LTN USU WA MADOSO
JF-Expert Member
- Sep 14, 2016
- 1,193
- 859
Ndugu wana jf nichukue nafasi hii kwa masikitiko makubwa sana yanayofanywa na wizara hii nyeti ya katiba na sheria ambayo ni kinyume na taratibu kanuni na maadili ya kazi
Mno tarehe 29/05/2016 tume ya utumishi wa mahakama iliwaita watu waliofaulu usaili kuripoti kazini tarehe hiyo 29 mwezi wa tano walianza kazi hao waajiriwa wapya ni mahakimu ,wasaidizi wa ofisi,walinzi,watunza kumbukumbu nk takribani watu 1500 tanzania nzima walisainishwa mikataba yote ya kazi na kuanza kufanya kazi hawa watu walikuwa wanafanya kazi mikoa mbalimbali nchini ilipofika tarehe 27/06/2016 walipewa barua za kusimamishwa kazi kwa mda usiojulikana
Waliamliwa kurudi nyumbani mpaka utaratibu mwingine utakapotolewa mpaka sasa miezi mitatu imepita serikali ipo kimya na hawa watu walikuwa na kazi zao kwenye mashirika binafsi baada ya kuwaita kazini waliacha kazi kwenye mashirika hayo na kuja serikalini wengine wakiwa na familia zao mpaka sasa wanataabika hawajui hatima yao mahakama ni chombo cha kutenda haki je?
Haki ya hawa watanzania iko wapi ?
Namuomba waziri mwenye dhamana kuliangalia suala hili ili hawa watu wajue hatima yao kama kazi bado wanayo au wafanya taratibu zingine maana wanaogopa hata kusaini mikataba wakihofia mda wowote watahitajika serikali saidieni hili sawa
Mungu ibabariki Wizara ya katiba na sheria Mungu ibariki Tanzania.