumu?
 
Back
Top Bottom